Kuna watu hufa mara mbili

Kuna watu hufa mara mbili

Habari hizi usiku tulivu kama hivi ni raha sana hasa sisi tunaopenda simulizi za kutisha
 
ninacho amini yapo mengi ambayo siyaoni na siyafahamu kabisa
hufurahi pale ninaposikia jambo geni katika masikio yanguu
huu uzi swahiba nifah hujauona au ndo woga
 
Last edited by a moderator:
Kipindi kile ukimwi unaua sana. Kuna njemba iliRIP wananchi wakapanga kuzika jioni. Wakati wa ibada ya kikatoliki padre akaimwagia maiti yale maji wanasema ya baraka.... kulaaleki maiti ikapiga chafya.... Nakumbuka Padre aliyekuwa anawapa watu faraja ndio aliongoza zile mbio za marathoni... Sijawahi ona riadha ya namna ile maana hata kilema alisahau magongo akaunga msafara wa marathoni...

Maiti inatisha acheni masihara. Sijui kwanini zinamheshimu mshana jr

😱😱😱😱
 
Last edited by a moderator:
ninacho amini yapo mengi ambayo siyaoni na siyafahamu kabisa
hufurahi pale ninaposikia jambo geni katika masikio yanguu
huu uzi swahiba nifah hujauona au ndo woga

Naogopa swahiba, kifo sio mchezo ati!
Hata kusoma tu sitaki.
 
Last edited by a moderator:
Nina mashaka na madaktari wetu wanaotoa maamuzi kwamba sasa huyu mtu amekufa... Kuna jamaa alikurupuka kutoka kwenye fridge na kuingia mtaani anafahamika hapa mjini kwetu... Na ni mzima hadi Leo....
 
Nina mashaka na madaktari wetu wanaotoa maamuzi kwamba sasa huyu mtu amekufa... Kuna jamaa alikurupuka kutoka kwenye fridge na kuingia mtaani anafahamika hapa mjini kwetu... Na ni mzima hadi Leo....

Kama ilivyo kwenye makosa mengine ya kibinadamu Kama kwenye mtihani au hospital kupewa majibu ya mtu mwingine au mzazi kubadilishiwa mtoto nknk basi hata kwenye kifo ni hivyohivyo kuna watu hufa kwa bahati mbaya na wakifika kuzimu hugundlika kuwa wamekufa kimakosa na hivyo kurudishwa duniani....
 
Pendael24 kuna roho halafu kuna mwili halafu kuna ufahamu!huu ufahamu ndio kila kitu ni energy ambayo haifi

Mh twende taratibu kiongozi
Kuna mind body n soul
Is soul=to spirit?
Kisichokufa ni nini ni roho au ufahamu? Kama Conscious =mind which has all feelings n every effect in physical form mtu afapo hivi hufa ila roho ndio hubaki milele

Sasa umenichanganya uliposema ufahamu haufi nijuavyo ufahamu hufa n roho ndio haifi.niweke sawa
 
Last edited by a moderator:
Nimefuatilia mada hii. Ningependa kujua zaidi. Nami naomba unialike ktk mada yako kama wengine walivyoomba. Kuna kitu nimejifunza hapa.
 
kifo ni mara moja, hicho cha pili ni chako kupiga mateke watu waliokuwa wamezimia na madaktari kutokuwa makini kuthibitisha, teke lako huwapa mshutuko mkubwa na kufa! waziri mkuu mmoja alienda kuiona maiti ya dereva aliefariki kwenye ajali ya msafara wake, alipoikuta maiti inatoka damu alishauri itolewe mochwari na kupelekwa icu, yule dereva alitibiwa akapona!
 
Mh twende taratibu kiongozi
Kuna mind body n soul
Is soul=to spirit?
Kisichokufa ni nini ni roho au ufahamu? Kama Conscious =mind which has all feelings n every effect in physical form mtu afapo hivi hufa ila roho ndio hubaki milele

Sasa umenichanganya uliposema ufahamu haufi nijuavyo ufahamu hufa n roho ndio haifi.niweke sawa

Sawa twende na kimoja kimoja
-kimsingi body n conscious soul ndio vinaunda mind/ufahamu
-Soul /roho inapokuwa peke yake ndio Yaweza kuwa pepo/spirit
-ufahamu hufa, mwili unapoachana na roho, lakini Katika baadhi ya matukio roho hubeba baadhi ya kumbukumbu
 
kifo ni mara moja, hicho cha pili ni chako kupiga mateke watu waliokuwa wamezimia na madaktari kutokuwa makini kuthibitisha, teke lako huwapa mshutuko mkubwa na kufa! waziri mkuu mmoja alienda kuiona maiti ya dereva aliefariki kwenye ajali ya msafara wake, alipoikuta maiti inatoka damu alishauri itolewe mochwari na kupelekwa icu, yule dereva alitibiwa akapona!

Huyo alikufa Mara mbili
 
Nimesoma uzi huu from A to Z. Kuna vitu vingi binadamu hatuvijui, na tunaoamini katika Mungu tunajua Mungu kazuia tusivijue ili tusiwe na hofu ya maisha yetu na tuzidi kuwa na amani...
 
Mi niliwahi sikia hata maiti nyingine zinagoma kunyoosha miguu au hata kuvaa nguo mpaka zipigwe ndio zinakubali

Mmh hili la kupigwa hapana sijawahi kusikia, kwakuwa maiti ni kitu kinachoheshimiwa mno
 
Back
Top Bottom