Kuna watu hufa mara mbili

Nauliza.je hao maiti huwa chiu au ?huwa wanawake na waume au?huwa wamekufa kweli au wamezimia wewe unawamaliza kwa teke?
Maiti ni maiti tu zipo za kila aina inategemea marehemu alikufaje
 
Maiti inalia na kutoa kamasi?
Kweli duniani kuna mambo usikute huyu hakufa labda kachukuliwa msukule.
Hivyo wale waliomchukua walikuwa wanamfanyia vitimbwi kuwatisha ndugu zake.
 
Na kwamwono wako hiyo kitu inasababishwa na nini?
 
Nimesoma uzi huu from A to Z. Kuna vitu vingi binadamu hatuvijui, na tunaoamini katika Mungu tunajua Mungu kazuia tusivijue ili tusiwe na hofu ya maisha yetu na tuzidi kuwa na amani...

Hofu huletwa na shetani
 
Hapo pa kuisindikiza na teki pameniogopesha, Ujasiri unahitaji. Naweza kukubaliana na wewe @mshana jr kwamba ni kweli wale wanaohudumia huko akili zao zimeona mengi mpaka wamekuwa kama wendawazimu
 
hilo jipya kwangu daaah..!!
hao wahudumu ni majasiri
 
na kama ukikutana na wale ndugu zetu ambao ukianguka asubuh mchana kwishney udongoni ndo kabisaaaaaaaaa
Na hii ilikuwa imezidi hasa maeneo ya kijijini kwetu! Mtu akianguka saa tatu kufikia saa sita tani sita zipo juu yake, sasa inatokea akazimika mshikaji wangu wa kalibu kwa mida kama ya saa nne! Basi kaburi likachimwa na maandalizi yote....saa tisa msafara kwa mazishi uanze jamaa akaludi....mpaka leo yupo na anamaisha yake poa tu!
 
Hapo pa kuisindikiza na teki pameniogopesha, Ujasiri unahitaji. Naweza kukubaliana na wewe @mshana jr kwamba ni kweli wale wanaohudumia huko akili zao zimeona mengi mpaka wamekuwa kama wendawazimu
SASA HUYU MSHANA KU.NYA SIJUI TUMWELEWEJE?LEO ANAJIFANYA ANAFANYA KAZI MOCHWARI WAKATI 24HRS 7DAYS A WEEK YUPO MTANDAONI,ETI KAISINDIKIZA MAITI KWA TEKE.ANATAFUTA WATEJA WA USHIRIKINA ILI AWAUZIE VITU VYA MAITI FEKI,TUJIHADHARI NA HUYU JAMAA ANATUMIA JAMII FORUM KUTANGAZA BIASHARA FEKI.
 
Kaka nimefurahi sana kukuona live na nimejifunza tuwe tunaheshimu watu humu Jf...unaweza his I hivi kumbe mtu yupo tofauti kbisa

BE BLESSED
Poa poa Shukrani pia kukufahamu Bitoz mzee wa mabibo
 
mshana jr
Huu uzi ulipita siku nyingi kidogo ila leo umerudi. Sawa, sasa nakuunga mkono kuwa wapo wafu wafao mara mbili. Kisa changu ni cha kweli; Tulikuwa wadogo.
Mdogo wangu alikufa katika mazingara ya kutatanisha. Siku moja kabla hajafa, tuligombana nikamchapa kweli kweli mpaka akaenda jificha hadi mama aliporudi ndo alirudi na yeye. Sasa kwa sababu alijua alikosea hakushitaki kwa mama nami nikamezea.
Asubuhi akafa ghafla. Sio kwa kile kipigo bali baadaye tulisikia kuwa alilogwa na Bibi mkubwa. Marehem babu alikuwaga na wake wengi na miongoni mwao huyo mmoja ndo alimloga.
Akazikwa mchana. Usiku, jamaa alikuja; Ukawa ugomvi haswa, akaichukua fimbo ile ile niliyomchapa nayo, akanishukia ka mbwa mwizi apigwavyo. Ilibidi nipige yowe baba akanisaidi, japo hakumwona wala fimbo hakuzisikia ila ile fimbo jamaa aliiacha pale pale kitandani.
Tukio hilo halikuishia hapo. Muda ule ule baba anawaza ni nini kimetokea tukasikia kelele nyumba ya mama kule, mbali kidogo ka mita 50 hivi. Mdogo wangu mwingine karudishwa usiku huo wa manane ati ameenda kwa huyo bimkubwa kuomba chakula. Aliporudishwa usiku ule, mama alichanganyikiwa kwani nyumba ilikuwa imefungwa kwa ndani hivyo hatukujua alipitia wapi.
Alipoulizwa, akasema kuwa marehem ndiye alikuja mchukua wakaenda kula huko kwa bimkubwa. Je, hii ni nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…