Kuna watu hufa mara mbili

Kuna watu hufa mara mbili

Maiti akiamka na wewe ukamwacha tu bila kumpiga teke arudi kulala nini kitatokea? Je ataendelea kuwa hai?
 
Maiti akiamka na wewe ukamwacha tu bila kumpiga teke arudi kulala nini kitatokea? Je ataendelea kuwa hai?
Imagine akitoka akatokomea kusikojulikana si jumba bovu litakuangukia...??? Hapana siwezi kukubali ikisimama tu naituliza..... kesi za wizi/upotevu wa maiti ni noma
 
Kuna mtoa hoja alisema roho inakuwa imetoka lakini mwili unataka mambo yake yaendelee,
Sisi kwetu iliwahi tokea bibi alipofariki(bi mkubwa dadake bibi) aligoma kuingia kwenye nyumba ya mwanaye (baba mkubwa)na awali siku aliyofariki wakati wa kuosha mwanaye alitaka kuingia wanapomkogesha maiti iligoma kuoshwa(ilijibana kwenye vidole na mikono kwa nguvu)mpaka mmoja kumuomba atoke , alipotoka ilikaa sawa. Wakaja watu wakamuomba amsamehe mwanae.
Wakati wa kuzika yule baba alipendekeza maiti iingie ndani kwenye nyumba anayoishi yeye kwake kwani ndie mama yake pekee na ndiye mtu pekee aliyebaki hai kama mwanae, wakati wa kutaka kuiingiza watu walihangaika na jeneza mlangoni halikupita mpaka wale wazee wakamuomba marehemu amsamehe kijana wake. Baada ya maombi jeneza liliingia bila shida.

Watu wa karibu wanadai alimnyanyapaa mama ake mzazi kwa kumsikiliza mke kipindi ambacho yeye mgonjwa hajiwezi.
 
Unaweza kudhani ni stori za kijiweni au kufikirika lakini haya mambo yapo na uzoefu wangu wa kuhudumia wafu ulinifanya nikutane naye.

Kuna watu hufa mara mbili na mara nyingi ikiwa ni usiku, wahudumu wa mochwari wanalifahamu hili vema! Unaletewa mwili uuhifadhi kwenye jokofu lakini kwa wakati huo majokofu aidha yamejaa au kuna miili mingi inahitaji kuipanga vema kabla hujaiload kwenye jokofu.

Miili yote inayoletwa mochwari imeshathibitishwa na daktari kwa maandishi kuwa huyu ni marehemu/maiti hana uhai tena hapumui na ni mzoga lakini ukiwa kwenye harakati za kupanga hizo maiti ghafla mojawapo ya maiti inasimama wima na kutaka kupiga hatua huku macho bila kupepesa yakiwa yamemtoka pima! !! Huna jinsi unaisindikiza na teke irudi ilipokuwa na baada ya hapo hainyanyuki tena.

Mochwari kuna mengi ya ajabu ya kutisha na kustaajabisha na wahudumu wa huko wanaona mengi! Lakini kitu kisicho na majibu ni kwamba kwanini kuna maiti hua zinafufuka na kufa tena ?

Bado kuna mengi hatuyajui.
hiyo hospital,hawafanyi last office?au akifika mortuary anafunguliwa?manake nafkiria hayo macho anayatoaje ndani ya shuka?
 
Hizi nazo pombe bro mshana
d621497775f6390eb4886adc8db6b595.jpg
[emoji276] [emoji276] [emoji276] [emoji276]
 
Nimewahi kuskia kuna wahudumu wengine wanakuwa na rungu wakiona umefufuka wanakumaliza kimyakimya
 
teh teh teh teh eti unaisindikiza na teke weee dhubutu sidhani kama hata hizo nguvu utakuwa nazo zaid ya kupata kifafa cha ghafla
 
inasemekana waafrika weng tunazikan angali tu hai.wenzetu mtu anapodhaniw kufa hupimw na vipimo ver effectivenes.mfano baada ya kuchek heartbeat kuna machine i think ni kama wana ku bust kifuani kama 3times hv usiposhtuka bas ni majib tosha umekufa
 
Ukute mangi kafa siku anaenda kulipwa deni lake lazma akurupuke kifoni
 
Unaweza kudhani ni stori za kijiweni au kufikirika lakini haya mambo yapo na uzoefu wangu wa kuhudumia wafu ulinifanya nikutane naye.

Kuna watu hufa mara mbili na mara nyingi ikiwa ni usiku, wahudumu wa mochwari wanalifahamu hili vema! Unaletewa mwili uuhifadhi kwenye jokofu lakini kwa wakati huo majokofu aidha yamejaa au kuna miili mingi inahitaji kuipanga vema kabla hujaiload kwenye jokofu.

Miili yote inayoletwa mochwari imeshathibitishwa na daktari kwa maandishi kuwa huyu ni marehemu/maiti hana uhai tena hapumui na ni mzoga lakini ukiwa kwenye harakati za kupanga hizo maiti ghafla mojawapo ya maiti inasimama wima na kutaka kupiga hatua huku macho bila kupepesa yakiwa yamemtoka pima! !! Huna jinsi unaisindikiza na teke irudi ilipokuwa na baada ya hapo hainyanyuki tena.

Mochwari kuna mengi ya ajabu ya kutisha na kustaajabisha na wahudumu wa huko wanaona mengi! Lakini kitu kisicho na majibu ni kwamba kwanini kuna maiti hua zinafufuka na kufa tena ?

Bado kuna mengi hatuyajui.
Mkuu ina maana kati ya hizo maiti hakuna inayomzidi huyo mtu wa mochwari ujanja akapigwa yeye na kufa?
 
Back
Top Bottom