Kuna watu hufa mara mbili

Kuna watu hufa mara mbili

Utashangaa kuna watu wanaogopa mtu aliyekufa....
Nashindwaga kuelewa wanawaza nini na mtu aliyekufa hana lolote la kumdhuru mtu.....
 
Utashangaa kuna watu wanaogopa mtu aliyekufa....
Nashindwaga kuelewa wanawaza nini na mtu aliyekufa hana lolote la kumdhuru mtu.....
[emoji23] [emoji23] [emoji23] ni kwa vile dini ziliwaaminisha kuwa kifo ni kitu kibaya kabisa
 
Mara nyingi inategemea na mfu alikutwa na mauti ktk hali gani...??...
1471754165363.jpg
 
mshana jr ni bora ikifufuka usiipige teke ni kuirudisha wodini na nduguze wakija watakushukuru kuwa umeifufua ukaingia katika vitabu vya Guinness
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kisa kuingia vitabu vya rekodi hapana kaka..ndugu wengine sio kabisa na bado kuna hilo dubwana linaitwa serikali...utahangaishwa mpaka uione dunia chungu
 
kuna story niliwahi kuisikia juu ya mortuary technician mmoja miaka ya zamani kidogo pale mawenzi regional hospital moshi.
alikua akiingia kwenye wodi za wagonjwa na yasemekana akimwambia mtu utanifuata basi ilikua haichukui muda mtu huyo anafariki...
je jambo hili linawezekana au ni story za kahawa?


Yule zeru zeru. Nilikutaga hizo story ila sinauhakika kama ni kweli.
 
Unaweza kudhani ni stori za kijiweni au kufikirika lakini haya mambo yapo na uzoefu wangu wa kuhudumia wafu ulinifanya nikutane naye.

Kuna watu hufa mara mbili na mara nyingi ikiwa ni usiku, wahudumu wa mochwari wanalifahamu hili vema! Unaletewa mwili uuhifadhi kwenye jokofu lakini kwa wakati huo majokofu aidha yamejaa au kuna miili mingi inahitaji kuipanga vema kabla hujaiload kwenye jokofu.

Miili yote inayoletwa mochwari imeshathibitishwa na daktari kwa maandishi kuwa huyu ni marehemu/maiti hana uhai tena hapumui na ni mzoga lakini ukiwa kwenye harakati za kupanga hizo maiti ghafla mojawapo ya maiti inasimama wima na kutaka kupiga hatua huku macho bila kupepesa yakiwa yamemtoka pima! !! Huna jinsi unaisindikiza na teke irudi ilipokuwa na baada ya hapo hainyanyuki tena.

Mochwari kuna mengi ya ajabu ya kutisha na kustaajabisha na wahudumu wa huko wanaona mengi! Lakini kitu kisicho na majibu ni kwamba kwanini kuna maiti hua zinafufuka na kufa tena ?

Bado kuna mengi hatuyajui.

Kaka hapo kwenye kumalizia na teke, kazi nyingine zinahitaji uwe na roho mbaya na ujasiri uliopitiliza
 
Huyo anaekufa mara mbili atakua ana unfinished business... Hata ya yule mzee wa unfinished business itatokea ivo ivo
 
Back
Top Bottom