Angekuwa anawalazimisha watoto wako kuja kwake kucheza hapo ungetilia shaka. Ila sababu kakataza watoto wake mwenyewe kucheza na wako (yawezekana kuja kwako anawakataza) hayo ni maamuzi yake uyaheshimu. Unless utueleze kama wakipatwa na lolote wajibu ni juu yako au juu yake mzazi wao.
Nilipokuwa mdogo jirani yetu mwarabu alipiga marufuku watoto wake kucheza na sisi. Mwanzoni nilikuwa nasikitika, baada ya kukua nikaelewa kwanini.
Niliwahi enda kwa relative likizo ya chuo mkoa mwingine nikampa mdogo wangu hela akanunue biscuit dukani. Mama yake kumuulizia tu akawahi kumfuata dukani. Nikaambiwa wao watoto wao huwa hawawapi hela bali wananunuliwa wanachotaka (sera yao ni kutozoesha watoto hela, na kutowapa kila kitu kwa wakati hata kama uwezo upo), pili hawatoki nje ya geti wanaweza ibiwa, kutekwa au kung'atwa na nyoka maana wako nje ya mji na nyoka ni wengi mkoa ule na kuna matukio ya utekaji.
Sasa ukikurupuka ukampangia mzazi malezi wakati hajavunja sheria wala amri za Mungu unakuwa unathibitisha kwanini anakataza watoto wake wasikuzoee.