Kuna watu wanaamini kuwa upinzani ni utakatifu na kuwa CCM ni unajisi. Ukweli ni kuwa chama hakimfanyi mtu kuwa Mtakatifu au najisi

Kuna watu wanaamini kuwa upinzani ni utakatifu na kuwa CCM ni unajisi. Ukweli ni kuwa chama hakimfanyi mtu kuwa Mtakatifu au najisi

Hapo kuna watu 2 katika vyama,kuna viongozi na wananchama.wanachama wengi wema wapo but hakuna kiongozi yoyote mwema kwenye vyama either CCM or CDM na sio kwa vyama vyetu tu ni Duniani kote.
Politics ni mchezo mchafu.
 
Kwani hapa Duniani uliona chama gani hakitumii hilarious na mbinu chafu kubaki madarakani???
Nitaanza europe haswa UK na ireland, omna uzoefu napo huku. Siasa za kwa asilimia kubwa very clean, kurushiana maneno kupo but hawajafika magnitude ya kuuana na kufanyiana hila chafu, utashinda kwa hoja na sera tu
i am not say ni watakatifu but wako far above kulinganisha na siasa za tanzania
 
Wema wa upinzani utapimwa siku ukishika madaraka na sio sasa wakiwa hawana hayo madaraka.

Sikatai kuwa CHADEMA wapo watu wema Pia lakini kulinganisha wema wa CCM na CHADEMA haipo Sawa kabisa kwa sababu hawajawahi kuwa katika nafasi na kiwango Sawa
Kwani nini lengo la post yako,mbona inamwelekeo wa kulinganisha mema na mabaya ya pande zote mbili upande wa chama tawala na upande wa upinzani?.
 
Watu wema popote pale hapa duniani ni Wachache.
Sio kwenye vyama vya siasa tuu Bali hata kwenye taasisi zingine za kidini.

Mtu mwema chamani inategemewa na majukumu yake.
Katiba ya chama ndio muongozo WA wanachama na sio Tabia za wanachama
Kwa sababu ya ujinga na upuuzi wa halaiki, katiba haziheshimiwi, kuanzia kwenye vyama hadi taifa. Matokeo yake tabia za viongozi huongoza kwa asilimia zaidi ya 90.
Viongozi wakiwa waovu, uovu huongezeka, wakiwa wema vivyo hivyo tabia hiyo hutawala.
 
Ila kiukweli kuna chama ni najisi kabisa hata Mola anakijua!
Kipo tyr hata kuua achilia mbalia wizi, dhuluma na unyanyasaji!
 
Habari za Sabato!

Kuna watu wanaamini kuwa watu wote wa CCM ni Najisi, wezi, majambazi, mafisadi yaani kitendo cha kuwa CCM wanaamini wewe ni muovu. Jambo ambalo sio kweli

Wakati huohuo wanaamini kuwa chama cha upinzani kama CHADEMA ndio kuwa Mtakatifu au mzalendo wa taifa. Jambo ambalo sio kweli.

Majizi, waovu, na madikteta wapo vyama vyote. Ubaya hauna chama kama vile ubaya hauna kwao.

Watu wema wanaweza kuwa chama chochote tuu. Wapo CHADEMA wema, na wapo CCM wema.
Wapo CHADEMA wabaya na wapo CCM wabaya.

Wapo wanaccm wanaamini kuwa mpinzani au kuwa CHADEMA ni kuwa muasi, mhaini, pingapinga na Muda wowote unaweza kuangusha serikali. Jambo ambalo sio sahihi.
Kumbe unaweza kuwa CCM na ukawa Muasi, mhaini, na pingapinga na Muda wowote unaweza kuiangusha serikali.

Hoja ni nini?

Kila chama kinaowajibu wa kutambua watu wema waliopo ndani ya chama hiko ili waongoze kwa sababu wema wakiongoza taifa limepata kuanzia CCM wenyewe na upinzani.

Halikadhalika na upinzani, wawape watu wema uongozi ili hata CCM nayo inufaike na watu hao.

Mwema ni mwema hata awe CHADEMA au CCM. Awe muafrika au Mzungu.
Na mbaya ni mbaya hata awe CHADEMA au CCM. Awe muafrika au mzungu.

Nawatakia IBADA Njema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa, Manzese Kanisani, Dar es salaam

..hoja yako haina uhalisia.

..kundi la WAOVU / WAHUNI ndio limeshika hatamu huko CCM.

..watu wema, waadilifu, hawana sauti wala ushawishi ndani ya CCM.

..Mazingira hayo ndiyo yanayochochea imani kwamba ukiwa CCM wewe ni muovu.
 
Back
Top Bottom