Kuna watu wanadhani Rais Samia yupo Ikulu kalala, kwa sababu walizoea 'show-off' na kelele

Kuna watu wanadhani Rais Samia yupo Ikulu kalala, kwa sababu walizoea 'show-off' na kelele

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAMA SAMIA ANAFANYA KAZI, MSIDHANI KALALA IKULU.

Na, Robert Heriel

Kuna watu wananifurahisha sana, yaani ukiwasikiliza ni kama wachekeshaji fulani hivi ambao hawajatambua vipaji vyao.
Wapo wanaosema Mama Samia hafanyi kazi, wapo wanaosema nchi inaongozwa na JK, wapo wanaosema Rais ni Mpole basi kila mtu ilimradi aseme ajualo kulingana na haki zake kikatiba.

Kundi hili linafikiri kuwa Rais Samia Suluhu yupo ikulu kajifungia chumbani amelala huku akijifunika shuka na kuota ndoto za abunuasi.
Kundi hili linafikiri kuwa Rais Samia akishachoka kulala anaamka, kisha anawasha luninga na kuanza kuangalia Tamthilia za KUFLI na THE CITY. Hahahah! Kundi lina vioja sana.

Wakati akiangalia tamthilia hizo kuna wakati huingia instagram na Facebook kuangalia yanayojiri huku mtandaoni, yaani hayo ndio mawazo ya kundi hili ambalo linafikiri kuwa Mama Samia hafanyi kazi.

Kitu kimoja ambacho kundi hili nitalitetea kufa na kupona ni kuwa lilizoea masuala ya showoff na kelele kwenye media. Kundi hili halina makosa kwa sababu lilizoea na likajua kuwa kufanya kazi kwa Rais ni kuonekana kwenye TV kila siku. Kundi hili halina makosa kwa sababu lilizoea na kujua kuwa Kufanya kazi kwa Rais ni kupiga makelele na kushushua wasaidizi wake ati hiyo ndio ishara ya uzalendo na kutetea rasilimali za taifa.

Kundi hili halina makosa kwa sababu lilizoea na kujua kuwa kuchapa kazi ni kupewa matumaini hewa yasiyo na kichwa wala miguu kwa kuambiwa nchi yetu ipo uchumi wa juu na ni nchi tajiri.

Kundi hili halina makosa kwa sababu lilizoea na kujua kuwa kuchapa kazi kwa Rais ni kumtaja taja Mungu hata bila msingi wowote. Utadhani Rais ni kasisi wa kanisa au sheikhe wa masjid. Hivyo Mama Samia kwa vile hana mazoea hayo anaonwa kuwa sio mpenzi wa Mungu, hahahah! Dunia ina vioja kweli.

Kundi hili halina makosa kwa sababu lilizoea na kujua kuwa Uchapakazi wa Rais ni kutoa matamko pasipo kujali sheria za nchi, kutoa tamko kwa jambo lolote hata lisilomhusu Rais.

Kundi hili halina makosa kwa sababu lilizoea na kujua kuwa uchapakazi wa Rais ni kuonekana yeye pekeake kwenye vyombo vya habari utadhani hakuna viongozi waandamizi.

Kundi hili halina makosa kwa sababu lilizoea na kujua kuwa uchapakazi wa Rais ni kuua na kutotoa nafasi kwa vyama vingine vya kisiasa kuwa huru kueneza itikadi zao na kutafuta wanachama wapya ndani ya chama chao.

Kundi halina makosa kwa sababu liliaminishwa na kuzoezwa kuwa uchapakazi wa Rais ni kutukana mabeberu na kujifanya kuwatunishia misuli wakati nyuma ya mgongo unawaita wahisani na kuwapigia magoti. Ati kuwatukana wazungu iliaminishwa kuwa kama ishara ya uzalendo, hahahaha! Daaah! Inachekesha sana.

Kundi hili halina makosa kwa sababu liliaminishwa kuwa uchapakazi wa Rais ni kuwatetea wanyonge hata kama wanavunja sheria, sio ajabu machinga ukamkuta anauza mbele ya duka lako kisa anakitambulisho chake cha elfu 20 wakati wewe unayatoa kodi ya malaki ya pesa ukibaki umebung'aa.

Kuna watu wanadhani Mama Samia amelala ikulu kwa sababu hawamsikii sikii kama ilivyokuwa zamani. Kuna watu hawajui kabisa kuwa Rais Samia Suluhu naye anafanya Ziara karibu kila siku lakini kwa vile yeye sio muumini wa showoff na kelele zisizo na maana yoyote, kelele zisizoleta chakula kwa wananchi anafanya kazi zake kama kawaida.

Kundi hili linadhani kuwa Rais kufanya kazi ni kuunda vipropaganda uchwara ambazo kimsingi hazisaidii wananchi wa tabaka la chini.

Wito wangu kwa kundi hili ambalo nimeshasema halina makosa, na kwa watanzania kwa ujumla ni kuwa Rais Samia Suluhu anafanya kazi sio kwa kelele zisizo na maana, na siku akipiga kelele ujue zinamaana, anafanya kazi bila showoff na siku akifanya showoff ujue zinamaana kwa kiasi kikubwa ndani ya nchi.

Sasa wewe danganywa kuwa upo uchumi wa kati wakati mfukoni mwako ni alfu lela ulela.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dodoma
 
Kupiga kelele kuna umuhimu wake kwasababu kunawaamsha watendaji waliolala, wanaofanya kazi kwa mazoea.

Hawa ndio wale wanaorudisha pesa za miradi serikalini kwa kisingizio pesa zimekosa kazi ya kufanya, kujiona mabosi kufanyia kazi ofisini badala ya kutoka kwenda field kuangalia maendeleo ya miradi, ndio maana Samia anazunguka mpaka Kariakoo.
 
Hapo ndipo tofauti kati ya MBWA na MBO inapojidhihirisha, wakati katika Management By Walking Around (MBWA) mtawala hupenda kujionyesha ili apate kusifika na kuogopeka mbele ya umma, lakini katika Management By Objective (MBO) kiongozi hupenda kufanya kazi zake kimkakati ili matokeo yenye tija na ufanisi yakapate kuthibitika mbele ya umma.
 
images (52).jpeg
 
Sawa.
Ndugu mwandishi umejuaje yote hayo uliyoyaeleza kama ni sahihi?
Unashindanae Mhe Rais au niaje?
Na hayo makundi yaliyopo wewe umejuaje kama yapo?

Punguza mkuu

Mbona sijatumia akili kubwa kujua hayo mkuu, hivyo sidhani kama swali lako la kwanza nitalijibu.

Swali la pili, mhe. mbona karibu kila siku yupo ziarani.

Makundi hayo nimeyajua kwa sababu naishi kitaa Mkuu
 
Hapo ndipo tofauti kati ya MBWA na MBO inapojidhihirisha, wakati katika Management By Walking Around (MBWA) mtawala hupenda kujionyesha ili apate kusifika na kuogopeka mbele ya umma, lakini katika Management By Objective (MBO) kiongozi hupenda kufanya kazi zake kimkakati ili matokeo yenye tija na ufanisi yakapate kuthibitika mbele ya umma.

Mkuu umeongea kitaalamu sana mpaka ukanitisha kwa baadhi ya istilahi.
Hata hivyo imeeleweka
 
Back
Top Bottom