Kuna watu wanadhani Rais Samia yupo Ikulu kalala, kwa sababu walizoea 'show-off' na kelele

Tangu Madame ameapishwa, nimejaribu kufuatilia, ukiacha zile siku ameenda Zanzibar kwenye mapumziko ya sikukuu ya Eid, siku zingine zote yupo ofisini anachapa kazi. Kwa hakika, KAZI INAENDELEA.
Tunataka kuona matokeo ya hizo kazi kwenye huduma za kijamii, mfumuko wa bei, kuimarika kwa thamani ya pesa kutoka $ 1 kwa shilingi 2300 mpaka shilingi 1,500, watumishi kua na mishahara mizuri, bei ya petroli kushuka kutoka 1,800 aliyoiacha mwendazake mpaka 1,400
 
Huyo aliyekuwa anapiga kelele kila siku zilisaidia nini?mbona kila siku alikuwa anateua na kufukuza?kama samia kwenda kariakoo ni kutokana ba watendaji kukaa maofisini, jpm ni sehemu gani ambayo hakwenda?ili kuzindua hata vi miradi vidogo, nini kimetokea kulazimisha kuifungua stendi ya mbezi wakati ilikuwa hata bado kukamilika?si bora hata hao wanaorudisha pesa, zinaonekana kumbe zilifika kuliko wakati wa jiwe, ambapo walikuwa hata hawazipati hizo pesa?huwezi ukaendesha nchi bila kufuata utaratibu wa ki bajeti ukafanikiwa, yeye alikuwa anatumia utaratibu wa kina PAPA NDAMA MTOTO WA NG'OMBE, PAPA MSOFE, MZAMILI KATUNZI, anatoa pesa za miradi majukwaani kutegemea na VIBES, lililopo!!!
 
Nakubali. Mimi nikiwa mmojawapo
Hakika mkuu tuko wengi, japo kwa muktadha wa Jukwaa huru/Jamiforums hakuna mwenye njaa.
Ujue hakuna kitu kinauma una njaa kali ukipita huku kiongozi mwenye dhamana anakuambia serikali haina shamba.
 
Hatari kiongozi Watanzania sasa wana amani mioyoni hata kama hawana mia mbili mfukoni.
Sasa wale ambao hawana amani kwa sababu ya kutokuwa na kitu mfukoni na hali wana majukumu nao wanaipataje hiyo amani ya moyo?
 
Rais hatakiwi kupiga kelele
 
Hatutaki maneno weka muziki😠!
 
Sasa wale ambao hawana amani kwa sababu ya kutokuwa na kitu mfukoni na hali wana majukumu nao wanaipataje hiyo amani ya moyo?
Suala lililopo ni kwamba hata maneno ya faraja ni sehemu ya amani kama afanyavyo mheshimiwa rais Samia.
Kuliko watu wanalia hali mbaya ya kiuchumi mifukoni, halafu unasema hawa ni majizi. Kuhusu kuwa na kitu tunaishi kwa imani kuwa kesho naweza kupata.
 
Hivi kweli kuna watu wanapata faraja kwa maneno ya mwanasiasa?
 
Hivi kweli kuna watu wanapata faraja kwa maneno ya mwanasiasa?
Ndio mkuu faraja inapatikana japo sio kwa wanasiasa wote. Ndo maana mimi nikaweka mahususi kwa rais Samia Suluhu.
Rejea kwa Watanzaia mbalimbali wanazungumziaje utawala wa mheshimiwa Samia Suluhu, linapokuja suala la faraja/furaha na ule wa mwendazake.
 
Hao faraja wanajipa wenyewe kwa sababu ya kufurahia kifo cha Magufuli hata Samia akicheka tu kwao inaweza kuwa ni faraja, hivyo ni matatizo ya kisaikolojia tu waliyonayo.
 
Baadhi ya Sera/Sheria mbovu za nchi ni kuwanyang’anya vijana uwezo.

Hapa naongelea vijana kuminywa kwa kuporwa haki zao, kunyimwa haki na kupuuzwa (hawasikilizwi). Naanza kwa Kuongezeka kwa Deni la Taifa na Propaganda mfu za Serikali, zenye lengo la kuhadaa umma ili kubaki madarakani tu. Serikali ya AWAMU YA 5 ilitamka kuwa inajenga miradi mikubwa kwa FEDHA za ndani. Asilimia kubwa ya Watanzania waliamini na kushangilia, na wale wachache wenye uelewa hawakupewa nafasi ya kuhoji. Imekuja kujulikana kuwa, FEDHA za Mifuko ya Jamii zilichukuliwa na Wafanyakazi wakaporwa haki zao za kulipwa FAO LA KUJITOA na kuchelewesha malipo ya Wastaafu.

Vijana wasomi, waliosoma sayansi na wenye ujuzi wameajiriwa kwenye Makampuni, Mashirika na Viwanda. Hizi ni talent, na hazina za wasomi kwa nchi, na walivyoajiriwa kwenye haya Makampuni na Viwanda, wamepata fursa ya kuongeza utaalamu na uzoefu. Hii ndio Econonomic interelligency ambayo Serikali ilipaswa kutumia ili kunyanyua uchumi wa nnchi through Innovation. Ajira na mikataba za hawa vijana (wenye utaalamu na uzoefu-Innovation) zilivyokoma, Serikali iliwanyima Akiba zao (PESA za NSSF). Kumbuka Serikali ilifuta fao la kujitoa mwaka 2018 na kuweka Fao la kukosa ajira. Watu wote skilled labour (wataalamu hawa), hawapewi akiba yao, Haki imepotea. Hawa watu wangelipwa fedha zao, wangeweza kujiajiri kwa kufungua makampuni, kujenga viwanda vidogo. Badala yake hawa skilled labour wanaambiwa wasubiri miezi 18 na kama hawataajiriwa, wakae hadi 55 years wastaafu.

Serikali ilitumia pesa za mifuko ya jamii (Kukopa au kupora kienyeji) ili kujenga miradi. Hapo awali serikali imesema inajenga miradi kwa pesa za ndani (propaganda)..Lakini ukweli wenyewe ni kupora haki za wafanyakazi vijana na mafao wastaafu. Pia Serikali ilikopa sana Nje na kwenye mabenki, ndio maana deni la taifa limepaa sana.

Serikali inapaswa kuwapa wafanyakazi akiba zao ili waweze kutumia skill zao na uzoefu waliopata katika makampuni/viwanda ili kufungua biashara mpya. Hii ndio namna ya kutanua wigo wa Kodi (MWugulu NCHEMBA TRA). Mitaji itatoka wapi ya biashara mpya kwa wazawa kama mikopo benki sio rafiki? Suluhisho ni Serikali kurejesha FAO LA KUJITOA NSSF na kulipa wafayakazi akiba zao kwa Haki.


Serikali inatakiwa kuwezesha vijana, kutoa International passport kwa graduate wote, ili wapambane fursa za ajira kokote duniani. Baadae watakuwa diapora kubwa inayotuma pesa Tanzania, kama ilivyo Zimbabwe, Kenya na India walivyoenda wengi Canada na UK. Serikali kurejesha Fao la Kujitoa, Hasa kwa Sekta binafsi, kwa kuzingatia kuwa Sekta binafsi Security ya ajira ni delicate sana.
 
Hao faraja wanajipa wenyewe kwa sababu ya kufurahia kifo cha Magufuli hata Samia akicheka tu kwao inaweza kuwa ni faraja, hivyo ni matatizo ya kisaikolojia tu waliyonayo.
Sidhani kama ni faraja ya kifo cha hayati Magufuli na wala haiwezi kuwa tatizo la kisaikolojia. Maisha ya kukoromeana/kutishiana/kutoa kauli za kibabe enzi za mwendazake yalikuwa sio.

Ndo maana uongozi wa rais Samia Suluhu hakuna kugoma ni mwendo wa upole. Hapo ndo amani/furaha inapokuwepo miongoni mwa Watanzania.
 
Mama Samia ana muda mchache sana toka aingie madarakani sasa unafikiri ni yapi hayo aliyoyafanya katika muda huu ambayo yamebadili yale aliyoyafanya Mwendazake katika miaka mitano kiasi cha kuwaondolea hao watu furaha? furaha za hao watu ni tokea siku waliposikia Jiwe kafariki hata Mama samia hajaapa kuwa rais ndio maana nakwambia furaha za hao watu ni kifo cha Magufuli tu.

Mimi sishangai wewe kukataa ila ukweli ni kwamba tatizo la hao watu ni suala la kisaikolojia, pamoja na hayo mambo ya Jiwe ila hao jamaa ni kana kwamba walikuwa wanaishi Tanzania tofauti na sie wengine ndio maana wanasema walikuwa wanaishi bila furaha na amani kitu ambacho nashangaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…