Kuna Watu Wanahitaji Msaada, Ila Hawajui Namna Ya Kuomba Bila Kujidhalilisha

1995_No_Ku_Fake

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2026
Posts
1,561
Reaction score
3,328
Kuna Watu Wanahitaji Msaada, Ila Hawajui Namna Ya Kuomba Bila Kujidhalilisha

Habari wana JF,

Leo asubuhi nimeamka na wazo moja zito sana kichwani. Kuna kipindi katika maisha mtu anapitia hali ngumu, lakini jambo gumu zaidi siyo hata kukosa—bali ni kujua namna ya kuomba msaada.

Wengine wana ndugu, marafiki na watu wanaowajali. Lakini bado wanaweza kukaa kimya wakiteseka, siyo kwa sababu hawahitaji msaada, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wasumbufu, waombaji au watu wasioweza kujitegemea.

Ukweli ni kwamba maisha yana misimu. Leo unaweza kuwa na uwezo wa kumsaidia mwingine, kesho ukajikuta wewe ndiye unahitaji mtu akushike mkono.

Tujifunze jambo moja: Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone. Wakati mwingine tabasamu lake linaficha vita vikubwa sana.

Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.

Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.

Wana JF, nyinyi mnaonaje—je, mtu anaweza kuhitaji msaada mkubwa lakini akashindwa kuomba kwa sababu ya heshima au kuogopa kudharaulika?
 
Siku hizi hata kuomba msaada unahitaji uwe na network nzuri. Kama wewe ni mtu wa kukaa kimya na huna marafiki wa maana, hata ukiomba msaada kwa kupiga magoti hakuna mtu atakayekusikia. Watu wanawasaidia wale wanaowajua au wale ambao wanajua mbeleni watapata faida fulani kutoka kwao tu.
 
Kuna Watu Wanahitaji Msaada, Ila Hawajui Namna Ya Kuomba Bila Kujidhalilisha

Habari wana JF,

Leo asubuhi nimeamka na wazo moja zito sana kichwani. Kuna kipindi katika maisha mtu anapitia hali ngumu, lakini jambo gumu zaidi siyo hata kukosa—bali ni kujua namna ya kuomba msaada.

Wengine wana ndugu, marafiki na watu wanaowajali. Lakini bado wanaweza kukaa kimya wakiteseka, siyo kwa sababu hawahitaji msaada, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wasumbufu, waombaji au watu wasioweza kujitegemea.

Ukweli ni kwamba maisha yana misimu. Leo unaweza kuwa na uwezo wa kumsaidia mwingine, kesho ukajikuta wewe ndiye unahitaji mtu akushike mkono.

Tujifunze jambo moja: Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone. Wakati mwingine tabasamu lake linaficha vita vikubwa sana.

Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.

Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.

Wana JF, nyinyi mnaonaje—je, mtu anaweza kuhitaji msaada mkubwa lakini akashindwa kuomba kwa sababu ya heshima au kuogopa kudharaulika?
Mkuu umenena vyema sana. Kuna kipindi nilipitia hiyo hali aise! inakutesa kisaikolojia na kuusumbua mwili.

Unaona kabisa uwezo wa kufanya jambo unao lakini mazingira ndio yanakua magumu balaa.

Nilichojifunza ni kwamba unapopitia hali ya namna hiyo unahitaji kumkumbuka Mungu, yaani anza kusali na muulize Mungu ni kitu gani anataka kukufundisha. Ukikaa sawa na Mungu utajikuta unapata amani na milango inafunguka.

Binafsi nilijikuta nimefirisika katika mazingira tatanishi sana, nikaenda kuishi ugenini yaani nilibakiwa na elfu 50 tuu, 40k nilipanga geto nikabakiwa na 10k ya kula sikuwa na godoro Wala mkeka.

Inshort katika hicho kipindi ndio nilijifunza kuwa mtulivu, kusali pasipo kwenda kanisani, kusoma neno la Mungu, kupangilia maisha yangu, zaidi nilijifunza mimi ni nani katika Mungu.

Simshauri mtu kuombaomba sana kwa watu bali omba kwa kadiri Mungu atakavyokupa amani kwa watu wa kuwaomba.
 
Kuna Watu Wanahitaji Msaada, Ila Hawajui Namna Ya Kuomba Bila Kujidhalilisha

Habari wana JF,

Leo asubuhi nimeamka na wazo moja zito sana kichwani. Kuna kipindi katika maisha mtu anapitia hali ngumu, lakini jambo gumu zaidi siyo hata kukosa—bali ni kujua namna ya kuomba msaada.

Wengine wana ndugu, marafiki na watu wanaowajali. Lakini bado wanaweza kukaa kimya wakiteseka, siyo kwa sababu hawahitaji msaada, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wasumbufu, waombaji au watu wasioweza kujitegemea.

Ukweli ni kwamba maisha yana misimu. Leo unaweza kuwa na uwezo wa kumsaidia mwingine, kesho ukajikuta wewe ndiye unahitaji mtu akushike mkono.

Tujifunze jambo moja: Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone. Wakati mwingine tabasamu lake linaficha vita vikubwa sana.

Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.

Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.

Wana JF, nyinyi mnaonaje—je, mtu anaweza kuhitaji msaada mkubwa lakini akashindwa kuomba kwa sababu ya heshima au kuogopa kudharaulika?
Umeongea kitu muhimu sana kwenye maisha.
Unajua, kwa mtu yeyote yule aliye staarabika kuomba msaada hasa wa kujikimu huwa ni mtihani mkubwa sana.
Kuna watu wengi wanacheka na kutabasamu lakini wanapitia changamoto kimya kimya. Kuomba msaada wa kuishi ni jambo linalohitaji kujitoa ufahamu hivi....vinginevyo ni ngumu sana sio wote wanaweza.
Kama ulivyosema, kama una rafiki na unajua hali yake ameyumba, usisubiri akuombe, msaidie kama una weza na tena usihesabu umemsaidia mara ngapi, fanya kadri utakavyoweza. Maisha jinsi yalivyo, usije kuwa sehemu ya wale ambao huishia kusema ningejua ningemsaidia zaidi.
 
Sio msaada tu unaotolewa kwa utwezwaji wa utu wa mtu sikuizi hata madeni huombwa kwa unyenyekevu,utulivu na sababu yenye mashiko (ili bosi au tajiri akulipe chako kwa wakati inabidi umpe sababu kama unauguliwa,unatakwa kufuzwa ulipopanga au unaumwa nje na apo utazungushwa)
 
Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.

Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.
Nakubaliana na wewe.
 
Tunaochoogopa sio kuomba msaada ila kutagazwa unakuta mtu anasema bila mim huyo agekuwa amekufa agali alikusaidia jero tu ya dawa tatu mtu anapokusaidia anataka sifa
Lakn wapo watu wenye moyo mwema mola awabariki awajalie maisha mema milele
Wengine wanakunyima na kukutangaza wanakutangaza juu.

Kwa kifupi utapitia aibu tatu.

1)Kuomba ni aibu ya kwanza

2)Kunyimwa ni aibu ya pili

3)Kutangazwa ni aibu ya tatu

🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone.
Mkuu ngumu kujua mtu anahitaji msaada kama hauishi naye ,ebu angalia watu wanaojionyesha instagram/facebook kama mambo mazuri kumbe wanahitaji msaada mkubwa wa kifedha ,sasa mtu kama huyo utaanzaje kumsaidia wakati amepiga picha mbele ya G-wagon bila caption au yupo kwenye balcony anakunywa juice?

Kuna mtu namjua huwa ananipiga vizinga hadi vya buku 2 ila kwenye facebook anapiga picha yupo ndani ya ndinga au yupo kama ofisini mbele kuna laptop anabonyeza bonyeza ,sasa kwa mtu mwingine anaweza akajua jamaa ana mkwanja kumbe ni KAPUKU.
 
Kuna Watu Wanahitaji Msaada, Ila Hawajui Namna Ya Kuomba Bila Kujidhalilisha

Habari wana JF,

Leo asubuhi nimeamka na wazo moja zito sana kichwani. Kuna kipindi katika maisha mtu anapitia hali ngumu, lakini jambo gumu zaidi siyo hata kukosa—bali ni kujua namna ya kuomba msaada.

Wengine wana ndugu, marafiki na watu wanaowajali. Lakini bado wanaweza kukaa kimya wakiteseka, siyo kwa sababu hawahitaji msaada, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wasumbufu, waombaji au watu wasioweza kujitegemea.

Ukweli ni kwamba maisha yana misimu. Leo unaweza kuwa na uwezo wa kumsaidia mwingine, kesho ukajikuta wewe ndiye unahitaji mtu akushike mkono.

Tujifunze jambo moja: Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone. Wakati mwingine tabasamu lake linaficha vita vikubwa sana.

Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.

Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.

Wana JF, nyinyi mnaonaje—je, mtu anaweza kuhitaji msaada mkubwa lakini akashindwa kuomba kwa sababu ya heshima au kuogopa kudharaulika?
Sio Kila Mtu ni wakuomba msaada,
Tunafeli hapo tu
 
Mimi sipendi hii tabia ya mtu unamwomba pesa , halafu anahitaji umweleze shida uliyonayo kwnz,,
Unaanza kujieleza shida yko mwanzo mwisho,,
anakusikiliza unavyojieleza ila baadae anasema sina pesa.
Sasa kwann ulitaka nikueleze shida na huna uwezo wa kunisaidia?
Kwni lazima kujieleza kwko na pesa huna?
Hili jambo linadhalilisha sn utu wa mtu.
 
Maisha yamebadilika hatuishi kama jamii, tunaishi kiubinafsi siku hizi

So Ukija kuomba, tambua unajidhalilisha
 
Mimi sipendi hii tabia ya mtu unamwomba pesa ,ila anahitaji umweleze shida uliyonayo kwnz,,
Unaanza kujieleza shida yko mwanzo mwisho,,
anakusikiliza unavyojieleza ila baadae anasema sina pesa.
Sasa kwann ulitaka nikueleze shida na huna uwezo wa kunisaidia?
Kwni lazima kujieleza kwko na pesa huna?
Hili jambo linadhalilisha sn utu wa mtu.
Na kujieleza ndio kutamfanya akusaidie,mara nyingi tunaguswa kutokana na shida ya mtu,mtu akiguswa sana ndio hushawishika kukusaidia

Ila ushauri kwa wale wanao wasaidia watu ,msaidie mtu bila kumtangaza,kwanza ukitangaza unakosa thawabu kwa Mungu,toa kwa kutaka radhi za Mola wako,utapata kheri hapa duniani na kesho huko akhera
 
Kwenye nyimbo yake Justfy my thug,Jay Z alisema

"Death before dishonor and I tell you what else
I tighten my belt before I beg for help,
Foolish pride is what held me together through the years"

Tangu nimesikia nyimbo hiyo mwaka 2004 hadi leo naishi humo
 
Back
Top Bottom