1995_No_Ku_Fake
JF-Expert Member
- Aug 24, 2026
- 1,561
- 3,328
Mkuu umenena vyema sana. Kuna kipindi nilipitia hiyo hali aise! inakutesa kisaikolojia na kuusumbua mwili.Kuna Watu Wanahitaji Msaada, Ila Hawajui Namna Ya Kuomba Bila Kujidhalilisha
Habari wana JF,
Leo asubuhi nimeamka na wazo moja zito sana kichwani. Kuna kipindi katika maisha mtu anapitia hali ngumu, lakini jambo gumu zaidi siyo hata kukosa—bali ni kujua namna ya kuomba msaada.
Wengine wana ndugu, marafiki na watu wanaowajali. Lakini bado wanaweza kukaa kimya wakiteseka, siyo kwa sababu hawahitaji msaada, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wasumbufu, waombaji au watu wasioweza kujitegemea.
Ukweli ni kwamba maisha yana misimu. Leo unaweza kuwa na uwezo wa kumsaidia mwingine, kesho ukajikuta wewe ndiye unahitaji mtu akushike mkono.
Tujifunze jambo moja: Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone. Wakati mwingine tabasamu lake linaficha vita vikubwa sana.
Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.
Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.
Wana JF, nyinyi mnaonaje—je, mtu anaweza kuhitaji msaada mkubwa lakini akashindwa kuomba kwa sababu ya heshima au kuogopa kudharaulika?
Umeongea kitu muhimu sana kwenye maisha.Kuna Watu Wanahitaji Msaada, Ila Hawajui Namna Ya Kuomba Bila Kujidhalilisha
Habari wana JF,
Leo asubuhi nimeamka na wazo moja zito sana kichwani. Kuna kipindi katika maisha mtu anapitia hali ngumu, lakini jambo gumu zaidi siyo hata kukosa—bali ni kujua namna ya kuomba msaada.
Wengine wana ndugu, marafiki na watu wanaowajali. Lakini bado wanaweza kukaa kimya wakiteseka, siyo kwa sababu hawahitaji msaada, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wasumbufu, waombaji au watu wasioweza kujitegemea.
Ukweli ni kwamba maisha yana misimu. Leo unaweza kuwa na uwezo wa kumsaidia mwingine, kesho ukajikuta wewe ndiye unahitaji mtu akushike mkono.
Tujifunze jambo moja: Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone. Wakati mwingine tabasamu lake linaficha vita vikubwa sana.
Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.
Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.
Wana JF, nyinyi mnaonaje—je, mtu anaweza kuhitaji msaada mkubwa lakini akashindwa kuomba kwa sababu ya heshima au kuogopa kudharaulika?
Nakubaliana na wewe.Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.
Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.
Wengine wanakunyima na kukutangaza wanakutangaza juu.Tunaochoogopa sio kuomba msaada ila kutagazwa unakuta mtu anasema bila mim huyo agekuwa amekufa agali alikusaidia jero tu ya dawa tatu mtu anapokusaidia anataka sifa
Lakn wapo watu wenye moyo mwema mola awabariki awajalie maisha mema milele
Mkuu ngumu kujua mtu anahitaji msaada kama hauishi naye ,ebu angalia watu wanaojionyesha instagram/facebook kama mambo mazuri kumbe wanahitaji msaada mkubwa wa kifedha ,sasa mtu kama huyo utaanzaje kumsaidia wakati amepiga picha mbele ya G-wagon bila caption au yupo kwenye balcony anakunywa juice?Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone.
Sio Kila Mtu ni wakuomba msaada,Kuna Watu Wanahitaji Msaada, Ila Hawajui Namna Ya Kuomba Bila Kujidhalilisha
Habari wana JF,
Leo asubuhi nimeamka na wazo moja zito sana kichwani. Kuna kipindi katika maisha mtu anapitia hali ngumu, lakini jambo gumu zaidi siyo hata kukosa—bali ni kujua namna ya kuomba msaada.
Wengine wana ndugu, marafiki na watu wanaowajali. Lakini bado wanaweza kukaa kimya wakiteseka, siyo kwa sababu hawahitaji msaada, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wasumbufu, waombaji au watu wasioweza kujitegemea.
Ukweli ni kwamba maisha yana misimu. Leo unaweza kuwa na uwezo wa kumsaidia mwingine, kesho ukajikuta wewe ndiye unahitaji mtu akushike mkono.
Tujifunze jambo moja: Kama una uwezo wa kumsaidia mtu, usisubiri mpaka ajidhalilishe ndiyo umuone. Wakati mwingine tabasamu lake linaficha vita vikubwa sana.
Na kwa wale wanaopitia wakati mgumu, msikate tamaa. Kuomba msaada siyo udhaifu. Udhaifu ni kukata tamaa wakati bado kuna kesho.
Maisha yanaweza kubadilika kwa siku moja, ujumbe mmoja, simu moja au mtu mmoja mwenye moyo wa kukusaidia.
Wana JF, nyinyi mnaonaje—je, mtu anaweza kuhitaji msaada mkubwa lakini akashindwa kuomba kwa sababu ya heshima au kuogopa kudharaulika?
Na kujieleza ndio kutamfanya akusaidie,mara nyingi tunaguswa kutokana na shida ya mtu,mtu akiguswa sana ndio hushawishika kukusaidiaMimi sipendi hii tabia ya mtu unamwomba pesa ,ila anahitaji umweleze shida uliyonayo kwnz,,
Unaanza kujieleza shida yko mwanzo mwisho,,
anakusikiliza unavyojieleza ila baadae anasema sina pesa.
Sasa kwann ulitaka nikueleze shida na huna uwezo wa kunisaidia?
Kwni lazima kujieleza kwko na pesa huna?
Hili jambo linadhalilisha sn utu wa mtu.