Hii sababu ni 100%Kimazingira
•Upatikanaji wa Chakula Kingi: Katika mazingira ambapo chakula kinapatikana kwa urahisi na kwa wingi, watu huwa na uwezekano mkubwa wa kula kupita kiasi.
Ulafi,ama wengine wanatia kwenye fuko chini ya meza ili baadae abebe.Habari.
Juzi nilikuwa kwenye harusi ya ndugu. Wakati wa kupata chakula kuna jamaa alikuwa anakula hatarii alikula sahani saba hadi kamati ya chakula wakakataa kumpa chakula kingine alikuwa bado anadai. Nini kinasababisha mtu kula sana wataalam??
Mkali ni yule aliyemaliza dumu 3 za maji aisee nilisema uchawi upoDuu huyo ni kiboko
.mhhhmh.! mkuu hapa umezidisha chumvi acha kutufunga kamba bhana duuuh.!Tulikuwa naye 'power Mwamgiga', anakula ndoo ya wali ya lt10, galoni la maziwa, mkungu wa ndizi na creti la soda ndiyo anashiba.
Soda anafungulia ukucha.
Akitaka kubeba maji, ni pipa mbili zinajazwa halafu mzega wa kubebea ni mwamba wa nguzo za simu za Ttcl, mwanaume anaondoka nazo.
Gari mbili anazizuia kwa mkono mkavu.
Chai yake ni chai ya maziwa birika zima na mkate unakatwa kati kati kwa mkono unafinywa na kusokomezwa mdomoni, hataki silesi!
Mgekutana na mtu wa hivyo, mgelimwandika kwa kulalamika na kujaza server.
Wapi palipozidi nipunguze?.mhhhmh.! mkuu hapa umezidisha chumvi acha kutufunga kamba bhana duuuh.!
Kula ni starehe yanguKama una utani na Vishu Mtata sawa
Watu wanakula usibishe sema hujawahi kukutana naoHaiwezekani mtu kula sahani saba, nabisha.
TungewakimbizaNdo watokee watu 10 kama huyo mwamba apo mngeikimbia sherehe
Nawajua wasukuma kwa kushika unga wanajitahidiNjoo huku shinyanga uone watu wanavyokupigia ugali
Siyo rahisi sahani 7.Habari.
Juzi nilikuwa kwenye harusi ya ndugu. Wakati wa kupata chakula kuna jamaa alikuwa anakula hatarii alikula sahani saba hadi kamati ya chakula wakakataa kumpa chakula kingine alikuwa bado anadai. Nini kinasababisha mtu kula sana wataalam??
Kweli japo sio rahisiSiyo rahisi sahani 7.