kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Kuna watu wanavizia kila kitu anachoongea Samia kama Rais, Nchimbi kama makamu wa Rais na Mwigulu kama Waziri Mkuu wa Tanzania na kukigeuza ili ionekane kana kwamba Samia, Nchimbi na Mwigulu hawapo pamoja, lao sio moja na hawaendi njia moja. Hizi ni siasa za bei rahisi sana za watu waliochoka sana safari ya siasa.
Kinachowaashangaza watu hawa ni kuona hauchi kunakucha na taifa linasonga mbele kama vile hakuna kilichotokea. Ilikuwa October 2025 uchaguzi ulifanyika na sasa ni April 2026, miezi 6 sasa hakuna hili wala lile kwa viongozi hawa wakuu 3. Watavizia kama fisi anavyovizia mkono wa binadamu udondoke autafune.
Wanasubiri Samia kasema nini, nchimbi kasema nini na mwigulu kasema nini ili waseme "amemsema yeye".
Wanawachonganisha wapigane, tunalijua hilo, tafuteni lingine.