Kuna watu wanatembea na mizigo mizito kichwani ukipata nafasi wasikilize

Kuna watu wanatembea na mizigo mizito kichwani ukipata nafasi wasikilize

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Leo nikiwa katika usafiri wa jamii baba mmoja mwenye plasta jichoni alinisalimia vizuri tu na kuniuliza ninapoelekea. Ni wazi kuwa alikua anatafuta mtu wa kuongea nae ila asichokijua ni kuwa ninashare story humu jukwaani hasa mikasa halisi ya watu.

Huyu bwana alidumu kwenye ndoa kwa miaka 28 na binti yao wa kwanza mwenye miaka 27 alishaolewa harusi na anaishi kwa mume wake. Mzee mwenyewe alikua dereva wa Malory makubwa ya kusambaza bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Uchumi wao si haba waliishi katika nyumba ya kisasa aliyoijenga kwa pesa yake. Binti yake akiwa na ujauzito wa tatu kuna jirani aliyemuonba wakutane bar ya jirani kwa mazungumzo. Wakiwa bar jirani alinunua round ya kwanza na soup ya kongoro walipata supu na chapati huku jirani akiongelea uchumi wa nchi na bei ya vitu kupanda.

Walipata round ya tatu na kuku wa makange, alimuuliza jirani yaani umeniita kuja kuninunulia chakula? Jirani alimtaarifu kuwa yale yalikua ni maandalizi kwani alikomuitia ni zito. Mwisho alifunguka kuwa unafahamu mume wa binti yako ndiye Ben-10 wa mke wako? Mzee anasema ilichukua kama dakika tano hivi yale maneno kuingia akilini.

Jirani alimfahamisha kuwa akiwa safari, mkwe mkwee anatawala nyumba yake na majirani humuona a vyoingia na kutoka, huwa anatoka saa nane usiku kwake anakwenda kuitokia roll call kuwa alilala pale. Jirani aliendelea kuwa mkewe ni mwerevu sana katika kuficha hili, ukimuuliza atakataa na anaweza kubadilisha mbinu. Kama una moyo panga mtego wa kuwafuma.

Ni kweli mzee dereva aliaga ana peleka mzigo DRC Congo kumbe amechukua chumba guest mpaka saa tano sita ndiyo akaibuka nyumbani. Mtego ulinasa mkwe akiwa katika matrimonial bed ya wakwe hakuwa na Pa kukimbilia. Walizichapa sana na mkwe alimrushia ngumi baba mkwe jichoni iliyomuumiza sana wakati huo mke akitoka kuomba msaada.

Nyumbani binti alipoyasikia ujauzito uliharibika kwa shock, na binti aliapa kumuua mama yake. Mwisho binti alipata mental breakdown na ilibidi atibiwe hospitali maalum ya akili kwa muda mrefu, bibi alipewa wajukuu awalee na ndoa zote mbili zilivunjika.

Sikufahamu zaidi ya hapa kwani basi lilishafika Kwamtogole ambacho ndiyo kituo changu.
 
hiyo haina tofauti na mke kumfuma baba watoto wake akitafunwa bila kachumbari
 
Ndivyo mlivyo wanawake bora yako ww umepata kusimuliwa sisi yanatukuta alafu mwisho wa siku tunakufa kwa kihoro na siri zetu moyoni, kuna kitabu kina cover nzuri kweli alifu kimeandikwa hivii ALL YOU KNOW ABOUT WOMEN kubwa kama vile BIBLE ukiifungua ndani unakutana na page tupu hkna maandishi! Maana yake ni kwamba hkna abuse kuhusu mwanamke
 
Back
Top Bottom