Kuna watu wanatembea na mizigo mizito kichwani ukipata nafasi wasikilize

Leo nikiwa katika usafiri wa jamii baba mmoja mwenye plasta jichoni alinisalimia vizuri tu na kuniuliza ninapoelekea. Ni wazi kuwa alikua anatafuta mtu wa kuongea nae ila asichokijua ni kuwa ninashare story humu jukwaani hasa mikasa halisi ya watu.

Huyu bwana alidumu kwenye ndoa kwa miaka 28 na binti yao wa kwanza mwenye miaka 27 alishaolewa harusi na anaishi kwa mume wake. Mzee mwenyewe alikua dereva wa Malory makubwa ya kusambaza bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Uchumi wao si haba waliishi katika nyumba ya kisasa aliyoijenga kwa pesa yake. Binti yake akiwa na ujauzito wa tatu kuna jirani aliyemuonba wakutane bar ya jirani kwa mazungumzo. Wakiwa bar jirani alinunua round ya kwanza na soup ya kongoro walipata supu na chapati huku jirani akiongelea uchumi wa nchi na bei ya vitu kupanda.

Walipata round ya tatu na kuku wa makange, alimuuliza jirani yaani umeniita kuja kuninunulia chakula? Jirani alimtaarifu kuwa yale yalikua ni maandalizi kwani alikomuitia ni zito. Mwisho alifunguka kuwa unafahamu mume wa binti yako ndiye Ben-10 wa mke wako? Mzee anasema ilichukua kama dakika tano hivi yale maneno kuingia akilini.

Jirani alimfahamisha kuwa akiwa safari, mkwe mkwee anatawala nyumba yake na majirani humuona a vyoingia na kutoka, huwa anatoka saa nane usiku kwake anakwenda kuitokia roll call kuwa alilala pale. Jirani aliendelea kuwa mkewe ni mwerevu sana katika kuficha hili, ukimuuliza atakataa na anaweza kubadilisha mbinu. Kama una moyo panga mtego wa kuwafuma.

Ni kweli mzee dereva aliaga ana peleka mzigo DRC Congo kumbe amechukua chumba guest mpaka saa tano sita ndiyo akaibuka nyumbani. Mtego ulinasa mkwe akiwa katika matrimonial bed ya wakwe hakuwa na Pa kukimbilia. Walizichapa sana na mkwe alimrushia ngumi baba mkwe jichoni iliyomuumiza sana wakati huo mke akitoka kuomba msaada.

Nyumbani binti alipoyasikia ujauzito uliharibika kwa shock, na binti aliapa kumuua mama yake. Mwisho binti alipata mental breakdown na ilibidi atibiwe hospitali maalum ya akili kwa muda mrefu, bibi alipewa wajukuu awalee na ndoa zote mbili zilivunjika.

Sikufahamu zaidi ya hapa kwani basi lilishafika Kwamtogole ambacho ndiyo kituo changu.
Inawezekana kwa jambo kama hilo aende kufumania bila mashahidi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingawa sina uhakika sana kama hii stori ni ya kweli au ni tungo tu.

Vyovyote vile mimi binafsi namheshimu sana mwanamke, ila tu mwanamke tofauti na mama wengine wote nakua na tahadhari kubwa sana nao.
 
Hapa nahisi mzee atakuwa ampelekei moto mkewe vizuri...

Yani kama mzee hujui kupeleka moto utasaidiwa sana...
Kwa hiyo ni sawa mkwe kula kuku na mayai?.

We huwajui wanawake,ngoja siku ukioa,hawajui wanachotaka.
 
Ingawa sina uhakika sana kama hii stori ni ya kweli au ni tungo tu.

Vyovyote vile mimi binafsi namheshimu sana mwanamke, ila tu mwanamke tofauti na mama wengine wote nakua na tahadhari kubwa sana nao.
Upo sawa mkuu...

Maandiko yamesema 1Petro 3:7 Kadhalika, ninyi wanaume kaeni na wake zenu kwa akili, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.
 
Yaani dogo kamvua chupi mama mkwe?
Dogo huyo huyo kampinga ngumi ya jicho baba mkwe?

Dunia sio mbaya ila walimwengu ndio wabaya.
 
Hapa nahisi mzee atakuwa ampelekei moto mkewe vizuri...

Yani kama mzee hujui kupeleka moto utasaidiwa sana...
Hakuna cha kupelekewa moto wala nini.
Msaliti ni msaliti tu.
Kuna wanawake wana cheat kwa kisingizio cha hali ngumu...ajabu na matajiri nao wana cheat.
Roho ya ku cheat hainaga sababu maalum ni ulemavu tu.
 
Leo nikiwa katika usafiri wa jamii baba mmoja mwenye plasta jichoni alinisalimia vizuri tu na kuniuliza ninapoelekea. Ni wazi kuwa alikua anatafuta mtu wa kuongea nae ila asichokijua ni kuwa ninashare story humu jukwaani hasa mikasa halisi ya watu.

Huyu bwana alidumu kwenye ndoa kwa miaka 28 na binti yao wa kwanza mwenye miaka 27 alishaolewa harusi na anaishi kwa mume wake. Mzee mwenyewe alikua dereva wa Malory makubwa ya kusambaza bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Uchumi wao si haba waliishi katika nyumba ya kisasa aliyoijenga kwa pesa yake. Binti yake akiwa na ujauzito wa tatu kuna jirani aliyemuonba wakutane bar ya jirani kwa mazungumzo. Wakiwa bar jirani alinunua round ya kwanza na soup ya kongoro walipata supu na chapati huku jirani akiongelea uchumi wa nchi na bei ya vitu kupanda.

Walipata round ya tatu na kuku wa makange, alimuuliza jirani yaani umeniita kuja kuninunulia chakula? Jirani alimtaarifu kuwa yale yalikua ni maandalizi kwani alikomuitia ni zito. Mwisho alifunguka kuwa unafahamu mume wa binti yako ndiye Ben-10 wa mke wako? Mzee anasema ilichukua kama dakika tano hivi yale maneno kuingia akilini.

Jirani alimfahamisha kuwa akiwa safari, mkwe mkwee anatawala nyumba yake na majirani humuona a vyoingia na kutoka, huwa anatoka saa nane usiku kwake anakwenda kuitokia roll call kuwa alilala pale. Jirani aliendelea kuwa mkewe ni mwerevu sana katika kuficha hili, ukimuuliza atakataa na anaweza kubadilisha mbinu. Kama una moyo panga mtego wa kuwafuma.

Ni kweli mzee dereva aliaga ana peleka mzigo DRC Congo kumbe amechukua chumba guest mpaka saa tano sita ndiyo akaibuka nyumbani. Mtego ulinasa mkwe akiwa katika matrimonial bed ya wakwe hakuwa na Pa kukimbilia. Walizichapa sana na mkwe alimrushia ngumi baba mkwe jichoni iliyomuumiza sana wakati huo mke akitoka kuomba msaada.

Nyumbani binti alipoyasikia ujauzito uliharibika kwa shock, na binti aliapa kumuua mama yake. Mwisho binti alipata mental breakdown na ilibidi atibiwe hospitali maalum ya akili kwa muda mrefu, bibi alipewa wajukuu awalee na ndoa zote mbili zilivunjika.

Sikufahamu zaidi ya hapa kwani basi lilishafika Kwamtogole ambacho ndiyo kituo changu.
Kwa hiyo nimekupa store yangu uje kuibandika huku
 
Sikuizi Kwenye hizi familia kuna maasi mengi mno yanafanyika sikuizi Mungu aturehemu
 
Hapa nahisi mzee atakuwa ampelekei moto mkewe vizuri...

Yani kama mzee hujui kupeleka moto utasaidiwa sana...

Rafiki, ndio uchague kupelekea moto na mkwe? Inamaana basi anaweza kupelekea moto na Kila mtu, hata kaka yake au ndugu yeyote.

Huyo mkwe kijana anaujasiri wa kupitiliza. Unatoa wapi nguvu ya kumrushia ngumi Baba mkwe? Tena amekufuma Kwa Mke wake aliyekuzalia mkeo.
 
Back
Top Bottom