Kuna watu wanauawa bila Hatia kwa tuhuma za wizi, watanzania tuache kukurupuka

Kuna watu wanauawa bila Hatia kwa tuhuma za wizi, watanzania tuache kukurupuka

Glenn

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2015
Posts
70,481
Reaction score
167,331
Heshima kwenu wakuu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeona leo niwashauri Watanzania wenzangu wanaopenda kufanya maamuzi bila kufanya utafiti.
Wazo/ ushauri huu nimeamua kuuleta hapa baada ya tukio baya la kujaribu kuutoa UHAI wa kijana mmoja asiye na hatia jijini Arusha leo mchana.

TUKIO LENYEWE
majira ya saa 6:30 mchana nikiwa maeneo ya GOLDEN ROSE hotel,
Niliona kijana mmoja akijaribu kuvuka barabara kwa haraka.

KILICHOFUATA
baada ya baadhi ya watu walipomwona akivuka haraka, walianza kupiga kelele za mwizi mwiziii, ghafla nilimwona rafiki yangu jina kapuni naye akitoka na chuma mkononi mwake naye alianza kulifuata kundi hilo linalomfukuza kijana.

KIJANA AKAMATWA
kwa wale wenyeji wa Arusha maeneo ya golden rose lina watu wengi, hivyo huyo kijanahaikuwa vigumu kukamatwa na ghafla walianza kumshambulia kwa vyuma ngumi na mateke.

TUKIO LILIVUTA HISIA
Baada ya kuona hivyo ghafla moyo wangu ulifadhaika kwa kuona kijana anauawa mbele ya macho yangu, hivyo nilitamani KUJUA sababu inayompelekea umauti kwani sikuona kama atapona.
Nilianza kuwahoji waliokuwa mstari wa mbele kumpiga kwa kuanzia na huyu jamaa ninayemfahamu.
Hakunipa majibu ya kuridhisha, wapili na wa tatu wote hawakuwa na majibu

NILICHUKUA HATUA ZA KUHATARISHA UHAI KUMNUSURU
baada ya kukosa majibu ya kwanini wanataka kumuua ndipo nilipoamua kuingia ktkt ya kundi kubwa na kuwaomba wale wanaompiga kujiridhisha na hatua hiyo kabla hawaja muua.
Walinikasirikia wakidai huyo ni mwizi nami niliwahoji
Kaiba nini
Aliyeibiwa yu wapi
Ameiba k2 gn?
Walikosa majibu, wakatulia japo kabla ya kutulia walinikasirikia na kunitolea lughachafu, nami ckujali nilivaa ujasiri nikwaambia tumhoji

MAHOJIANO YAKAANZA
baada ya kuanza kuhoji tuligundua ni mtu alikuwa na haraka zake akikimbilia mteja anayemsubiri dukani baada ya kumpigia simu kuwa anamsubiri.
Ndipo umati uliponigeukia na kunipongeza kwa ujasiri.

SWALI
je ni watanzania wangapi wameuawa bila hatia?
Kuna gharama gani kuhoji na kujiridhisha kabla ya kuchukuahatua?

NINASHAURI TUSIFANYE MAAMUZI KABLA YA UTAFITI
 
pole na hongera sana kwa huo moyo mkuu,huku kitaaa watu wakisikia tu neno mwizi basi wao ni kubeba chochote alichonacho karibu,kuna watanzania wengi sana wamekufa bila hatia,kuna jamaa alikufa udsm pale kisa tu mpenzi wake walipozinguana akaamua kuita mwizi
 
asante kutukumbusha uhai ni muhimu,mie hata km ameiba kweli bado uhai wa mtu ni muhimu.Watanzania wanachekesha sana mbona wanaowaibia kny umma huwa hawashambulii mpaka kuuwa,au MAFISADI HAMYAJUI NYIE???
Kweli ndg. tunaua mwizi wa simu, mwizi wa mabilioni ya EPA anaombwa kurudisha kwa wakati wake
 
Tuna hasira ya tusichokijua...chochote tutachoona kinafaa tunamalizia hasira zetu na kuacha mzizi wa tatizo ukizidi kutambaa.. Mungu atuhurumue kwa kweli.
Uko sahihi, tumezalisha watoto yatima na wajane kizembe kwa kutohoji. Tukisikia kelele za mwizi wote tunageuka watakatifu na kumhukumu mtu tusiyejua kaiba nini
 
pole na hongera sana kwa huo moyo mkuu,huku kitaaa watu wakisikia tu neno mwizi basi wao ni kubeba chochote alichonacho karibu,kuna watanzania wengi sana wamekufa bila hatia,kuna jamaa alikufa udsm pale kisa tu mpenzi wake walipozinguana akaamua kuita mwizi
Ni kweli, asante
 
Hongera bro japo kuna watu watakuja kukuhoji na kukusmbia hii story yako ni ya kutunga [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Well said , nakumbuka aliuliwa mwanafunzi wa ifm pia kama umepitia post za hapa jf kuna kijana kapigwa risasi tatu miguun japo alijisalimisha akidaiwa mwizi kumbe ni mwanafunzi .. Naogopa sana kushiriki katika kutoa uhai wa mtu maana najua ipo siku hiyo damu itanidai
Mbaya sana
 
Hayo hayo ya kukurupuka jamaa mmoja Mbeya aliuwawa kwa kuhisiwa anaiba mbuzi kumbe alimkuta mbuzi amejikaba shingo kamba imemnyoga anataka kufa akaamua kumnasua. Watu walipomkuta anamnasua mbuzi wakaita mwizi kisha?.....kipigo hadi kufa.
Unaona sasa!
 
Back
Top Bottom