UmenenaKinacho sumbua taifa letu hili ni, kukulupuka, siasa za kukulupuka, elimu kukulupukia, kua nako ni kukulupuka, kila kitu kukulupuka, kuchangia mawazo kukulupuka, kilimo kululupuka, muziki kukulupuka, yaani kila kitu ona sasa tutauana tutakwisha bila sababu.
Nzalendo asante pia kwa mchango wako, tushirikiane kubadili jamii yetuKwanza nakupongeza sana kwa hatua uliyoichukua,
Ni mara nyingi watu wasio na hatia wanauawa
Jana tarehe 20 Alfajiri maeneo ya Moshi Bar G/mboto kuna vijana wawili wameuawa kwa kuchomwa moto
Katika kuhoji hawa waliiba wapi? hakuna mwenye jibu au walimuibia nani hakuna mwenye jibu.
Hii ni Hatari
Wengine wanauwawa kwa ajili ya ugomvi wa kipuuzi kama kugombea wanawake na mambo kama hayo chuki au wivu na husda.
Kama adui yako akitaka kukumaliza anakuvizia hadharani akiita mwiziii unauwawa pasi na shaka.
Kwanza nakupongeza sana kwa hatua uliyoichukua,
Ni mara nyingi watu wasio na hatia wanauawa
Jana tarehe 20 Alfajiri maeneo ya Moshi Bar G/mboto kuna vijana wawili wameuawa kwa kuchomwa moto
Katika kuhoji hawa waliiba wapi? hakuna mwenye jibu au walimuibia nani hakuna mwenye jibu.
Hii ni Hatari
Wengine wanauwawa kwa ajili ya ugomvi wa kipuuzi kama kugombea wanawake na mambo kama hayo chuki au wivu na husda.
Kama adui yako akitaka kukumaliza anakuvizia hadharani akiita mwiziii unauwawa pasi na shaka.
Kuna kijana alitofautiana mpenzi wake, ukaibuka ugomvi kati yao, binti alipozidiwa aliita mwiziii...watu wakajaa na ghafla wakamshambulia kijana akafariki na kuchomwa motohayo yametokea saut mwanza katika miaka minne wameuwawa wananzengo hawapungui 6 wakiwepo wanafunzi,watumishi,wote waliuwawa sbb ya kukurupuka na kutoa hukumu ya haraka
Tena utakuta wanawatetea kuwa hawajaiba wanakuuliza, una ushahidi?asante kutukumbusha uhai ni muhimu,mie hata km ameiba kweli bado uhai wa mtu ni muhimu.Watanzania wanachekesha sana mbona wanaowaibia kny umma huwa hawashambulii mpaka kuuwa,au MAFISADI HAMYAJUI NYIE???
Ilitokea wapi.?Kuna kijana alitofautiana mpenzi wake, ukaibuka ugomvi kati yao, binti alipozidiwa aliita mwiziii...watu wakajaa na ghafla wakamshambulia kijana akafariki na kuchomwa moto
Kuna mwamba alipigwa msumari wa nchi 6 maeneo ya Makongo juu! Katoka zake club alfajiri anakatiza mitaa likatokea kundi la watu walikuwa wanamkimbiza mwizi sijui akawapotea.. Sasa kwenye ile kaenda huku ... kapita huku sindio wakakutana na mwamba wakamvagaa!Heshima kwenu wakuu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeona leo niwashauri Watanzania wenzangu wanaopenda kufanya maamuzi bila kufanya utafiti.
Wazo/ ushauri huu nimeamua kuuleta hapa baada ya tukio baya la kujaribu kuutoa UHAI wa kijana mmoja asiye na hatia jijini Arusha leo mchana.
TUKIO LENYEWE
majira ya saa 6:30 mchana nikiwa maeneo ya GOLDEN ROSE hotel,
Niliona kijana mmoja akijaribu kuvuka barabara kwa haraka.
KILICHOFUATA
baada ya baadhi ya watu walipomwona akivuka haraka, walianza kupiga kelele za mwizi mwiziii, ghafla nilimwona rafiki yangu jina kapuni naye akitoka na chuma mkononi mwake naye alianza kulifuata kundi hilo linalomfukuza kijana.
KIJANA AKAMATWA
kwa wale wenyeji wa Arusha maeneo ya golden rose lina watu wengi, hivyo huyo kijanahaikuwa vigumu kukamatwa na ghafla walianza kumshambulia kwa vyuma ngumi na mateke.
TUKIO LILIVUTA HISIA
Baada ya kuona hivyo ghafla moyo wangu ulifadhaika kwa kuona kijana anauawa mbele ya macho yangu, hivyo nilitamani KUJUA sababu inayompelekea umauti kwani sikuona kama atapona.
Nilianza kuwahoji waliokuwa mstari wa mbele kumpiga kwa kuanzia na huyu jamaa ninayemfahamu.
Hakunipa majibu ya kuridhisha, wapili na wa tatu wote hawakuwa na majibu
NILICHUKUA HATUA ZA KUHATARISHA UHAI KUMNUSURU
baada ya kukosa majibu ya kwanini wanataka kumuua ndipo nilipoamua kuingia ktkt ya kundi kubwa na kuwaomba wale wanaompiga kujiridhisha na hatua hiyo kabla hawaja muua.
Walinikasirikia wakidai huyo ni mwizi nami niliwahoji
Kaiba nini
Aliyeibiwa yu wapi
Ameiba k2 gn?
Walikosa majibu, wakatulia japo kabla ya kutulia walinikasirikia na kunitolea lughachafu, nami ckujali nilivaa ujasiri nikwaambia tumhoji
MAHOJIANO YAKAANZA
baada ya kuanza kuhoji tuligundua ni mtu alikuwa na haraka zake akikimbilia mteja anayemsubiri dukani baada ya kumpigia simu kuwa anamsubiri.
Ndipo umati uliponigeukia na kunipongeza kwa ujasiri.
SWALI
je ni watanzania wangapi wameuawa bila hatia?
Kuna gharama gani kuhoji na kujiridhisha kabla ya kuchukuahatua?
NINASHAURI TUSIFANYE MAAMUZI KABLA YA UTAFITI