Kuna watu wanauawa bila Hatia kwa tuhuma za wizi, watanzania tuache kukurupuka

Kuna watu wanauawa bila Hatia kwa tuhuma za wizi, watanzania tuache kukurupuka

Nimeona acha nichangie maana imenigusa mno!
Haya maswala yanatokea sana na wengi wamepoteza maisha burebure tu.
Jambo kama hili sio la kufumbia macho sababu wewe unaekurupuka iko siku pia ndugu yako atafanyiwa hivyo!
Ni mfano mbaya hata ukipita sehemu ukakuta mtu amevamiwa na vibaka au majambazi ila kwakuwa mtu huyo hakuhusu au humjui unapita bila kutoa msaada wowote nakuhakikishia ipo siku utapita wewe utafanyiwa hivyo au ndugu yako au rafiki.tuache kupuuzia mambo ambayo baadae yatarudi na kutuwinda wenyewe
 
Najivunia lugha yangu ya kiswahili hivyo sina budi kuithamini na kuipenda nashukuru kwa kunirekebisha!!! Amani iwe nanyi daima
 
Nimeona acha nichangie maana imenigusa mno!
Haya maswala yanatokea sana na wengi wamepoteza maisha burebure tu.
Jambo kama hili sio la kufumbia macho sababu wewe unaekurupuka iko siku pia ndugu yako atafanyiwa hivyo!
Ni mfano mbaya hata ukipita sehemu ukakuta mtu amevamiwa na vibaka au majambazi ila kwakuwa mtu huyo hakuhusu au humjui unapita bila kutoa msaada wowote nakuhakikishia ipo siku utapita wewe utafanyiwa hivyo au ndugu yako au rafiki.tuache kupuuzia mambo ambayo baadae yatarudi na kutuwinda wenyewe
Umenena vema sana mkuj
 
Heshima kwenu wakuu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeona leo niwashauri Watanzania wenzangu wanaopenda kufanya maamuzi bila kufanya utafiti.
Wazo/ ushauri huu nimeamua kuuleta hapa baada ya tukio baya la kujaribu kuutoa UHAI wa kijana mmoja asiye na hatia jijini Arusha leo mchana.

TUKIO LENYEWE
majira ya saa 6:30 mchana nikiwa maeneo ya GOLDEN ROSE hotel,
Niliona kijana mmoja akijaribu kuvuka barabara kwa haraka.

KILICHOFUATA
baada ya baadhi ya watu walipomwona akivuka haraka, walianza kupiga kelele za mwizi mwiziii, ghafla nilimwona rafiki yangu jina kapuni naye akitoka na chuma mkononi mwake naye alianza kulifuata kundi hilo linalomfukuza kijana.

KIJANA AKAMATWA
kwa wale wenyeji wa Arusha maeneo ya golden rose lina watu wengi, hivyo huyo kijanahaikuwa vigumu kukamatwa na ghafla walianza kumshambulia kwa vyuma ngumi na mateke.

TUKIO LILIVUTA HISIA
Baada ya kuona hivyo ghafla moyo wangu ulifadhaika kwa kuona kijana anauawa mbele ya macho yangu, hivyo nilitamani KUJUA sababu inayompelekea umauti kwani sikuona kama atapona.
Nilianza kuwahoji waliokuwa mstari wa mbele kumpiga kwa kuanzia na huyu jamaa ninayemfahamu.
Hakunipa majibu ya kuridhisha, wapili na wa tatu wote hawakuwa na majibu

NILICHUKUA HATUA ZA KUHATARISHA UHAI KUMNUSURU
baada ya kukosa majibu ya kwanini wanataka kumuua ndipo nilipoamua kuingia ktkt ya kundi kubwa na kuwaomba wale wanaompiga kujiridhisha na hatua hiyo kabla hawaja muua.
Walinikasirikia wakidai huyo ni mwizi nami niliwahoji
Kaiba nini
Aliyeibiwa yu wapi
Ameiba k2 gn?
Walikosa majibu, wakatulia japo kabla ya kutulia walinikasirikia na kunitolea lughachafu, nami ckujali nilivaa ujasiri nikwaambia tumhoji

MAHOJIANO YAKAANZA
baada ya kuanza kuhoji tuligundua ni mtu alikuwa na haraka zake akikimbilia mteja anayemsubiri dukani baada ya kumpigia simu kuwa anamsubiri.
Ndipo umati uliponigeukia na kunipongeza kwa ujasiri.

SWALI
je ni watanzania wangapi wameuawa bila hatia?
Kuna gharama gani kuhoji na kujiridhisha kabla ya kuchukuahatua?

NINASHAURI TUSIFANYE MAAMUZI KABLA YA UTAFITI
Mkuu hii "Elimu" jaribu kuisambaza kadiri uwezavyo ili iwafikie watu wengi zaidi,nasi tutakusaidia kuisambaza ili isomwe na watu wengi zaidi ikiwa utaturuhusu kuisambaza.
 
Mkuu hii "Elimu" jaribu kuisambaza kadiri uwezavyo ili iwafikie watu wengi zaidi,nasi tutakusaidia kuisambaza ili isomwe na watu wengi zaidi ikiwa utaturuhusu kuisambaza.

CleverKing umekuwa mchangiaji muhimu na umetoa ushauri mwingi mzuri na wenye mafunzo
Nafikiri hapa pia ni mahali sahihi pamoja na majukwaa mengi zaidi,
Nitajaribu kutumia shuhuda za kusikitisha walizotoa wachangiaji ili kuweka mtiririko wa matukio unaoleta hisia zinazogusa watu.
Nakaribisha maoni na ushauri toka kwenu kwani KAZI HII INATUHUSU SOTE mkuu
 
Mtukufu wao kawambia wamnyanganye silaha haraka haraka...yaani hukumu bila hata mahakamani hajafikishwa.
Hakika viongozi huchangia sehemu kubwa ya uvunjaji wa sheria na hakuna mwanadamu aliyepewa haki ya kutoa uhai wa mwingine zaidi ya mwendo kasi decesions tu.
Vizuri ndugu kwa kuokoa uhai wa mtu huyo.
 
Cleverking hebu pitia shuhuda za hawa wachache zinazoashiria ukubwa wa tatizo hili la kufanya maamuzi pasipo kujiridhisha kama ni ya kweli.
Hayo hayo ya kukurupuka jamaa mmoja Mbeya aliuwawa kwa kuhisiwa anaiba mbuzi kumbe alimkuta mbuzi amejikaba shingo kamba imemnyoga anataka kufa akaamua kumnasua. Watu walipomkuta anamnasua mbuzi wakaita mwizi kisha?.....kipigo hadi kufa.

Well said , nakumbuka aliuliwa mwanafunzi wa ifm pia kama umepitia post za hapa jf kuna kijana kapigwa risasi tatu miguun japo alijisalimisha akidaiwa mwizi kumbe ni mwanafunzi .. Naogopa sana kushiriki katika kutoa uhai wa mtu maana najua ipo siku hiyo damu itanidai

Kuna uzi niliuona umu jana kijana kapigwa risasi tatu mguuni kisa kama baada ya tukio wanasema sio mwizi mpaka sasa cjafahamu kijana wa watu anaendeleaje inauma sana kwa kweli

Daaaaaah inauma xnaa MWAKA 2015. Nilimpoteza rafiki yangu na kaka yake waliuwawa Dar maeneo ya kigogo yeye na kaka yake akiwa ametoka likzo yake CHUO cha MWEKA Bsc ya wildlife waliuwawa na WATU kwa madai ya kuwa ni wezi wa bodaboda baada ya vibaka kushndwa kuwapora laptop na simu zao ndipo walipo waitia yoe ya mwiziiiii daah waliuwawa kikatili xnaaa inaniumaga mpaka Leo!!!! R.I.P DEAR BROTHERS

Daaa nimemkumbuka class mate wangu Edwin Macha aliuawa kwa kusingiziwa mwizi! Rest in peace bro

Wengi wameuwawa namna hiyo na ninamfahamu kijana mmoja(RIP) aliuwawa baada ya kuruhusiwa hospitali alikokuwa amelazwa kwa tatizo la ugonjwa wa kifafa uliomfanya aathirike kiakili pia.Bahati mbaya hakuwa amepona vizuri ndipo akipita jirani na nyumba moja Mwanza mtoto alipiga kelele mwizi mwizi na watu waliamua kumshambulia bila kuhoji hatimae umauti ukamkuta.Hii ni roho hatari sana maana hakuna aliye salama huwezi jua wewe unayeshabikia matukio kama haya nani atafuata maana huna guarantee kwa hili.

Mkuu hii "Elimu" jaribu kuisambaza kadiri uwezavyo ili iwafikie watu wengi zaidi,nasi tutakusaidia kuisambaza ili isomwe na watu wengi zaidi ikiwa utaturuhusu kuisambaza.
 
Watanzania wengi wetu ni wafuata mkumbo ukiona furani anacheka na wewe unaaza kusaidia kucheka bila kujali ni nini kinachomchekesha yule
 
Back
Top Bottom