Ni kweli usemacho kuwa siku za mtu hupangwa na Muumba, kwani ni ngumu kumwokoa mtu kwa watu wenye hasira kali,Huyo uliyemuokoa...Mungu alikuwa hajapenda afe....ila alijarbu kutoa somo tu kwa watu kupitia wewe mana inaonekana watu Wa huko wamekaa kama killers...vinginevyo mbinu uliyotumia si chochote kwa umati wenye hasira...na istoshe hata wewe wange kuunganisha
Wakati tunafanya utafiti mwizi yupo tu amesimama anasubiria utafiti uishe???
HII KITU INAITWA "MOB JUSTICE" NA MARA NYINGI MTU ANAYEULIWA UKIAMBIWA KAIBA NINI AU MALI YA THAMANI GANI UTABAKI KUSHANGAAA......UTAKUTA KUKU AU SIMU ETC....NI BORA HASIRA HIZO HAO WANAOJIFANYA KUCHUKUA SHERIA MKONONI WAKAZIAMISHIAA KWA WEZI WA MALI ZA UMMA NA MAFISADI...Sio kidogo
Dah very painful,Daaaaaah inauma xnaa MWAKA 2015. Nilimpoteza rafiki yangu na kaka yake waliuwawa Dar maeneo ya kigogo yeye na kaka yake akiwa ametoka likzo yake CHUO cha MWEKA Bsc ya wildlife waliuwawa na WATU kwa madai ya kuwa ni wezi wa bodaboda baada ya vibaka kushndwa kuwapora laptop na simu zao ndipo walipo waitia yoe ya mwiziiiii daah waliuwawa kikatili xnaaa inaniumaga mpaka Leo!!!! R.I.P DEAR BROTHERS
Hongera Kaka Kwa kuingilia kati swala hili,Heshima kwenu wakuu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeona leo niwashauri Watanzania wenzangu wanaopenda kufanya maamuzi bila kufanya utafiti.
Wazo/ ushauri huu nimeamua kuuleta hapa baada ya tukio baya la kujaribu kuutoa UHAI wa kijana mmoja asiye na hatia jijini Arusha leo mchana.
TUKIO LENYEWE
majira ya saa 6:30 mchana nikiwa maeneo ya GOLDEN ROSE hotel,
Niliona kijana mmoja akijaribu kuvuka barabara kwa haraka.
KILICHOFUATA
baada ya baadhi ya watu walipomwona akivuka haraka, walianza kupiga kelele za mwizi mwiziii, ghafla nilimwona rafiki yangu jina kapuni naye akitoka na chuma mkononi mwake naye alianza kulifuata kundi hilo linalomfukuza kijana.
KIJANA AKAMATWA
kwa wale wenyeji wa Arusha maeneo ya golden rose lina watu wengi, hivyo huyo kijanahaikuwa vigumu kukamatwa na ghafla walianza kumshambulia kwa vyuma ngumi na mateke.
TUKIO LILIVUTA HISIA
Baada ya kuona hivyo ghafla moyo wangu ulifadhaika kwa kuona kijana anauawa mbele ya macho yangu, hivyo nilitamani KUJUA sababu inayompelekea umauti kwani sikuona kama atapona.
Nilianza kuwahoji waliokuwa mstari wa mbele kumpiga kwa kuanzia na huyu jamaa ninayemfahamu.
Hakunipa majibu ya kuridhisha, wapili na wa tatu wote hawakuwa na majibu
NILICHUKUA HATUA ZA KUHATARISHA UHAI KUMNUSURU
baada ya kukosa majibu ya kwanini wanataka kumuua ndipo nilipoamua kuingia ktkt ya kundi kubwa na kuwaomba wale wanaompiga kujiridhisha na hatua hiyo kabla hawaja muua.
Walinikasirikia wakidai huyo ni mwizi nami niliwahoji
Kaiba nini
Aliyeibiwa yu wapi
Ameiba k2 gn?
Walikosa majibu, wakatulia japo kabla ya kutulia walinikasirikia na kunitolea lughachafu, nami ckujali nilivaa ujasiri nikwaambia tumhoji
MAHOJIANO YAKAANZA
baada ya kuanza kuhoji tuligundua ni mtu alikuwa na haraka zake akikimbilia mteja anayemsubiri dukani baada ya kumpigia simu kuwa anamsubiri.
Ndipo umati uliponigeukia na kunipongeza kwa ujasiri.
SWALI
je ni watanzania wangapi wameuawa bila hatia?
Kuna gharama gani kuhoji na kujiridhisha kabla ya kuchukuahatua?
NINASHAURI TUSIFANYE MAAMUZI KABLA YA UTAFITI
NDIO MAANA HAKUIBAWakati tunafanya utafiti mwizi yupo tu amesimama anasubiria utafiti uishe???
Very sadDaaa nimemkumbuka class mate wangu Edwin Macha aliuawa kwa kusingiziwa mwizi! Rest in peace bro
Ni Mwanza Hostel za St.August.pole na hongera sana kwa huo moyo mkuu,huku kitaaa watu wakisikia tu neno mwizi basi wao ni kubeba chochote alichonacho karibu,kuna watanzania wengi sana wamekufa bila hatia,kuna jamaa alikufa udsm pale kisa tu mpenzi wake walipozinguana akaamua kuita mwizi
Hii ni mbaya sana mkuu, hatufikiri, kama tunachukia wizi tungeandamana kushinikiza wizi wa mabilioni tunayoibiwa na watawala ili wachukuliwe hatua.Hongera Kaka Kwa kuingilia kati swala hili,
Nakumbuka nilitaka kuuwawa mwaka 1998 pale muhimbili hospitali baada ya kuingilia kati kumuokoa kijana ambaye aliiba viatu msikiti wa muhimbili, pair moja ya Viatu ilitaka kutoa uhai wa kijana huyo na wangu ,kwani nilishaona jicho kijana limemtoka na ameshapoteza ufahamu wa kuwepo duniani watu walitupa matofali ,mawe na yalitupata wote lkn nilichofanya ni kumvuta kijana hadi getini kwenye polisi muhimbili na kufika hapo polisi waliingilia kutoa msaada.mimi nilikuwa hoi na nundu usoni lkn kwa uwezo wa mungu wote tulisalimika. Jamii inatakiwa iwe nasubira ktk kuushirikisha ubongo hasa kwenye matukio ambayo hayahatarishi maisha ya mtu,mfano hata kama mtu ni mwizi na hahatarishi uhai wako au wa mtu mwengine kwanini tatizo listatuliwe kwa kufuata sheria na kuepuka kujichukulia maamuzi ya kutoa roho ya mtu mwengine hata kama ni mwizi.
Akili za watz sijui zikoje jmnNDIO MAANA HAKUIBA
alisubiri ukweli kwa aliyemuibia
mm namshukuru sana aliyemuokoa
QUIGLEY
mdogo wangu alishawahi kuitiwa mwizi na mwanamke tu hawakuelewana na akashtukia kundi kubwa likimfukuza akajichomeka nyumba ya watu na walipoulizwa kaiba nini wakasema kamuibia mwanamke . Mwanamke kuulizwa kakanusha wakatawanyika
Uko sahihi sana kiongoziHII KITU INAITWA "MOB JUSTICE" NA MARA NYINGI MTU ANAYEULIWA UKIAMBIWA KAIBA NINI AU MALI YA THAMANI GANI UTABAKI KUSHANGAAA......UTAKUTA KUKU AU SIMU ETC....NI BORA HASIRA HIZO HAO WANAOJIFANYA KUCHUKUA SHERIA MKONONI WAKAZIAMISHIAA KWA WEZI WA MALI ZA UMMA NA MAFISADI...
OVA