Kuna watu wenye roho mbaya na roho za husuda nchi hii

Kuna watu wenye roho mbaya na roho za husuda nchi hii

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
259
Reaction score
292
Kuna watu wanaroho za korosho,roho mbaya kwa watumishi wa Umma katika nchi hii.Hawataki kuona watumishi wa umma wanaongezewa kipato.

Baada ya taarifa ya ikulu Jana kutoka ikisema mhe Rais Samiah Suluhu Hassan amekubali kufanya nyongeza ya mishahara kwa asilimia 23.3% kwa watumishi wa umma wameanza kulalamika na kusema nchi hii haina uwezo wa kuongeza mishahara kwa watumishi wote kwa asilimia tajwa.

Naamini hawa watu wana nia ovu na serikali ya awamu ya sita hawapendi kuona inafanikiwa, watu hawa wanafikira za kumkwamisha mhe Rais Samiah Suluhu Hassan.

Watu hawa wanaishi awamu ya tano ambayo haikuhitaji Wala kujali masrahi ya wafanyakazi ikiwemo nyongeza ya mishahara.

Watu hawa walijipanga kuona mhe Rais anashindwa ili iwe kicheko Kwao bahati mbaya wanaona Kila kitu kinaenda roho zinawauma.

Nawaomba watu hawa wanyamaze wamuache mhe Rais aendeshe nchi kwani uongozi ni kupokezana vijiti kwa sasa kijiti Kiko Kwa mhe Rais Samiah Suluhu Hassan.Asanteni jumapili njema.
 
Yesu Aliwatendea Binaadamu wema muda wote Nadhani kilichomtokea kila mtu anakijua,Mashetani yanaishi ndani ya watu na kuna watu ni Mashetani Ila Hawajijui....Maombi ni Muhimu jamani...Tufanye Ibada Tusitumike na Shetani.
 
ndugu haya maisha yangekua ni kufanyiana mema trust me bado ingeboa ndio mana ikawa hivo wema na wabaya warefu na wafupi wanene na wembamba weee fanya mambo yako mengine yasiyo ya lazima achana nayo
 
ndugu haya maisha yangekua ni kufanyiana mema trust me bado ingeboa ndio mana ikawa hivo wema na wabaya warefu na wafupi wanene na wembamba weee fanya mambo yako mengine yasiyo ya lazima achana nayo
Umenena vyema
 
Amina yaani watu ameongeza mishahara halafu Kuna mtu anajishebedua eti nchi haina kipato. Wakati wenye mamlaka wameongezwa.
 
ndugu haya maisha yangekua ni kufanyiana mema trust me bado ingeboa ndio mana ikawa hivo wema na wabaya warefu na wafupi wanene na wembamba weee fanya mambo yako mengine yasiyo ya lazima achana nayo
Wewe ubaya gani haukoboi ili unialike nije kukufanyia [emoji848][emoji2960]
 
Wewe ubaya gani haukoboi ili unialike nije kukufanyia [emoji848][emoji2960]
hakuna ubaya usioboa lakini mimi ni mtu ninayejali amani ya moyo wangu zaidi hivo hata huo ubaya ukifanya nitaishia kukuangalia tu na hakuna kitakacho badilika
 
Amina yaani watu ameongeza mishahara halafu Kuna mtu anajishebedua eti nchi haina kipato. Wakati wenye mamlaka wameongezwa.
Suala la kuongeza mishahara lipo KISHERIA na ni takwa la KATIBA.

Tulipumbazwa na Rais wa awamu ya 5, alikanyaga katiba kwa miaka yote sita kutowalipa stahiki zao watumishi na kuwafanya waishi kama 'vichaa' kwa stress.

Rais afuate Katiba siyo huruma wala hisani yake kuwaongeza salary watumishi, watanzania tumepumbazwa sana na hawa watawala wanaofikiri wao ni miungu.
 
Mambo yao waachie wenyewe, yasikuumize kichwa...
 
Back
Top Bottom