RESILIENT KATO
JF-Expert Member
- Aug 21, 2024
- 1,472
- 2,766
Kidoti!ni cheusi au kekundu!!?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchana mwema pia DadakidotiEP 15
Baada ya kufika pale duka la dawa sijataka kukaa namuaga auntie na kwenda nyumbani. Auntie ananiambia nimsubiri afunge tuondoke wote lakini namkatalia nachukua bodaboda na kurudi nyumbani. Nyumbani namkuta mdogo wangu, dada wa kazi wapo sebuleni nawasalimia na kwenda chumbani kwangu sina mudi kabisa ya kuongea na mtu yeyote.
Auntie anarudi ananigongea namfungulia anakaa kitandani na kunilaza miguuni kwake na kuniuliza kwa upole mbona umekuja umebadilika Lisa kwani Dav amekufanya nini? Namwambia Aunt wewe si ulikuwa unamsifia Dav wewe yaani hapo tena sijisikii kumuita kaka kama mwanzo. Unaweza kuamini kuwa ananinataka kimapenzi, mwanamke wake namjua, mama yake ananichukulia kama bint yake, marafiki zake wanajua kuwa mimi ni mdogo wake baadhi ya marafiki zangu wanajua sisi ni ndugu inakuwaje ananitaka kimapenzi. Simpendi Dav aunt naanza kumchukia.
Auntie huku akinichezea nywele zangu. Lisa mwanangu sikia Dav hajakukosea kukueleza hisia zake. Kumbuka mna historia wewe na Dav hamjafahamiana leo au jana angekuwa na nia mbaya na wewe angelishakwambia maneno hayo zamani tu. Lakini kumbuka amevumilia muda gani. Pili alikupambania na bado atakupambania. Angekuwa na nia mbaya asingeniambia na mimi. Namuuliza auntie kwani na wewe ulikuwa unalijua hili?
Akanijibu ndio sio mimi tu hata mama yake Dav anajua angekuwa na nia mbaya kabisa asingetushirikisha na sisi. Dav anakupenda tena sana alafu ni kijana mzuri tu. Au una mahusiano mengine huko Dar na kama unayo yakoje mimi ni rafiki yako unaweza kunambia.?
Kama mnavyojua Lisa sio mtu wa kujichanganya nikitoka kazini nipo kwangu siku za kuwa nyumbani nitafanya usafi labda na kwenda kanisani. Sio mtu wa kwenda club, sijui beach sijui wapi, kwa ujumla sio mzururaji. Mimi ni kazini, kanisani, na kuwatembelea ndugu na penyewe mara moja moja ndio Maisha yangu.
Hapana auntie sina mahusiano husiano kwa sasa.
Basi mwanangu jaribu kumpa nafasi Dav japo kidogo najua hawezi kukuumiza wala kukudhuru kumbuka mimi na mama yake Dav tupo upande wako. Auntie ananibembeleza mpaka nalala huyu mwanamke (auntie) alikuwa na upendo sijawahi kuona
Kumekucha!
Nimekubalia Dav ombi lake, tunapendana sana yaani mapenzi ni matamu yaani ukinichanja damu inatoka jina Dav. Maisha yanaendelea vizuri kabisa na Dav ndo alikuwa mwanaume wangu wa kwanza katika Maisha yangu nampenda sana. Maisha yangu hayaishi safari ni Dar – Morogoro, Morogoro – Dar na Dav hivyo hivyo asipokuja yeye nitaenda mimi Morogoro na kuna kipindi naweza kwenda kwa Dav nikaishia kwake hata kwetu nisifike.
Nipo Dar kazini napokea simu namba ngeni. Halo Lisa mambo, namwitikia na kumuuliza nani mwenzangu anajibu kuwa yeye ni Omary (Omary huyu tulikutana naye ep 4) tumesalimiana akanambia kuwa anategemea kuja Dar wiki moja mbele nikamjibu karibu.
Wiki imepita kweli Omary ananipigia simu na kuomba kuonana na mimi. Sijamkatalia ila nikamwambia kuwa tuonane Jumamosi sababu ni siku ambayo nakuwa sipo kazini.
Jumamosi imefika Omary akanitumia location. Waswahili wanasema kubali wito kubali wito kataa neno. Nikaenda kuonana nae nina shahuku kujua anataka kunambia nini.
Nimefika pale alipo tumekumbatiana nimekaa nikaagiza juice ya matunda huku nina hamu sana ya kujua Omary anataka kunambia nini.
Lisa umependeza sana na unaonekana mkubwa tofauti na kipindi kile.
Hahaa ni kweli nimekua ila sijabadilika bado lakini miaka imeenda lazima nibadilike kidogo.
Lisa naomba unisamehe sana najua kipindi kile nilikuumiza bila sababu.
Unaongelea nini tena.
Lisa bado nakupenda sana nahitaji nikuoe wewe ni mwanamke wa ndoto zangu naomba unisamehe. Huu mguu ni wako nimetoka kanda ya ziwa mpaka dar kwa ajili yako.
Omary kwani mke wako Hawa si yupo sasa inakuwaje unaangaika tena.
Omary huku akitokwa na machozi. Hii ilikuwa mara ya kwanza kumuona mwanaume anatokwa na machozi. Akaanza kunambia “kwani Lisa hujui kilichotokea kati yangu na Hawa hata dada yako hajakwambia?”
Kumetokea nini kati yenu? Mimi sijui chochote nikiongea na dada ni salamu tu hakuna zaidi ya salamu labda na mambo ya familia. Hivyo sijui kitu.
Hawa alinidanganya kumbe yule mimba ambayo ndo ulimwacha nayo haikuwa yangu. Nimelea mtoto ambaye sio wa kwangu yule mwanamke ni msaliti na muuaji. Alinidanganya. Kipindi kile nataka kuanzisha mahusiano na wewe alinionyesha msg ulizokuwa unachati nae ukimweleza unavyompenda supervisor na anavyokununulia vitu. Basi mimi nikamwamini nikajua kweli unatoka na supervisor. Na nilipokuwa naona supervisor mara kwa mara akikuuliza kama unataka soda tunakunywa staff nzima na ukikataa hanunui, na yule dada alivyokuwa amedaivet simu yako nikaamini kweli utakuwa unatoka nae.
Nikaamua kuwa na yeye kumbe alikuwa mjamzito tayari na mhusika alikuwa nje ya nchi kimasomo. Nilitaka kufunga nae ndoa ya kanisani (naomba nieleweke omary sio jina lake nimetumia tu omary kwahiyo msishangae ) alikataa tukaishia kufunga ndoa ya serikali kumbe alikuwa anajua anachokifanya. Jamaa yake alipomaliza masomo amekuja kumchukua yeye na mtoto na ninavyoongea na wewe walishafunga ndoa ya kanisani na sasa wanatarajia mtoto mwingine (kumbe Hawa ni mjamzito)
Omary ilinihukumu pasipo kufuatilia sikutoka na mwanaume yeyote pale kazini kwenu. Pili unafikiri hiyo miaka yote mi ningekaa nakusubiri wewe ili ujue ukweli? Asingekuacha je ingekuwaje. Mimi nipo na mahusiano yangu tena yapo imara siwezi kumsaliti mpenzi wangu wala kuwaza kumuacha. Ila pole kwa yalokukuta. Alinibembeleza sana lakini nikamkatalia nawezaje kumkubalia wakati mimi na Dav tuko sawa.
Tuliachana hapo akiwa mnyonge sana. Toka siku hiyo sina taarifa zake. Ila asikwambie mtu, ukisikia aliyekuumiza bila sababu moyo wako unafurahi sana. Kwakweli moyoni nilifurahia anguko la omary. Mchana mwema.
asante kipenziMchana mwema pia Dadakidoti
Auntie aishi miaka 100......nimemmisi auntie wangu ila ninaamini hipo siku nitakutana nae. mtu mmoja aseme neno moja kwa ajli ya auntie
AmenAuntie aishi miaka 100......
Inauma Sana ,aunt wherever you are tafadhali rudi tena Lisa anakupenda SanaAuntie aishi miaka 100......
Mwenyezi Mungu amjalie afya njema Auntie.nimemmisi auntie wangu ila ninaamini hipo siku nitakutana nae. mtu mmoja aseme neno moja kwa ajli ya auntie