Kuna wengine hatujui tulipokosea

Kuna wengine hatujui tulipokosea

Dah, wa kishua halafu kwenda shule unakutana na mbwa mwitu 10?
Nwei tuendelee kustorika
namaanisha tulikuwa tunaonekana wakishua. sababu watu walikuwa wanakuja kwetu kufanya kazi za vipande wanapewa hela, wakati mwingine chakula. pili babu yangu alikuwa hali chakula bila mboga wala alikuwa hali dagaa. tatu shule ya msingi tulokuwa tunaenda na viatu shuleni tunapewa na hela ya kutumia tulikuwa tunahesabika.nne kipindi hicho hapakuwepo na usafiri kama daladala au bodaboda hivyo ilibidi tutembee kwa mguu tu. asante
 
Epi 3

Mwaka umepinduka bibi mzaa mama na babu na bibi wanapambana kuhakikisha naendelea na masomo wananitafutia chuo wanakuta nafasi zimeisha naambiwa kuwa tusubiri mpaka mwakani.

Si baba wala mama anayetoa ushirikiano wao wako bize na Maisha yao wanaoangaika ni babu na bibi tu pande zote mbili.

Wakati chuo ambacho walikuwa wameki- target wamesema tusubiri hivyo nikawa nipo tu kijijini.

Sina hili wala lile nipo na bibi tunapiga stori anapokea simu na kunipa simu na kunambia Lisa simu yako. Napokea simu kumbe ni dada yangu mtoto wa baba yangu mkubwa anayeishi mjini ananiambia kuna kazi kwenye kampuni yao anakofanya kazi wakati naendelea kusubiri kwenda shule ningeenda kujishisha pale ili nisikae bila kazi. Basi dada yangu akanitumia nauli kesho yake asubuhi nikaenda mjini na keso yake naanza kazi pale kama kibarua. Tunalipwa sh 4,000 kwa siku ila wanalipa kila mwisho wa wiki nakakubali make kwa kipindi hicho ilikuwa kubwa kumbuka sina majukuma nakula bure nalala bure kwa dada yangu.

Nimezoea kazi sasa na haikuwa kazi ngumu Lisa nimenenepa ghafla kama nimelkula hamira nimependeza yaani Lisa, Lisa kweli nina rangi ya choklate si mfupi si mrefu, nina jicho la kusinzia, vidimpo vya uchokozi na kidoti changu kwenye paji la uso. Lisa si haba wanaume wanaanza kujipendekeza kuanzia kazini kwetu mpaka mtaani. Naletewa zawadi kila iitwapo leo kidogo mji umenchangamsha nimekuwa muongeja japo dada yangu ni mpole.

Dada ananipa somo.

Sikia mdogo wangu Lisa usije ukajiloga ukaanzisha mahusiano na wanaume wa pale kazini. Utafukuzwa kazi na ukifukuzwa kazi hupo tayari kurudi kijijini?

Dada Hapana sitaki kurudi kijijini nakuahidi sitakuwa na mahusiano yoyote pale kazini nataka nitafute hela niwe kama wewe dada yangu.

Dada yangu ni fundi cherehani akitoka kazini huwa anashona nguo hiyo ni kazi yake ya ziada. Sasa dada oda ni nyingi kutoka kazini kwetu na wateja wengi ni wanaume. Jumamosi na jumapili watu hawakatiki nyumbani kwa dada. Wanalete nguo awashonee lakini wengi wao ni kuniwinda Lisa. Maneno ya dada yanatembea kwenye akili yangu sitaki kuwa na mahusiano na wanaume wa kazini. Hivyo nikawa nawatolea nje.

Wengine wakawa wanazusha wenyewe kuwa wana mahusiano na mimi wakati sio kweli. Kumbe hata supervisor wetu alikuwa ananitaka ila hajaniambia tukiwa kazini ananiuliza kama natoka soda nikikubali tunanunuliwa staff nzima. Nikikataa watu hawanywi soda. Baadhi ya watu wakadhani natoka nae maneno mpaka yakamfikia dada yangu ambaye tulikuwa vitengo tofauti. Na kila kitengo walikuwa na ofisi yao. Kwa hiyo mimi na dada tulikuwa tunaachana getini tu.

Dada akaniuliza nikamwambia kuwa siwezi kuvunja ahadi yangu kwakohata siku moja.

Kuna dada mmoja kumbe anatoka na supervior staff mwenzangu mtu mzima kidogo, nikimwamkia haitikiii, kumbe kadaivet simu yangu ili ajue huwa tunaongea nini mimi na supervisor.

Weekend dada hayupo ananipigia kunipa maagizo ya nyumbani simu yangu haipo hewani anapokea Ana (aliyedaivet simu yangu) dada anagundua kuwa simu yangu imedaivetiwa. Jumatatu tunaenda kazini dada yangu aliikuwa anafanya kazi upande wa utawala Ana anaitwa na kupewa onyo kali na uongozi. Tukio hilo likanifanya niendelee kuwa maarufu pale kazini.

Kuna rafiki yangu huyu kipenzi tumwite Hawa si jina halisi tunafanya wote kazi na umri wetu hatujatofautiana sana tunaambiza visiri vyetu vya kitoto.

Kuna jamaa tumwite Omary si jina lake sasa huyu jamaa tumemkuta pale kazini ni handsome anajua kuvaa akipita ananukia ana bezi kama ya Jaiva nae alikuwa kati ya wale wanaoniwinda. Kimoyomoyo nikasema potelea mbali maneno ya dada nitamkubali Omary nampenda sana.

Nikaona nimshirikishe shoga yangu Hawa. Kumbe Hawa ni mjanja keshapiga hatua moja mbele zaidi yangu kumbuka yeye amekulia mjini mimi ni wakuja tu.

Natarudi. mimi ni mvivu sana kesho nitajitahidi kumalizia jamani
niliemkwaza anisamehe
 
namaanisha tulikuwa tunaonekana wakishua. sababu watu walikuwa wanakuja kwetu kufanya kazi za vipande wanapewa hela, wakati mwingine chakula. pili babu yangu alikuwa hali chakula bila mboga wala alikuwa hali dagaa. tatu shule ya msingi tulokuwa tunaenda na viatu shuleni tunapewa na hela ya kutumia tulikuwa tunahesabika.nne kipindi hicho hapakuwepo na usafiri kama daladala au bodaboda hivyo ilibidi tutembee kwa mguu tu. asante
Kwa aliye chini ya miaka 40 na hakukulia kijijini hawezi elewa unamaanisha nini, enzi zetu za primary kuvaa viatu ilikuwa indicator mojawapo ya kutokea familia ya kishua.Uko sahihi madam
 
nimetumia kama utambulisho wangu japo si halisi
Hapana haujamuelewa, swali lake linalenga kwenye neno 'make' ambalo unalitumia sana ndani ya sentensi za kwenye simulizi yako..anauliza, hilo ni neno la kiswahili?
Ndo maana kuna comment nimemjibu kuwa hilo neno kwa nilivoelewa mimi unafupisha tu badala ya kuandika 'maana yake' wewe unafupisha tu unaandika 'make'
 
Back
Top Bottom