Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole Sana Kaka ,Revacatus kazinja ? Dah pole aiseDaah!! Umenikumbusha mengi.
Baba yangu mzazi alinikataa kata kata nikiwa na mwaka mmoja, mama yangu akanipeleka kwa baba yake (babu yangu). Nimekulia huko na kusomea huko na kitu cha kushukuru niliandikishwa shule kwa jina la Babu yangu.
Sijawahi kumuona Baba kwa sura ila kwa sauti nimewahi kuongea kwa njia ya simu. Mara ya mwisho kuongea nae akiwa na dada yake ananiuliza una uhakika gani kama mimi ni Baba yako? Nilikata simu hadi leo sijawahi hata kuhangaika kumtafuta.
Nachojua tu kwao ni KAMACHUMU anaitwa REVOCATUS KAZINJA
Ndiyo maisha ndugu.Pole Sana Kaka ,Revacatus kazinja ? Dah pole aise
Wazazi wa dizain hii vilaza hawafaiEp 5
Nakata tiketi ya kwenda Morogoro, naaga pale kazini kwa mbwembwe kuwa naenda kusoma. Utawala wananisihi sana nisiondoke kwani nipo kwenye orodha ya wafanyakazi wanaokaribia kupata ajira ya kudumu. Dada amenisihi sana lakini nimewagomea naikukumbuka sana nafasi hii.. Inabidi nirudi Kijiji kuaga na kujiandaa kwa ajili ya safari.
Nimefika kijijini babu na bibi wanalipokea vyema jambo la mimi kurudi shule lakini upande wa bibi mzaa mama inakuwa tofauti inakuja barua kwa babu ya kuzuia mimi nisiende Morogoro. Barua inaeleza Kwa sababu zifuatazo:-
Na nyingine kibao ila hizi zilikuwa zimetiliwa mkazo. Barua hii iliandikwa na mjomba kutoka upande wa mama naikukumbuka sana barua hii. Hapa ndo unapojidhiirisha msemo wa mdharau mwiba mguu huota tende.
- Kuwa baba hana kazi maalumu ya kumuingizia kipato ni misheni town tu.
- Baba hana mke hivyo mimi kama mtoto wa kike nani atakayeniangalia?
- Baba hana nyumba ya kuishi.
Napokea simu kutoka kwa mama ni miaka sita imepita tangu tulivyoonana kwenye msiba hatujawahi kuonana tena ananipigia simu na kunambia nisiende Morogoro kwa baba atatuma nauli nimpe muda tu ili niende Dar. Nae namkatalia babu nae anajaribu kunishawishi lakini wapi.
Natishia kujiua kuwa hakuna wa kunizuia kwenda kwa baba yangu labda kifo tu. (wazazi wawekeni wazi Watoto wenu.) nampigia baba simu na kumwambia kuwa wanajaribu kunizuia nisije huko wanadai kuwa huna nyumba, huna mke, huna kazi utanitunzaje? Baba ananijibu kama nimekuzaa mwanangu nitashindwaje kukutunza. Alokwambia sina nyumba nani achana nao mwanangu wewe siku ya safari ikifika panda bus njoo mimi ni baba yako.
Naongea na babu ananiruhusu ila ananiambia nikikuta Maisha ni magumu nimpigie simu anitumie nauli nirudi kanda ya ziwa. Tunakubaliana siku ya safari inafika napanda bus kuja zangu Morogoro huku nikifurahi kuja kuishi na baba yangu na kuwaona wadogo zangu ambao nawasikika kwa majina tu.
Nipo kwenye bus Kidoti mie naenda Morogoro. Tumefika Dodoma kwenye siti ya pembeni abilia mwenzangu ameshuka na anapanda kijana mdogo tu age mate wangu anatoka zake Dodoma anakuja Dar ndo makazi yake. Tunasalimiana anajitambulisha kuwa anaitwa Dev si jina lake. Kijana huyu anakula hovyo. Ananunua vitu anakula kama mwendawazimu yaani kama kero tunakaribia Gairo Dev anaumwa tumbo nampa pain killer nilikuwa nazo. Dev anakaa sawa tunaanza stori za hapa na pale tunabadilishana namba wote tunashuka Morogoro tulifika usiku. Ananisubiri mpaka wenyeji wanapokuja kunihchukua naye aendelee na safari zake. Kumbe yeye anaishi Morogoro wote tunaenda Morogoro mjini tofauti mitaa tu japo si Jirani.
Ajabu anaekuja kunipokea msamvu sio baba yangu mzazi ni baba yangu mkubwa kaka yake na baba. Ananiambia kuwa baba yangu kasafiri kikazi yupo tanga akirudi atanikuta kwake. Nakubali nitafanyaje sasa na wakati mji huo sio mwenyeji na baba yangu.
ya kulalia tukutane kesho. nawapenda
Ila hii mijizi Mungu anajua 😅😅nimeishatapeliwa mara tatu nimekoma mimi 🙌🏼😅Ep 11
Siku ya field imefika nimejiandaa nimeenda kazini kwa kina kaka Dev naanza kazi. Natambulishwa kama mdogo wake kaka Dav yaani nipo na furaha, Napata marafiki wapya. Maisha yanaendelea walau kipindi hichi nina nafuu nikiamua kupika napika, nikiamua kuacha hakuna wa kuniuliza nafanya chochote ninachojisikia kufanya najiona kabisa kaka Dav na untie wameniamisha kabisa sayari.
Pale kazini ninaendelea vizuri nimempata rafiki mpya mcheshi tumuite Husna. Muda wa lunch huwa tunaenda kununua na kuja kula pale kazini. Kuna sehemu ofisi imetenga kama sehemu ya kulia chakula. Hivi imekuwa ni kawaida yetu kwenda kununua na kuja kula pale kazini. Tofauti na kina kaka Dav wao huenda kula huko huko na kurudi.
Kaka Dav ananitambulisha kwa baadhi ya ndugu zao na mama yake kama mdogo wa ihari na mimi aunt anamfahamu kaka Dav kama kaka yangu wa ihari. Maisha ni mazuri siku moja kaka Dav ananitambulisha kwa girlfriend wake ni mzuri kwelikweli yaani Maisha yangu yamejaa amani.
Nimeshazoeleka pale kazini kuna kaka mmoja anaitwa Rafael. Rafael anajenga mazoea kidogo kidogo kwangu mara wakienda kula ataniuliza Lisa unakunywa soda gani namtajia wakirudi amenibebea.
Mazoea yakaanza kidogo kidogo siku nyingine ananibebea chips anamuita Husna ananiletea mimi na shoga yangu tunakula tu ikafika hatua ikawa kama sheria kila wakienda kula lazima arudi na chakula kwa ajili yangu.
Ikumbukwe Kaka Dav ameshanipa onyo kuhusu wanaume wa kazini pale. Ila mtu akikuletea kitu huwezi kukataa, pia kaka Dav ameshanionya pia kuhusu Rafael. Siku moja kama ilivyo kawaida ya Rafael kuniletea chakula siku hiyo kanibebea chips na soda, nipo na Husna tunataka kula. Mara kaka Dav anaingia huku amefura kwa hasira anakuja moja kwa moja kwangu hivi Lisa unataka nikuonye mara ngapi kuhusu huyo Rafael? Chips zile zote zimemwangwa chini ananifuata amenishika tai anataka kunipiga. Nimeogopa nimefumba tu macho nasubiri kibao kama si ngumi kitue kwenye mwili wangu. Nasikia ameniachia nafumbua macho nakuta ameweka mikono yake mifukoni huku amanikazia macho na kunambia nisamehe Lisa sikukusudia kukufanyia hivi ila sitaki uwe na mazoea na wanaume wa hapa watakuchezea tu mdogo wangu.
Hakuna shida kaka nimekuelewa naondoka zangu na kurudi ofisini kwetu. Nachukua simu na kumtumia ujumbe Rafael. “Samahani Rafael naomba usinunulie kitu chochote tena”
Unamwogopa huyo kaka yako?
Hapana namheshimu sitaki kumkwaza. Kidogo kidogo nikaacha mazoe kabisa kwa Rafael.
Maisha yanaendelea siku zangu za kukaa pale zimeisha inabidi nirudi zangu kumalizia masomo yangu. Kwakweli kilikuwa kipindi ambacho kilikuwa na nafuu Kwangu. Narudi kuendelea na masomo yangu.
Muda umefika nimemaliza chuo, nipo tu nyumbani kwa baba mdogo naona kidogo wamepunguza masimango nafanya kazi zote kama kawaida lakini ile kupigwa bila sababu hakuna tena kusimangwa hakuna. Kazi ikawa kupata kazi sasa. Kila siku wakina babamdogo na mke wake wananipa ahadi zisizotimia za kutafutiwa kazi lakini hamna mabadiliko.
Siku moja baba anakuja hoja niendelee na masomo tena Magogoni ninakubali lakini kwa sharti nikae hostel baba yangu ankubali anatuma pesa kwa mdogo wake. Nimeshafanya maombi ya hostel msimbazi centre nimepata nafasi na magogoni nimepata nafasi.
Ninapewa hela kwenda benk kulipa ada ya chuo, hela ya miwani macho yalikuwa yananisumbua kidogo na hela ya kununua vitambaa ya kushona suti kwa ajili ya sare. nimepewa sh 1.2 kwa ajili ya matumizi yote.
Ada za wadogo wangu huwa napewa mimi kwenda benk lakini siku hiyo nakutana na msiba mpya katika Maisha yangu. Nimeenda moja kwa moja posta bank ya CRDB tawi la Holland ilikuwa tarehe 17/6/2014 siku ya jumanne sijawahi kuisahau hii siku katika Maisha yangu
Lengo langu ilikuwa nilipie ada ya chuo laki sita, na ada ya hosteli laki tatu, nikitoka hapo ndio niendelee na mizunguko mingine. Nimeingia ndani ya benki nimechukua fomu ili nijaze tena mbele ya tela kabisa. Nipo bize naendelea na shughuli zangu akaja mbaba anaonekana mtu wa heshima amevaa suti na tai juu akanianamia na kuninong’oneza unalipa ada? Nikamjibu ndio sasa mwanangu naomba unisaidie na mimi nimekuja kulipa ada ya wadogo zako lakini sijui hata hizi fomu zinajazwaje nikamjibu sawa lete tu fomu nikujazie
Akaleta fomu ananitajia majina najaza kiasi nimjazia nikachukua slip zake nimempa naendelea na za kwangu nimemaliza niachukue pochi yangu hamna baasha nayo haipo nataamaki kumbe nimeibiwa napiga kelele mlango wa benki unafungwa watu walokuwa ndani ya benki hawaruhusiwi kutoka nje. Tumeenda kwenye CCTV Camera kuangalia kuanzia kipande cha mimi naingia ndani ya benki. Watu wote wanaonekana sura nikiwemo mimi ila yule baba aoniibia haonekani sura kuanzia alivyoingia mpaka anaondoka.
Kumbe wakati ananiongelesha alichukua mfuko kutoka kwenye mfuko wa suruali lake akaukunjua na kuchukua pochi yangu ilokuwa juu mahali naandikia na kuitumbukiza kwenye mfuko wake kisha anatoka zake nje yuule.
Nilipiga kelele kama kichaa nikaombwa namba ya baba akapigiwa simu aliongea tu kiustaarabu rudi tu nyumbani mwanangu kuibiwa ni kawaida mwenyewe nimeshawahi kuibiwa pole usiwe na wasiwasi.
Wakati naendelea kulia ndani ya benk kuna baba mtu mzima anaamua kunisaidia kuanzia kwenda kuangalia kwenye CCTV. Ananipeleka polisi central kutoa taarifa tunapigwa danadana. Tunaambiwa turudi kesho yake. Nawaza narudije nyumbani, baba nimeshaongea nae je wale watu yaani baba yangu mdogo na mke wake itakuwaje.
Baba ananipigia ananisisitiza nirudi nyumbani tena kwa upole. (NAMPENDA SANA BABA YANGU YEYE NI SHUJAA WANGU) basi narudi nyumbani ile kuingia ndani tu babamdogo anaanza ee Lisa kama ulikuwa hutaki shule si ungesema yaani hela hile yote umeenda kuionga si bora ungeiacha kaka yangu angefanyia kitu kingine. Simjibu nanyamaza tu. Baba kila muda ananipigia simu na kunambia usiwaze mwanangu haikuwa riziki ananitmia jumbe za kunitia moyo. Yaani baba hakunilaumu wala sijui kufanyaje kuhusu pesa ile mpaka leo kuna amani kati yangu na baba yangu. Namuomba Mungu aendelee kumlinda baba yangu.
Kila siku naenda polisi central hamna jipya zaidi ya kuambiwa kuwa upelelezi unaendelea. Na kila nikienda nampa baba yangu tarifa nachoambiwa baba akaniambia niache kwenda polisi hamna msaada wowote na nisahau kuhusu hiyo hela Maisha mengine inabidi yaendelee. Ila kuhusu shule itabidi nisubiri tena labda mwaka mwingine tena ajipange upya make sasa hivi hela imemuishia make analipa na ada ya wadogo zangu pia. Nimemwelewa baba na kuendelea kutulia nyumbani.
mchana mwema
Sijawahi kuona Bamdogo wa hivi 😅😅😅nawajua wana roho nzuri sana huyu ni kiboko.Ep 12
Nimeamua kuvunja ukimya.
Ilikuwa likizo mdogo wangu ndio wamemaliza mtihani wa kidato cha nne anasubiri matokeo. Jumapili asubuhi ameenda kanisani misa ya kwanza. Muda umeenda hajarudi tumeenda kuangalia kanisani hayupo simu yake inaitia chumbani kwake hajaenda nae. Tumetafuta mpaka tumechanganyikiwa ni jioni imeingia.
Baba mdogo ameichukua simu ya dogo anajaribu kutoa password mwisho anafanikiwa anangalia simu yake ya mwisho kupokea ni jina la msichana tena ndugu yake mtoto wa shangazi yake wanajaribu kumpigia anapokea mwanaume vita ikaanza mama yake anataka aniangushie tena msala kama wa ile simu aliyokuwa amemnunulia. Itakuwa Lisa ndo anamwaribu mdogo wake atakuwa anajua alipo. Ananisogelea anataka kunipiga kofi nikalikwepa na kumwambia mamdogo sijawahi kukuvunjia heshima mimi sio ngoma yako makosa afanye mwingine niadhibiwe mimi kwa hili utanisamehe wala usijaribu tena kuninyanyulia mkono wako la sivyo nitasema maovu yako mbele ya mume wako.
Anamugeukia bamdogo unamwona mwanao siku hizi jeuri toka ajue baba yake ana nyumba ana mahali pa kwenda anajibu anavyojisikia. Nikamwambia mamdogo unasahau kuwa ile simu wewe ndo ulimnunulia mwanao na mkaniangushia mimi msala tena mkachangia kunipiga na bamdogo. Bora ungekaa kimya siku hiyo kuliko kunipiga na kunitukana ili uonekane mwema. Mimi sio mbuzi wako wa kafara na toka siku hiyo sijawahi kukusamehe.
Duh siku hiyo ilikuwa vita sana mdogo wangu alivyorudi walipigwa sana na mama yake mpaka nikawaonea huruma. Kumbe dogo alikuwa kwa shemeji.
Siku zimeenda kweli kweli nakaribia kumaliza mwaka nipo tu nyumbani. Maisha hayaelewiki. Kila jumamosi huwa naenda kusali jumuiya. Kuna rafiki yangu huwa tunakutana kwenye kusali changamoto zake na zangu hazitofautiani sana. Yeye anaishi na kaka yake na mke wake naye vitimbwi kama vya kwangu.
Siku moja ananitumia ujumbe Lisa jitahidi ufanye juu chini tukutane jumuiya nina jambo la kukwambia. Jumamosi imefika nimeenda kusali jumuiya baada ya kumaliza kusali ananiambia Lisa si unajua kutumia computer? Namwambia ndio kuna mtu anatafuta mfanyakazi wa stationery kama hupo tayari kesho tukienda kusali kanisani nitakupeleka ukaonane nae kama mkielewana jumatatu uanze kazi, nikamwambia sawa.
Basi jumapili tumeenda kanisani tulivyotoka kanisani tukapita kwenye stationery sio mbali na kwetu ni kama dakika 20 tu kwa kutembea. Boss ananifanyia interview kidogo. Ananipa kazi mshahara laki moja na nusu na tunakubaliana kesho nianze kazi (jumatatu) rafiki yangu ananiuliza kwenu watakubali namwambia yaani wakubali au wakatae mimi kazi lazima nifanye nitakaa ndani mpaka lini?
Nafika nyumbani babamdogo ananiuliza mbona umechelewa leo na misa ya kwanza imeisha tu muda? Bamdogo nilipita sehemu (namtajia mtaa ilipo stationery) kuonana na boss nimepata kazi.
Kazi gani? Namjibu ya stationery akasema sawa unaanza lini nikamjibu kesho. Unalipwa sh ngapi. Namjibu laki moja na nusu. Akaniuliza atakupa hela ya kula na nauli? Nikasema Hapana kila kitu kipo humo humo ila hata kama nitabaki na elfu hamsini tu kwangu ni kubwa sana. Isitoshe situmii nauli akasema sawa. Moyoni nikawaza mbona amekubali haraka hivyo huyu anawaza kufanya nini tena.
Nikaendelea na shughuli zangu za nyumbani kama kawaida. Mpaka usiku unaingia hatujaongelea tena swala la kazi. Mke wake sijamwambia chochote nikiamini mume wake atamwambia.
Jumatatu imefika nimeamka mapema sana ili niache nimefanya kazi za nyumbani. Nimefanya kila kitu nimemaliza wao wameamka tayari wapo mezani wanakunywa chai ili na wao waende kazini najiandaa natoka nje hata chai sijanywa nawaaga kuwa naenda kazini. Baba mdogo anasema kumbe ulikuwa siliazi? Namwambia ndio akasema rudi ndani uendelee na shughuli zako. Mimi vitimbwi vyao nimeshavizoea havinitishi tena namjibu bamdogo nimekaaa sana ndani siwezi kuruhusu kuipoteza nafasi hii kwa gharama yoyote ile tutaonana jioni nafungua mlango mimi yule naenda zangu kazini.
Bosi kaja na kunikabidhi ofisi, ananielekeza sehemu ya kuacha funguo jioni na kuondoka zake. Ofisi inafungwa saa moja jioni. Nimeshida zangu ofisini muda wa kurudi umefika nafunga ofisi napeleka funguo na kurudi zangu nyumbani. Nimefika nyumbani saa moja na nusu hivi nawakuta wao wamesharudi mamdogo anaangaika na jiko. Baba mdogo anaanza kazi gani unarudi usiku mshahara wenyewe mdogo ona mpaka sasa chakula hakijapikwa mama yako anaangaika peke yake jikoni. Siku hizi nina ujasiri namjibu bamdogo itabidi mzoee tu hamna namna nimekaa sana nyumbani na mimi nina mahitaji yangu binafsi.
Lisa umekua sasa unajibu siku hizi unajibu chochote unachojisikia. Simfatilii sana naungana na mama mdogo jikoni tunaendelea kupika huku kanuna. Mimi wala simfuatilii tena. Nimefanya kazi kama wiki hivi jioni moja bamdogo akaniambia itabidi niache kazi yangu ya kijinga niende kariakoo kuna stationery ya rafiki yake ameshanifanyia mpango nifanye kazi kwake. Nikamwambia sawa hamna shida nitaangalia maslahi nikamuuliza amekwambia atanilipa sh ngapi? Akasema utaenda kujua huko huko.
Nikamwomba boss wangu ruhusa na kwenda kariakoo kwa rafiki yake bamdogo, nilivyofika pale nimejitambulisha akasema ndo umekuja kuanza kazi nikamwambia Hapana nataka nijue kwanza utanilipa sh ngapi akanijibu tumeshaongea na baba yako anajua kila kitu hajakwambia? Nikamwambia hajanambia kitu ngoja nirudi tu nyumbani nikishaongea nae nitakuja nikaondoka. Moja kwa moja nikaenda kazini kwangu. Jioni nimerudi nyumbani naulizwa kama natokea kariakoo. Nikamwambia kazi ya kariakoo siitaki siwezi kufanya kazi ambayo sijui nitalipwa sh ngapi.
Kumekucha nimefanya kazi zangu ninaaga kuwa naenda kazi naulizwa kama naenda kariakoo nikamwambia kuwa siendi kariakoo na kazi ya kariakoo sihitaji.
Bamdogo ananiambia kuna option mbili tu kati ya mbili nichague moja nikafanye kazi kariakoo ndio niendelee kuishi kwake au niendelee na kazi yangu nayofanya sasa hivi niondoke nyumbani kwake. Nikamwambia nitaendelea na kazi yangu na nitaondoka kwako hakutegemea kama ningeweza kumjibu vile yaani kipindi hiki simwogopi kabisa. Akanambia amenipa notisi ya mwezi mmoja ukiisha tu niwe nimempisha kwake. Nikamwambia hakuna shida.
kwa ufupi nimepewa notisi ya mwezi mmoja.
Muwe na jioni njema.
pole mwayaIla hii mijizi Mungu anajua 😅😅nimeishatapeliwa mara tatu nimekoma mimi 🙌🏼😅
sasa hivi ni rafiki yangu sanaSijawahi kuona Bamdogo wa hivi 😅😅😅nawajua wana roho nzuri sana huyu ni kiboko.
Kama hivo ni vizurisasa hivi ni rafiki yangu sana
Yaani asante sana dearpole mwaya
ulisoma shule gani morogoro kidoti na kwa shangazi yako forest anaitwa nani ukute jirani yanguEp 8
Naanza shule kumbe shule yenyewe ni kwa ajili ya kurudia mtihani wa kidato cha nne baba hajawahi kuonekana mbele ya macho yangu zaidi ya kuongea kwenye simu tu. Kipindi cha shule kilikuwa kigumu sana. Baba anatuma pesa kupitia simu ya mamkubwa kwa ajili ya nauli na matumizi mengine lakini napewa hela ndogo nauli napewa mitano tu na ni sehemu ya kupanda daladala mbili kwenda na kurudi ni mianane hapo hujanywa hata maji. Nalikuwa naambiwa kuwa wakati wa kwenda shule niwe nawahi kutoka nitembee kwa mguu alafu wakati wa kurudi sababu tunachelewa kutoka ndo nipande daladala.
Kwa bamkubwa hawana umeme wala solar hivyo wanatumia vibatali. Japo majirani zao wote wana umeme. Hivyo nilikuwa na bajate yangu ya kununua mafuta yangu kwa ajili ya kujisomea usiku siruhusiwi kutumia mafuta ya familia. Watoto wa mamkubwa wakawa wananichezea mchezo nikinunua mafuta wananivizia wanamwaga maji chini wanachukua mafuta yangu na kunambia kuwa mafuta yangu yamemwagika.
Namshukuru Mungu baba alikuwa anamwelewa shemeji yake yaani mamkubwa hivyo akituma pesa kwa mamkubwa ananitumia na mimi kisiri hayo ndo yakawa Maisha yangu ya shule. Masomo yalikuwa yanaanza saa sita mchana na kutoka jioni saa kumi na moja mpaka uje ufike nyumbani saa moja mpaka saa mbili.
Nimeshazoea mazingira naona sawa tu. Ukinywa chai asubuhi mpaka cha usiku na ukichelewa kufika nyumbani ukakuta wameshakula hawakuwekei chakula utasubiri asubuhi chai. Nilivyoona vile nikasema Lisa ukiendelea kuwa mzembe utakufa kwa njaa hapa. Kumbuka nalala na kuku tena wa kienyeji hivyo namimi nikaanza kuiba mayai usiku naiba mayai yangu matatu naweka kwenye begi naenda nayo shule napita kwa muuza chips nampa mayai matatu na sh miatano jioni napita nachukua chips yangu yai tena nakula nikishiba ndo narudi nyumbani. Nikute wamekula hawajala wala sina mpango na chakula chao. Mamkubwa anamwambia baba mwanao ameanza kuwa na wanaume huyu akirudi hali chakula nyumbani kila siku anasema kashiba kumbe mie najisevia mayai na hawakunigundua mpaka natoka pale.
Dav ananitafuta yeye anasoma Mzumbe University mawasilano yanakuwa nikiwa shule kama weekend mara kwa mara anakuja kunitembelea. Siku nyingine anakuja na marafiki zake ananitambulisha kwao kama mdogo wake. Tunaanza kuishi Maisha ya dada na kaka na Dav ananisaport vitu vidogo vidogo.
Shule na Maisha kwa bamkubwa hayakuwa rahisi hata kidogo. Kusimangwa kwa vitu vidogovidogo. Kuibiwa hela ukitoka tu wazee wanazama wanakupekua mpaka unasema nini hiki hata wakikutana n amia wanasepa nayo. Matokeo nimefeli tena.
Baba anarudi kutoka Tanga nafurahi kumwona baba amerudi amechoka hana nuru baba yangu yaani kazeeka sana. Baba nae hana pa kuishi amefikia pale kwa kaka yake. Hakuna kipindi nachukia kukikumbuka kama kipindi hiki.
Baada ya kufeli tena naambiwa nije dar kwa baba mdogo nije wanitafutie kozi yoyote nisomee. Hapo haulizwi kuwa utaenda au utaenda ni amri tu inatolewa nawe unafuata. Namshirikisha Dav ananiambia kwanini wanakwambia uende dar? Lisa unapita magumu sana huko dar unapoenda hujawajua bado kama ilivyokuwa kwa baba yako mkubwa na je ukikuta mambo ni magumu zaidi ya hapa utafanyaje? Kaka Dav ngoja niende itakavyokuwa hivyo hivyo sina jinsi tena. Natamani kurudi kijijini lakini siwezi ngoja nione Dar itakuwaje labda nitapata mwanga kidogo.
Dav anajua kwa uchache baadhi ya mapito yangu sababu namshirikisha na amekuwa mshuri wangu mkubwa sasa.
Nimefika Dar kwa baba mdogo Watoto wake wapo shule wanasoma boarding wapo na mdada wa kazi. Mazingira ni mazuri tu mama mdogo ndo anapewa jukumu la kufuatilia nafasi za chuo. Tunaenda magogoni tunakosa nafasi tunaambiwa nisubiri mpaka muhula mpya.
Wakati naendelea kusubiri natembezwa kwa baadhi ya ndugu zangu baba zangu wakubwa na wadogo ni wapo wengi sababu babu alikuwa ameoa wanawake watatu kwahiyo alikuwa na Watoto wengi. Wengi wao wapo hapa Dar na baadhi yao wamejipata wengine ndo hivo tena.
Ruti za kuzunguka kwa ndugu zangu zinaendelea napelekwa mpaka kwa mjomba wangu ambae anaishi na mdogo wangu tunayezaliwa tumbo moja kwa baba mama toka amezaliwa sijawahi kumwona nina hamu kubwa sana ya kukutana na mdogo wangu Joy (si jina lake)) nafika kwa mjomba joy ndo anafungua geti mzuri sana anafanana na baba copy na paste nieleweke baba nae ni hansome hivyo Joy japo nakufanana na baba ni mzuri sana.
Namkimbilia Joy kumuwao ananikwepa yaana hata kiherehere na mimi hana kabisa hii moment huwa inaniuma sana.
Nimeambiw nitakaa pale wiki mbili ili tuweze kuzoeana na Joy. Joy anaanza kulia na kumwambia mjomba kuwa hataki kuniona na ni bora ningekuwa nimekufa tu.
Kinaitwa kikao na mama anakuja Joy analazimishwa aniombe msamaha tena kwa kupiga magoti. Joy ananiomba msamaha kwa kulazimishwa ila bado ananichukia.
Mama naye analazimishwa twende naye kwake tupajue anapoishi. Mama anakubali kishingo upande. Njiani anatupa somo sikia nyie Watoto tukifika nyumbani sitaki kusikia mtoto hata mmoja ananiita mama yake atakayethubutu kufanya hivyo nitakachokifanya atasahau kuwa mimi ni mama yake niiteni shangazi mnasikia nyie wajinga wawili. Nimemnukuu mama.
Tunafika kwa mama kumbe mama ameolewa na mwanaume mwingine ana hela chafu mama anaishi kama malkia. Mume wa mama anamwambia mbona Lisa anafanana sana na wewe. Mama anajibu lazima tufanane sababu mimi ni shangazi yake.
Nimechoka uwii kuandika si mchezo.
Alfa James ila jina la shangazi yangu kapuni asanteulisoma shule gani morogoro kidoti na kwa shangazi yako forest anaitwa nani ukute jirani yangu