Kuna wengine hatujui tulipokosea

Kuna wengine hatujui tulipokosea

Yani siku zote omba mwanamke akupende hata misamaha utapata


Na hii inatupa picha halisi kwamba,kwanini mwanamke hata akiolewa maadamu kuna mwanaume ambaye anampenda kwa dhati basi utachapiwa tu

So guys relux,achaneni na haya mambo ya kuchunguza simu za wenza wenu mtakutana na msicho kifurahia
 
Ep 19

Pigo la tatu.


Tabia ya mtu ni Ngozi kuibadilisha ni vigumu Dav haimbiliki wala hasikii. Kama ilivyo kawaida tukimisiana mmoja lazima amfuate mwenzake. Baba D amenitumia nauli niende Moro kama ilivyo kawaida yangu naondoka ijumaa jioni kutoka ubungo.

Siku hiyo gari niliyopanda ilipata shida kidogo njiani hivyo ilitupelekea mimi na abria wenzangu kufika stand ya msamvu usiku mkubwa sana. Wakati tupo njiani tunawasiliana na baba D nikimwambia tumefika hapa tumefika hapa. Hivyo nilivyofika tu Msamvu nilimkuta baba D ananisubiri amakeja kunipokea.

Tupo njiani sioni baba D aniulize nakula nini sababu ndo ilikuwa kawaida yake baba D kuniuliza unakula nini ili anunue chakula. Tulipofika nyumbani baada ya kumaliza kuoga baba D ananikaribisha chakula. Nilimuuliza baba D umepata wapi chakula? Akaanza kusema mama D hivi huamini kama mimi najua kupika? Wewe tangu lini ukapika leo ukapika ninavyokujua ulivyo mvivu wewe. Nimekupikia bwana ebu njoo ule uache maswali yako. Haya baba D ngoja leo nionje mapishi yako. Wali umepikwa umepikika sijui uliwekwa nazi mboga nazo zimeungwa na nazi. Nikala mimi mtoto wa watu huku nikijiuliza ameanza lini kupika huyu chai yenyewe kuchemsha kwake ni mtihani. Iweje leo amepika tena mpaka nazi. Nitapata jibu tu. Nimekula tumelala zetu.

Asubuhi nimeamka kama mnavyojua wadada tunajifanyaga wife material tukifikaga kwa maboyfriend zetu. Nilikusanya nguo chafu nimefua lakini ikifika muda wa kusuuza baba D ananiwahi anasuuza na kuanika yeye tulikuwa tunafulia ndani, tumeosha vyombo tumemaliza nimedeki ndani nataka nitoke nje kudeki barazani akaniwa mama D acha tu nitamalizia mimi nikamwachia huku nikimshangaa ana nini huyu. Ameniacha napika chai akaenda kununua vitafunwa.

Tumepanga jioni twende kumsalimia mama yake (nieleweke Dav ni mtoto wa mama) tumekunywa chai. Muda wa kupika umefika namfuata baba D na kumuuliza tunapika nini? Akanijibu mama D wewe kampuzike tu mtu umefika usiku mkubwa kufua na usafi utakuwa umechoka sana. Kwa hiyo kuhusu chakula nitashughulikia nikasema sawa. Kusema ukweli nilikuwa nimechoka sana baba D yupo bize na laptop yake. Nikaamua kwenda zangu chumbani kupumzika nilipitiwa na usingizi. Nakuja kustuka baba D ananiamsha nikale. Nimeamka baba D kanibeba mpaka sebuleni nakuta chakula kimeshatengwa.

Baba D naomba unieleze ukweli hiki chakula kimetoka wapi toka usiku bado najiuliza umewezaje kupika chakula kama kile? Nakujua wewe ni mvivu chai tu inakushinda inakuwaje chakula tena mpaka nazi?

Mama D acha wivu ebu tule bwana. Si unajua tutaenda bibi D tena ngoja nimpigie simu hapa.

Usinizuge kwahiyo bibi D ndo amepika hiki chakula? Ananizuga zuga pale mwisho natulia tunakula lakini kichwani nikijisemea lazima nijue kinapotokea hiki chakula.

Tumepumzika jua limepungua tumejiaandaa hao kwa bibi D. Tumefika kwa bibi D ametupokea vizuri lakini mazungumzo ya bibi D anasisitiza ndoa hataki tuendelee kuishi Maisha haya tunayoyaishi mmoja Dar mwingine Morogoro sio mazuri kabisa. Tunamwaahidi bibi D kuwa tutalifanyia kazi hivi karibuni. Tumeongea sana na bibi D jioni imeingia bib D anatufukuza akimsisitiza Baba D anirudishe nyumbani mapema. Hajui kama tumelala wote na sasa naenda tena kwa baba D.

Tukaondoka zetu tumefika nyumbani usiku saa mbili nataka kupika tena ananizuia kuwa nisipike. Na kila kitu kipo ndani nikajifanya mjinga ili nijue chakula kinapotokea.

Huku nikijichekesha chekesha kinafiki nikambwambia sawa nipo chumbani nimepunzika kidogo. Poa nitakuamsha uje kula.

Nipo chumbani kama dakika 20 hivi Dav akaja kuanza kuniita mama D, Mimi kimya mama D…. Lisa Lisa. Mimi nikajifanya nimelala usingizi mzito. Dav akatoka chumbani nikamsikia anaongea na simu akisema Baby waweza kuniletea hicho chakula. Mke mwenzio amelala fanya haraka asije akakusikia sababu naona ameanza kuwa na mashaka.

Nikasema shenzi huyu kumbe hanunui chakula kinapikwa tena na mtu amemuita baby. Nikakaa chonjo ili nimuone huyo mpishi.

Baada ya kimya kidogo nikasikia Watoto wanaita anko Dav tumeleta chakula. Aisee mapenzi yanauma. Nilitoka chumbani sikujua nilipitaje sebuleni nikajikuta nipo nje Dav anapokea kile chakula. Nikamshika mtoto alikuwa kama miaka sita hivi nikamuuliza ehe mtoto nani amekupa chakula hiki akasema mama ndo amesema tumletee anko Dav. Nikakishika kile chakula nikarudishia mtoto nikimwambia kamwambie mama kuwa mke wa anko dav ameshapika.

Dav alichukua kile chakula na kunipiga makofi mawili matakatifu na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kunipiga lakini sikukubali nikamwambia Dav kwa usalama wetu naomba hiki chakula kirudi kilipotoka au mimi niondoke ubaki na chakula chako. Niliingia ndani nikachukua mizigo yangu tayari kwa safari. Dav akanizuia. Nilinyamaza na kuanza kulia Dav alivyotulia nikachukua simu nikampigia mama Dav na kumweleza kila kitu huku nalia kwa kwikwi. Dav akiwa bafuni. Mama Dav alichukua bodaboda na kuja pale Dav hakuamini kama ningeweza kufanya hivyo. Basi mama alilalamika sana vijana wa siku hizi tusivyokuwa na maadili mimi moyoni nasema Dav kamwaga mboga na mimi nimemwaga ugali kama tunaachana sawa tu,

Basi mama akaniuliza nataka nini nikasema nataka aliyepika chakula aitwe na akanywe aache kabisa kumpikia Dav chakula. Mama akakubaliana na mim akamwamuru Dav kumpigia simu huyo mpishi. Kweli yule dada alikuja lakini wakajitetea kuwa Dav huwa anampa hela anampikia. Wamepanga nyumba moja lakini aprtiment tofauti.

Mama akalalamika sana mimi ndio maana natamani muoane hata leo yaani ningekuwa mwislam leo ningewapiga ndoa ya mkeka. Fanyeni haraka muoane mimi sipendi Maisha yenu ya kihuni haya. Mgekuwa mnaishi pamoja haya yote yasingetokea. Mama akaacha hali hiko poa akaondoka hakuna aliyeongea na mwenzake mpaka asubuhi niliondoka pasipo kumuaga Dav.

Nilimtumia ujumbe Dav imekwisha sasa endelea kubaki na huyo anayejua kupika mimi sijui kupika. Dav hakunijibu. Nilirudi zangu Dar na kufikia kwa shoga yangu Jack ila nikiri Mungu amenipa huyu mtu. Jack nakupenda sana kipenzi unajua kubebamatatizo yangu. Nikilia nalia nae asant Jack.
natamani kumaliza jamani.
 
Back
Top Bottom