Kuna wengine hatujui tulipokosea

Kuna wengine hatujui tulipokosea

Zawadi pekee ya mtoto wako kama wewe unaona kabisa sina utajiri mkubwa kama wengine wakubwa basi ni kumpa malezi Bora ya baba na mama.
Kuna raha ya mtoto wako kuona anapendwa Toka akiwa mdogo
bila uwezo wa MUNGU peke yangu siwezi ila nina imani Mungu atanisaidia
 
Ila kama hujaolewa na Dav anataka kukuoa mkubali tu. atakuwa keshajifunza mengi. Na wewe pia una mtoto hivyo kama akitaka kukuoa mkubalie tu, chansi ya wewe kuolewa ukiwa na mtoto ni ndogo.

Ujana una mengi na wanaume wengi huwa wanafeli na wanapoteza wife material sababu ya ujana.

Binafsi namependa Dav we msamehe tu ila mpe masharti akiyafuata mkubalie tu
Dav ananitamani leo kesho. mimi nimepita matatizo mengi hvyo hata wazo la kuolewa sina kabisa akilini mwangu.
 
Dav anasali au kuswali popote, Binadamu yeyote kama anamwamini Mungu na akawa serious na Mungu lazima afike mahali abadirike tabia, kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa, maisha yetu haya hapa duniani hatuwezi lolote bila Mungu.

Kumcha Mungu, kwenda kanisani/msikitini ni njia bora ya kurekebisha tabia, pesa au elimu haviwezi kumsaidia mtu yeyote hapa duniani kama hana Mungu,

Vitabu vitakatifu vinasema Pesa no chanzo cha mabaya ya kila aina hapa duniani!!

Tumche Mungu, tutakuwa na hofu ya Mungu!!
 
Maisha ni maamuzi, ili mtu aishi hapa duniani sio lazima awe ameoa au ameolewa, mtu aishi vipi hapa duniani ni maamuzi yake na wala hakuna kanuni ya kuishi,

So kuishi single sio dhambi kwa mwanaume na
mwanamke, cha msingi usimkwaze mtu katika u-single wako!!
 
bila uwezo wa MUNGU peke yangu siwezi ila nina imani Mungu atanisaidia
Najua utafanikiwa mkuu tena sana pia najiuliza why umekimbia majukumu Yako kama mke. Kwa dav.

Fatilia kuhusu post moja ya huyu mtu anaitwa masai dada then utajua kuwa hata baadhi ya shida kwenye ndoa huwa zinafika ukomo na maisha yanarudi kama mwanzo.

Ungejipa mda tu then Kila kitu kingekaa sawa.
 
bila uwezo wa MUNGU peke yangu siwezi ila nina imani Mungu atanisaidia
Sisemi natetea kuhusu dav Wala usinifikirie hvyo ila hata Mimi leo nikikaribia kuoa lazima nimalize na vipengele vyangu Kwa show Kali ili niweke commitment na mambo yanaendelea.

Kuna story Moja huko Nigeria nafikiri ilitokea baba anachepuka na mama kazuia lkn mchepuko ulituma Hadi video ya mmewe akiwa anapiga yowe Kwa mauno ya mchepuko Kwa mkewe ili kukwambia kuwa hakuna lolote utakalo Fanya.

Mke aliomba sana Kwa imani yake na mambo yalirudi kama mwanzo na badae familia ilikuwa sawa.

Amani ya Mungu ni Amani ya kweli na Wala sio amani ya kuwa single mother.
 
Maisha ni maamuzi, ili mtu aishi hapa duniani sio lazima awe ameoa au ameolewa, mtu aishi vipi hapa duniani ni maamuzi yake na wala hakuna kanuni ya kuishi,

So kuishi single sio dhambi kwa mwanaume na
mwanamke, cha msingi usimkwaze mtu katika u-single wako!!
asante
 
Najua utafanikiwa mkuu tena sana pia najiuliza why umekimbia majukumu Yako kama mke. Kwa dav.

Fatilia kuhusu post moja ya huyu mtu anaitwa masai dada then utajua kuwa hata baadhi ya shida kwenye ndoa huwa zinafika ukomo na maisha yanarudi kama mwanzo.

Ungejipa mda tu then Kila kitu kingekaa sawa.
usaliti unauma sikia kwa mtu omba yasikukute. navyomfahamu Dav ingekuwa yeye ndo alinifumania. pale ningetolewa maiti. nilivumilia mengi. mpaka alitembea na mdogo wangu lakini bado nilisamehe. hapana kwakweli sina chuki nae ila pia kurudi kwake siwezi.
 
Ila kama hujaolewa na Dav anataka kukuoa mkubali tu. atakuwa keshajifunza mengi. Na wewe pia una mtoto hivyo kama akitaka kukuoa mkubalie tu, chansi ya wewe kuolewa ukiwa na mtoto ni ndogo.

Ujana una mengi na wanaume wengi huwa wanafeli na wanapoteza wife material sababu ya ujana.

Binafsi namependa Dav we msamehe tu ila mpe masharti akiyafuata mkubalie tu
haha team Dav jamn mnataka akaniue
 
usaliti unauma sikia kwa mtu omba yasikukute. navyomfahamu Dav ingekuwa yeye ndo alinifumania. pale ningetolewa maiti. nilivumilia mengi. mpaka alitembea na mdogo wangu lakini bado nilisamehe. hapana kwakweli sina chuki nae ila pia kurudi kwake siwezi.
Sawa mkuu.
 
Dav ananitamani leo kesho. mimi nimepita matatizo mengi hvyo hata wazo la kuolewa sina kabisa akilini mwangu.

Kama wewe huna mume na yeye hana mke basi usiendelee kumkatalia. Kila mmoja wenu keshajifunza kwa yaliyomkuta.
Dunia ina mengi sana huyo ndio mumeo urudi sasa kwake. Kama ana mtoto alizaa huko nje chukua lea pamoja na huyo wa kwako. Kama hana basi umzalie kabisa muwe familia. mfunge ndoa lakini muache kuzini.

Atakuwa anajuta sana na kwa aliyopitia, atakuwa keshaacha utoto. sasa hivi akili zimekaa vizuri.

Hebu mpe nafasi akirudia ujinga tena basi nitakuwa upande wako.
 
realMamy njoo umuone team Dav mwenzako. 😛
 
Ep 21

Siku zilienda Dav hakuamini kama ningesema basi. Nilirudisha pete kwa mhuisika Dav hakuamini kama ningemwacha nilimwambia kuwa siku ukiona umebadilika na unaweza kuniheshimu japo kidogo na kutulia utanitafuta ila sio kwa sasa Dav nahitaji kupumzisha akili yangu sasa. Nikikaa sawa nitakwambia ila sidhani kama naweza kukusamehe. Hivi hatujaoana Dav huko hivi ukiniweka ndani ukajua tayari nipo chini ya himaya yako itakuwaje. Kinachoniuma mwanamke yuleyule toka umepanga mpaka umejenga kwako bado tunakosana kwa sababu yake. Kitanda kilekile ninachokilalaiaga mimi bora mgeenda sehemu nyingine si hapa. Au ningewakuta sehemu nyingine sio hapa kwako ningekusamehe kabisa. Au angekuwa mwanamke mwingine siku ile si ulikana ukasema ulikuwa unampa hela ili akupikie na hapa alikuja kukupikia tena sababu unampa hela? Dav alilia sana, alinipigia magoti lakini sikujali kilio chake wala magoti yake niliondoka zangu nikawaacha kwenye kikao na nikaazimia kumuondoa Dav kabisa Dav kweye Maisha yangu na nilifanikiwa kumuondoa mazima.

Mahusiano yangu na Dav yalidumu kwa miaka mitatu na miezi minne na kipindi chote hicho japo ilikuwa long distance relationship sikuwahi kumsaliti wala kuwaza kufanya hivyo mpaka tunaachana. Nikawa bize na Maisha yangu japo ilikuwa ngumu lakini mwisho wa siku niliamua kukubali matokeo.

Maisha yana pilika pilika nyingi sana. Kwenye heka heka za hapa na pale nikakutana na kijana mwingine mtanashati ni daktari katika hospitali kubwa hapa dar alinisumbua kwa kipindi cha mwaka na zaidi. Nilishamtoa Dav kwenye akili yangu nikaamua kuwa naye ila kumbe yule jamaa alikuwa ameoa na ana Watoto watatu familia yake inaishi mkoani lindi.

Nilivyogundua tu sikutaka kuangalia nyuma wala sina cha kupoteza kwake nikakimbia futi mia. Hakuna mtu namwogopa kama mume wa mtu. Maisha yalisonga nilikaa single miaka miwili yaani mtu akiniambia habari za mapenzi simwelewi kabisa hata kidogo. Nikaamua kujikita kwenye kazi zangu.

Nikaja nikakutana na huyu mpendwa namaanisha mlokele ni mtu maarufu kidogo nikaanza nae mahusiano nikiamini huyu ni mtumishi wa Mungu hawezi kunitenda. Msinilaaumu jamani Lisa nakula nashiba kuna siku tulijikuta tumevunja amri ya sita hata sielewi ilikuwaje. Mungu naye hakuwa mbali jamani mimba hiyo. Nikalea mimba yangu mpendwa yule naye kumbe ni silent killer ana matukio yake pia. nikaamua sasa kuwa bize na mimba yangu.

Namshukuru sana Mungu alinijalia handsome boy mwanangu ana miaka miwili sasa ananipa kila sababu ya kupambana. Sasa hivi nina amani na katoto kangu nikiwa single mother.

Kuhusu nyumba ya antie aliyokuwa anajenga niliimalizia na document zake ninazo mimi siku yoyote akitokea nipo tayari kumpa pasipo kudai chochote kile.

Dav alikuja kuoa mwanamke mwingine lakini walishindwana. Walikatana mpaka mapanga wakapelekana mpaka mahakamani. Dav siku hizi ni chapombe ana midevu kama osama yaani usmat ule hana tena nilikutana mwaka juzi nilivyooenda kumsalimia baba tulikutana mjini bahati mbaya nikiwa na kichanga aliumia sana. Kuna siku huwa anamfuata baba yangu na kuanza kumsumbua baba kuwa mimi nimke wake anamtaka mke wake nilimwambia baba ampeleke polisi. Ila baba hataki anampenda Dav ila mimi nilishakula viapo na viapo siwezi kurudi tena kwa Dav. Simchukii nilishamsamehe kabisa ila pia simpendi namchukulia kama mtu wa kawaida tu.

Mama naye yupo south Africa kuna kipindi aliumwa sana alipata ajali akateguka mguu akawa anahitaji msaada wetu ndugu zake wakatwambia kuwa twende kumuuguza tukagoma sio mimi sio Joy alikubali kwenda south Africa kumuuguza ilibidi aende mdogo wake. Alivyopona tu alikuja Tanzania akatuomba msamaha, tulimsamehe hivyo alirudi south kuendelea na Maisha yake ila tuko poa kabisa. Joy naye anaendelea vizuri mwezi wa 7 tunatarijia kula ubwabwa mdogo wangu antarajia kufunga ndoa. Hatuna ukaribu wa kivile ila tunawasiliana japo kidogo kidogo.

Baba naye ndoa yake inapumulia gas walitengana chumba na mama yetu wa kambo na mdogo wetu ni mdangaji maarufu Morogoro mjini. Yaani ni ameshindikana. Kwa baba mimi na Joy tuliacha kwenda kabisa nina miaka mitatu toka nilivyoenda mwaka 2021 sijawahi kukanyaga tena. Nikimmisi baba yangu huwa najitahidi kwenda na mabus ya kufika mapema moro na mtoto wangu tunafikia ofisini kwa baba jioni tunaru zetu Dar naondoka juu kwa juu.

Katika hekaheka zote hizo nimefanikiwa kujenga kakibanda kangu kadogo kazuri japo si kivile lakini kanaridhisha kapo Mbezi Msumi. Nitaarajia kuhamia kabla ya pasaka mwaka huu. Nina amani furaha na afya njema mimi na mtoto wangu tuko poa kabisa.

Sijutii kuwa single mother sababu mtoto wangu ananipa kila namna ya kupambana na ndiye mtu pekee niliye naye katika Maisha yangu japokuwa ni mdogo lakini ananipa furaha. Nina amani na sasa hivi naufanyia kazi msemo wa Joy naishi ulimwengu wangu kabisa. Mwanangu ndiye dunia yangu.

Asanteni kwa kuwa na mimi, niliyemkosea au kumkwaza kwa namna moja ama nyingine naomba anisamehe. Na samahani kwa kuwachosha ila nina Imani kuna mtu japo mmoja amejifunza kitu kutokana na historia ya Maisha yangu.

NAWAPENDA!

Mwishooooo.
Asante na mm nna mpenz Wang namsaliti sasa nmeamua kuacha kabsa ya dav yasje nkuta
 
Back
Top Bottom