Kuna yeyote aliyeona mabadiliko yoyote katika uwanja wa Mkapa?

Kuna yeyote aliyeona mabadiliko yoyote katika uwanja wa Mkapa?

Baada ya kutazama mchezo wa Azam hapo jana, Binafsi sijaona mabadiliko ya maana katika uwanja wa Mkapa licha ya mabilioni yaliyomwagwa, kufungiwa kutumika mara kwa mara na muda mrefu kupita tangu ukarabati huo uanze.

Pitch bado haina mvuto kama ilivyo kwa viwanja vingine vikubwa, LED Display za matangazo hazifanyi kazi wala sijaona kama zimeboreshwa, angalau zingefungwa double juu na chini kama uwanja wa Amahoro hapo Rwanda, Hakuna TV kubwa uwanjani. Sasa kipi kimefanyika hapo?? Hata hiyo tarehe 8 siku ya derby ninaona bado uwanja hautakuwa na maendeleo yoyote, pitch LED Display haziwashwi wameweka mabango tu kama viwanja vya mikoani. INAKERA SANA!
Watakula wapi, swali he taa zilizimika?
 
Mpaka nahoji hivyo mkuu binafsi roho inaniuma sana, Natamani kutazama mpira wenye ladha kama kwenye Ligi za mbele, Pitch safi, uwanja wa kisasa, TV, LED Display zinavutia nk. Siku nilipotazama mchezo wa Azam na APR pale Amahoro nilivuyiwa sana na ule uwanja, Niliposikia Uwanja wa Mkapa unafanyiwa maboresho tena kwa zaidi ya B31 nilifurahi nikajua kwa pesa hiyo. Uwanja wa Mkapa unaenda kuwa Old Trafford ya Tanzania. Mbaya zaidi baadhi ya michezo ya muhimu ya CAFCL 2023 ilihamishiwa viwanja vingine, Hiyo iliniuma ila nikajua soon mambo yatakuwa mazuri sana. Huenda niliweka matarajio makubwa kuliko uhalisia 😀 hicho ndicho kinanitafuta, Anyways labda napaswa kupunguza Expectations na kukubaliana na uhalisia!
Umesahau hii nchi ni ruksa kufanya kwa vitendo neno "kula urefu wa kamba yako"
 
mara ya mwisho ilikuwa kwenye mechi na timu ya tunisia ambayo viti vilirushwa nuilikaa vip B viti vimechakaa kwa kifupi huu ni upigaji mwingine
 
View attachment 3249165
Jamaa wewe una ajenda binafsi na huu uwanja,hizi zote ni nyuzi zako na zote.umerudia rudia content na kuitaja Amahoro stadium kama mfano katika kila uzi.Kwa taarifa yako uwanja bado upo kwenye marekebisho mpaka so tulia kijana
Kuhoji ni dhambi?

Alichoandika sio kweli?

Ww umeona mabadiliko yepi kwenye huo uwanja?
 
Kuhoji ni dhambi?

Alichoandika sio kweli?

Ww umeona mabadiliko yepi kwenye huo uwanja?
ina maana hujui kwamba bado kuna marekebisho kwenye uwanja wataifa yanaendelea?!na hii ndio sababu hadi leo mechi a simba na yanga zinachezewa KMC na Chamazi,hujaona hata kuna sehemu mechi ya juzi Smba na Azam viti viling'olewa na vinatakiwa viwekwe vipya ambavyo mzigo wake upo bandarini'.?
 
Back
Top Bottom