Mpaka nahoji hivyo mkuu binafsi roho inaniuma sana, Natamani kutazama mpira wenye ladha kama kwenye Ligi za mbele, Pitch safi, uwanja wa kisasa, TV, LED Display zinavutia nk. Siku nilipotazama mchezo wa Azam na APR pale Amahoro nilivuyiwa sana na ule uwanja, Niliposikia Uwanja wa Mkapa unafanyiwa maboresho tena kwa zaidi ya B31 nilifurahi nikajua kwa pesa hiyo. Uwanja wa Mkapa unaenda kuwa Old Trafford ya Tanzania. Mbaya zaidi baadhi ya michezo ya muhimu ya CAFCL 2023 ilihamishiwa viwanja vingine, Hiyo iliniuma ila nikajua soon mambo yatakuwa mazuri sana. Huenda niliweka matarajio makubwa kuliko uhalisia 😀 hicho ndicho kinanitafuta, Anyways labda napaswa kupunguza Expectations na kukubaliana na uhalisia!