Zamazamani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2008
- 1,869
- 787
Wanajamvi,
Nipo hapa kutaka kujua nakosea wapi.
Mpaka sasa ndani ya miezi sita nimeibiwa /poteza simu tatu- smart phones. Simu ya kwanza nikairipoti polisi, Central Police, Dodoma kwa taratibu za kawaida za kipolisi pale Cyber Crime Unit lakini nikawa sina IMEI number hivyo nikaambiwa ndiyo sababu ya kuwa ngumu kuipata, ikapotea.
Simu ya pili ikaibiwa Dar es Salaam, nikaripoti polisi Oysterbay. Pamoja na kuwapa IMEI number, na kuahidi kwamba nipo tayari kuongeza 'nguvu'- lakini nayo nikaishia kuzungushwa - ikapotea.
Simu ya tatu mwezi January mwanzoni ikiaibiwa Dar es Salaam, nikafuata taratibu za kipolisi - Cyber Crime Unit - nimefuatilia wee mpaka sasa nimekaribia kukata tamaa, naambulia stori na kuzungushwa tu, nayo pia inaelekea itapotea.
Sasa najiuliza: Nakosea wapi wakuu? Kama kutoa cha mboga ili kutia nguvu mbona siyo kesi na sijabisha wakuu? Najiuliza kwanini inakuwa ishu kubwa kupata huduma hii wakati ndiyo kazi yao kitaalam?
Naomba ushauri nini cha kufanya au wapi pa kwenda sababu simu zinaibiwa kila siku na hasara yake siyo ya kitoto, vinginevyo nikomae na vitochi tu.
PS. Najua kuna njia za ku-block isitumike au kui-trace simu ilipo pia ikawa mbinde -- njia pekee iliyoonekana itafaa ilikuwa ni kutumia chombo cha dola, lakini mpaka sasa bila bila.