Kuna yeyote aliyewahi kufanikiwa kupata simu yake iliyoibiwa kupitia Cyber Crime Unit?

Kuna yeyote aliyewahi kufanikiwa kupata simu yake iliyoibiwa kupitia Cyber Crime Unit?

Mkuu ulijaribu kwenda TCRA? Labda wangekupa mwangaza na pia ungejaribu kwenda pale sayansi kwa madogo wa UD-CICT (University Of Daressalaam College Of Information and Communication Technology) wangeweza kukushauri utumie manoeuvre gani maana hayo ndio mambo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
TCRA hawana Msaada wote kwenye Wizi wa Simu. Watakuambia nenda Kwa Mobile Operator wakusaidie. Kuna Siku niliibiwa simu nikaenda hapo nikapata Hilo Jibu. Cybercrime watakuzungusha oh nenda huko uliokoripoti Wizi wakusaidie Sisi hatupokei mtu binafsi hapa. Siyo Rahisi hata kidogo kupata simu iliyoibiwa via cyber. Ndio maana Wezi wa Simu hawaishi.
 
Zamazamani, Kama wewe sio POLISI hiyo Cyber Crime Act haikusaidii hata nilishaibiwa sana tu na kuripoti ila unawasaidia POLISI kupiga hela na cm yako sijui C - law haoni hii au na yenyewe tupeleka kwa mkulu ndio hapo naona umuhimu wa IGP kua Brigadier General watanyooka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini uibiwe zote hizo kwa nyakayi tofauti tofauti, tuanzie hapa kwanza
 
TCRA hawana Msaada wote kwenye Wizi wa Simu. Watakuambia nenda Kwa Mobile Operator wakusaidie. Kuna Siku niliibiwa simu nikaenda hapo nikapata Hilo Jibu. Cybercrime watakuzungusha oh nenda huko uliokoripoti Wizi wakusaidie Sisi hatupokei mtu binafsi hapa. Siyo Rahisi hata kidogo kupata simu iliyoibiwa via cyber. Ndio maana Wezi wa Simu hawaishi.
sio kweli
 
Wapo mimi ambao nilishuhudia kabisa walipata simu zao na wapo wengine niliwashuhudia pia hawakupata kwahiyo hiyo kitu ni 50-50 unaweza pata na ukakosa vile vile maana inategemea na mtu ambaye alieiiba akiwa mjanja huwezi ipata.
 
Mkuu nafahamu hasira ya kuibiwa sm. Niliibiwa simu mpya baada ya kutolewa kisu nje ya club na vibaka wakiwa na boda. Nilikasirika sana na kuwa tayari kufanya lolote kupata simu yangu.

Baada ya kuandika taarifa polisi na kupewa mpelelezi, akanishauri kupeleka Cyper Crime. Mpelelezi akahitaji hela nikampa. Makubaliano yalikuwa sm ikipatikana mtuhumiwa abanwe anilipe fidia ya kiasi cha hela nilichompa polisi. Nikamuunganisha polisi whatsaspp nikawa nacheki nae karibu kila siku. Tukawa kama marafiki hivi.

Baada ya muda akaniambia wale wezi walikuwa wanajulikana kwa kukaba watu wa club. Kwa hiyo polisi waliwawinda wakawaua, ila simu yangu haikupatikana!!! Nilipopeleleza nikaambiwa ni kweli siku za karibuni kuna vibaka waliuawa.

Nilipochimba zaidi nikaambiwa hiyo ni mbinu ya polisi ukiwa na kesi ya kufuatilia simu wakishakula hela wanakwambia watuhumiwa wameuawa!!! Wakati mwingine simu wanafanikiwa kuipata ila wanaichukua wao au kuchukua hela toka kwa mwizi.

Tatizo liko wapi?

Kwa kufuatilia ile simu polisi hao hao waliniambia changamoto walizo nazo kuhusu kufuatilia simu. Ni kwamba uwezo wa kitengo chao cha Cyber Crime ni mdogo kulinganisha na mahitaji. Hata baadhi ya mikoa wanategemea msaada wa Cyber Crime makao makuu Dar. Kwa hiyo wanaweka umuhimu kwenye kufuatilia mambo ya jinai. Mfano, kama mtu kaua wanaweka umuhimu kufuatilia movement ya simu yake ili kumkamata. Mfano mwingine wa umuhimu kwa polisi ni ambapo sm imeibiwa na jinai kubwa kutendeka wakati hiyo sm ikiibiwa, labda mtu kabakwa na kuibiwa sm.

Vile vile wanasema kuna tabia ya watu kutumia vibaya hiyo huduma. Wengine wako tayari kutoa hela kufuatilia nyendo za wenza wao kwa ajili ya wivu nk. Tatizo ni kwamba polisi hawakuelezi hizi changamoto zao wakati ukiomba huduma. Wao wanapiga hela wanaachana na wewe!!! Mpelelezi hakupi namba ya mtu wa Cyber Crime uwasiliane nae moja kwa moja. Mpaka sasa sijui hela yangu alikula mpelelezi wangu peke yake au aligawana na mtu wa Cyber Crime

Ushauri

Fuatilia sm kama kuna polisi unamfahamu binafsi na huyo polisi ana mtu anamfahamu binafsi kwenye kitengo cha Cyber Crime. Ikiwa hivi inaweza hata kuchukua miezi sita ila sm yako utaipata. Hata kama unamjua polisi binafsi kama hana anaemjua binafsi kwenye Cyber Crime tegemea miyeyusho. Ila kumbuka, kuipata sm ni lazima alieiiba aiwashe (iwe on). Kama hajaiwasha haiwezi kupatikana!!
 
Cyber Crime uwezo wa kutrack na kuipata simu iliyoibiwa wanao na wameshakamata simu nyingi tu! my sister mwaka jana pale Ostabay aliweza saidiwa na akapata simu zake 2 zilizoibiwa! Tatizo mpaka wawe motivated[emoji16]

Aliwa motivate kwa quumer,thats clear!
 
Kupeleka kesi yeyote polisi ni kumpa polisi deal....wao wanaangalia maslai yao tu,simu ya laki mbili unaambiwa utoe laki kama gharama za kutrack hiyo inakujaje? Na hapo kuna kupata na kukosa bora uipotezee tu...na mwizi kama hamjanja hawampati hata wafanyaje coz hiyo kama yao sasa ya mwaka sabini na saba...
 
2016 niliibiwa simu yangu dodoma uhindini (iPhone 6s+) karibia na car wash mida ya saa2 usiku, within a two days nikaipata na cover lake tatizo system charge tu ndio walikua wameiharibu

Niliipata msalato mbele kabisa ndani ndani kuna sehem wanauza matofali ndio huko waliko kuwepo, na bahati nzuri ile tunafika tumewakuta nayo simu red handed kabisa wenyewe wamekaa nje wanapiga story[emoji16][emoji16] kwa msaada wa central police (nililipia kiasi) na Internet cafe kuna mkaka mtundu wa simu (nako nililipia)

Ilikua wanazima na kuwasha huku icloud inasoma, police wakafatilia kupitia imei jioni nikapigiwa simu niende na hela ya tax twende hiyo sehem (walichezea makofi hadi nikawaonea huruma) na simu yenyewe nikaiuza wiki hiyohiyo
Taratibu Mkuu, Bongo kuna kifaa cha Trace IMEI ya mtu mpaka wampate au walitumia icloud kuikamata hiyo simu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi niliibiwa tableti nikaripot polisi mwezi wa tano, wakaanza kuitrec kwa soft wear zao ....but kila nikoenda naambiwa niwatafuti e ya usafiri wakamkamate mwalifu

Mualifu kakakamatwa na aliyemuuzia ...!! Iliwashinda kuiflash wakaibadilishia IMEI NUMBER

TCRA na wao wakaingilia kati wanamtaka fundi wa cm aliyefanya mchezo huo

Nilijisomba mahakamani nikaona usenge tu bora nikubali tu nijichange nikanunua nyingine

Cyber unit hawasaidiii kbs miyeyusho ming mpk uwatangazie dau kubwa

sent from toyota Allex
Mkuu unataka unambie hata ukibadili IMEI number bado wana uwezo wa kuitrace?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ulijaribu kwenda TCRA? Labda wangekupa mwangaza na pia ungejaribu kwenda pale sayansi kwa madogo wa UD-CICT (University Of Daressalaam College Of Information and Communication Technology) wangeweza kukushauri utumie manoeuvre gani maana hayo ndio mambo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah ulipoandika "madogo wa ud" nikaishia kuipuuza post yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo watu hawako stationary,Wana move arround,hata mnara ukurekodi uko area,lakini haiwezi kupinpoint hasa ulipo tuseme Hadi mita 10,inabidi wawepo watu wa kufanya legwork kukuotea,
Sasa tuseme uko nagurukuru,wanaokufuatilia wako dsm,halafu huko nangurukuru sio ulikojiandikishia nida Hapo inakuaje Kama sio itahitajika human resource kukutrace?
Na hiki ndicho hata mimi nakifahamu, wanaweza wakajua unaishi Mbagala Kibonde maji ila kujua kabisa nyumba ama sehemu ulipo ni mtihani.

Mfano mtu unatumia voda, mnara wa karibu yako ni wa tigo, tena upo karibu kwa takribani 1km.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi kati nimekwapuliwa simu yangu na vijana wa bodaboda. Nilitaka kwenye cyber crime unit lakini kwa shuhuda hizi ngoja nipige kimya. Sitaki harasa mara 2.
Nimejipanga kwenda kurevenji kwa wale wezi. Nitakwenda eneo lile lile na wana wa kitaa kama 10 hivi then nitakaa kihasara hasara huku nikichekezea simu. Akijipendekeza mtu tutahitimisha safari yake hapa duniani.
Huu sasa ndo uanaume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom