Soma hili gazeti labda utapata akili kuhusu hao wajanja
Nabii yeypte anaegawa maji ni hatari.
Manabii wote pia wanachumba maalum zile pesa unazotoa sadaka anaenda kuziwakilisha pale kwa mungu wake,kabla ya kupeleka benki, bada ya hapo inakuwa ngumu kwa mtu kukimbia unakuwa huambiliki.
Halafu wanakukaribisha kwa kutaka kukujua jina na namba za simu. Baadae watajua nani ana hela nani hamna kitu. Utashangaa utaona wale wenye mihela ndio wanatabiriwa sana. Baadae wanaitwa kwenye ofisi yake kwa kupewa maombi maalum hapo ndipo mpunga utatoa mwenyewe.
Kifupi wote wenye maji na mafuta na sijui cake wana vitu wamepewa na waganga wa kienyeji hasa conngo, mozambiq na Nigeria, Malawi n.k
Wanachimbia kitu kwenye jengo na pia ana kimungu chake kitunguri huko kwake kabla hajaingia job anasemea pale anataka nini kitokee kanisani.
Waongo wakubwa wote unaowaona hata hapa dsm.
Mchongo mzima aliutoa Nabii mmoja kula South Africa, aliacha hayo mambo baada ya mtu mmoja kutaka kumuuziza mkono wa mtu ili aongeze nguvu ya mvuto kwenye kujaza watu. Huyu zamani alikuwa mchungaji wa kawaida ila alishangaa pamoja na kufunga na kuomba aliona hela hapati na miujiza kanisani hamna ndipo alipowaendea manabii kuwauliza siri ni nini.
Kifupi yule aliyekuwa anauza ule mkono aliikamatwa na polisi na wote aliotaka kuwauzia walikamatwa.
Yeye polisi walimkamata ofisini kwake na watu kibao walikuwa wamepanga foleni nje wanasubiri wamwone awaombee ndipo wakamwona anatoka ma pingu.
Kule jela ndipi akili zilimrudia kwamba amepotea na amejiingiza kwenye kitu sio sabsbu yeye alikuwa ni mchungaji na mtoto wa mchungaji na pia alisomea bible school.
Alienda kwenye TV huko kwao kutubu wenye TV wengi walimkatalia sababu walisema manabii wanachangia pesa ndefu atavuruga biashara. Lakini TV nyingine aliongea na kuchapa vitabu.
Pia aliongea kwamba kila Nabii ana Jina lake halisi na aka. Jina la aka wanalichagua kwa mganga huko.
Achana na hao watu, ukila vitu vyao kuchomoa ni ngumu. Hata nabii wao wamkute na condom na chupi ya mwanamke bado watu watamtetea