Ustishe watu hapa mafuta kununua si lazma aende na ya kwake yaombewe hayo atumie achen kupotosha watu bhana. Hata mi nikiwa na huduma naweza weka mafuta niliyoyaombea mtu akitaka kwa lengo la kuchangia huduma isonge mbele ananunua si lazma
Huduma gani hiyo ya kuombea mafuta na kuyauza kwa wahitaji? Yaani Mungu akupe kipawa au talanta halafu wewe ukawa charge watu pesa kupata huduma ya Mungu kwa kuibatiza jina kuwa "kuchangia huduma"
Kama kweli hayo mafuta yana nguvu za Mungu watu wapewe bure...usiuze hata senti 5. Au waambiwe waje na mafuta yao yaombewe...otherwise mwenye huduma anakuwa anaigeuza kazi ya Mungu kuwa biashara.
Mathayo 10
8Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepewa bure, toeni bure.
Mwenye injili (Yesu) alishatoa maagizo kuwa huduma yake ni bure..haiuzwi.
Matendo 8
18 Hapo Simoni alingamua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
19 “Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyote nitakayemwekea mikono, apokee Roho Mtakatifu.”
20 Lakini Petro akamjibu, “Potelea mbali na fedha zako kwa vile unafikiri kwamba unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!
Ukisoma fungu la 20 hapo unapata dhima ile ile ya kuwa huduma ya Mungu haiuzwi at any cost..ni ya bure kwa yeyote anayeihitaji.
Lastly unaona hata Elisha alikataa kupewa zawadi toka kwa Naamani kwa huduma ya uponyaji wa ukoma. Maana angepokea ingekuwa kana kwamba Naamani amenunua uponyaji ule. Ila anakataa kupokea ili sifa ziende kwa Mungu.
Ukisikia kuna mtumishi wa Mungu yeyote anawauzia watu huduma ya Mungu hata kwa senti...huyo hajatumwa na Mungu...ni mbwa mwitu ndani ya vazi la kondoo.