Kunahitajika kauli moja ya Watanzania kuhusu matukio ya utekaji na kuumizwa

Kunahitajika kauli moja ya Watanzania kuhusu matukio ya utekaji na kuumizwa

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
8,406
Reaction score
9,619
Wakuu amani ya Bwana ikawe juu yenu na Mungu amebariki.

Tanzania bila utekaji na kuumizwa inawezekana .

Ipo vedio hivi ya kijana ambae inaonekana anajulikana kwa jina SATIVA ,simfahamu ila yupo na dam kama sie,

Alitekwa 23/6/ 2024 kwa mjibu wa taalifa za hapa na pale pitia mitandao ya kijamii , na imesemakana amekutwa katupwa hifadhini katavi na clip yake inatembea mitandaoni mpaka mda huu ,nani yupo nyuma ya jaribio hili lakutoa uhai wa ndugu mtajwa hapo juu hatujajua.

Kama nchi ikiwa tumeamua ishi kwa utaratibu huu wa kutekana ,kuumizana hakuna alie salama maana mtekaji anaweza tekwa pia na kuchomwa moto pia,

Kwa andiko hili najua jf imejaa watu makini sana.

Naomba kama sehem ya watz tulio jf kuja na hoja au tamko la pamoja nini kifanyike juu ya upuuzi huu ,wa kishamba na ujinga .

Karibuni wakuu

PIA SOMA
- SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Osterybay kabla ya kusafirishwa sehemu zingine na nimepigwa risasi ya kichwa

- Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana
 
Unakubalika sana Komredi
1000024318.jpg
 
Acheni kutukana serikali na viongozi, unaweza kujenga hoja bila matusi,kedi,dharau,dhihaka,ukitaka kuonekana mwamba,watakutatua tu marinda
Serikali inachotufanyia wananchi huoni kama ni zaid ya matusi?

Haitengenezi ajira inahimiza vijana tujiajiri huku ikijua aina ya elimu tuipatayo vijana ipo irrelevant.

Nchi ina raslimali kila pande lakin serikali haina akili ya kutumia raslimali hizo ktk kuendeleza nchi na wananchi wake

Inakopa na haioneshi wazi namna gani mikopo ile inafanya kazi ili kuwaondolea wananchi wake kadhia ya maisha ya kuunga

Mawaziri na wabadhirifu wa mali za umma inawalinda kwa nguvu zote paspo kutambua wale wapo pale sababu sisi wananzengo tumewachagua

Na ndo unahimiza tukipigwa shavu la kulia tugeuze na la kushoto?

Pumbavu zako...
 
Serikali inachotufanyia wananchi huoni kama ni zaid ya matusi?

Haitengenezi ajira inahimiza vijana tujiajiri huku ikijua aina ya elimu tuipatayo vijana ipo irrelevant.

NchibiIna raslimali kila pande lakin serikali haina akili ya kutumia raslimali hizo ktk kuendeleza nchi na wananchi wake

Inakopa na haioneshi wazi namna gani mikopo ile inafanya kazi ili kuwaondolea wananchi wake kadhia ya maisha ya kuunga

Mawaziri na wabadhirifu wa mali za umma inawalinda kwa nguvu zote paspo kutambua wale wapo pale sababu sisi wananzengo tumewachagua

Na ndo unahimiza tukipigwa shavu la kulia tugeuze na la kushoto?

Pumbavu zako...
Hapa umenadi tu ujinga wako,na Kama ulienda shule ni heri hiyo pesa ya ada ungefunguliwa genge la nyanya
 
Wakuu amani ya Bwana ikawe juu yenu na Mungu amebariki.

Tanzania bila utekaji na kuumizwa inawezekana .

Ipo vedio hivi ya kijana ambae inaonekana anajulikana kwa jina SATIVA ,simfahamu ila yupo na dam kama sie,

Alitekwa 23/6/ 2024 kwa mjibu wa taalifa za hapa na pale pitia mitandao ya kijamii , na imesemakana amekutwa katupwa hifadhini katavi na clip yake inatembea mitandaoni mpaka mda huu ,nani yupo nyuma ya jaribio hili lakutoa uhai wa ndugu mtajwa hapo juu hatujajua.

Kama nchi ikiwa tumeamua ishi kwa utaratibu huu wa kutekana ,kuumizana hakuna alie salama maana mtekaji anaweza tekwa pia na kuchomwa moto pia,

Kwa andiko hili najua jf imejaa watu makini sana.

Naomba kama sehem ya watz tulio jf kuja na hoja au tamko la pamoja nini kifanyike juu ya upuuzi huu ,wa kishamba na ujinga .

Karibuni wakuu

PIA SOMA
- SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Osterybay kabla ya kusafirishwa sehemu zingine na nimepigwa risasi ya kichwa
DAAH NDUGU YANGU CCM WAMEWEKA PAMBA MASIKIONI NA KUVAA MIWANI YA MBAO, HIVYO HAWAONI WALA KUSIKIA WANAJUA KINACHOENDELEA
 
Acheni kutukana serikali na viongozi, unaweza kujenga hoja bila matusi,kedi,dharau,dhihaka,ukitaka kuonekana mwamba,watakutatua tu marinda
Kutumia "Lugha ya Staha" au siyo?
Ulaghai huo ukigundulika ni hadaa, wanaohimiza ujinga huo wanakuwa vichaa?

Usisahau "kutatua marinda" haitokei upande mmoja tu! Hayo ya kwenu baada ya kuyatatua, wanatupiwa fisi na wao waji-injoyi!
Usijifanye huelewi.
 
Hili jambo lina tatizo sana hasa kwa upande wa Serikali. Watetezi wanazidi kuharibu kabisa afadhali wakae kimya

1. Wanaosema ni mapenzi imethibitika kutoka kinywani kwake alipelekwa Oysterbay kituo cha Polisi
2. Haiwezekani mtu wa kawaida ampeleke njia zote hizo kwasababu ya mapenzi !
3. Kama ana matusi au mapenzi, mtuhumiwa anafikishwa Polisi si Porini halafu anafunguliwa mashtaka
4. Ndugu walikwenda Polisi na kuambiwa hayupo, leo inajulikani alikuwepo. Polisi walificha nini? na kwanini
5. RPC wa katavi alisema '' wanaanzisha uchunguzi'' sasa mtuhumiwa kasema alikuwa Oystebay Police
6. Kituo cha Polisi Oyesterbay hawajakanusha kauli ya Sativa

Jambo hili linakwenda sehemu hii
1. IGP ajitokeze kueleza nini kilitokea katika Jeshi la Polisi na kwanini
2. Waziri wa mambo ya ndani ajitokeze aeleze jambo hili

IGP na Waziri wa mambo ya ndani wanaweza kukaa kimya na kudharau, kitu kimoja hakikwepeki tayari kuna kujichanganya katika Jeshi la Polisi kuanzia kukataa mtuhumiwa alipo, kituo cha Polisi kuhusishwa na majeruhi kuwa hai. Viongozi hawa wawili wanapaswa kujitathmini kwasababu tatizo linazidi kupanda ngazi!

Tindo JokaKuu Pascal Mayalla Maxence Melo
 
Dikteta chura ameamua kutumia jeshi kuteka watu.tumekabidhi madaraka jitu shamba kabisa.linashindwa kujibu hoja linakimbilia kuteka?watz tuamke tukamfurushe chura pangoni kama wanavyofanya wakenya.
 
Back
Top Bottom