Hili jambo lina tatizo sana hasa kwa upande wa Serikali. Watetezi wanazidi kuharibu kabisa afadhali wakae kimya
1. Wanaosema ni mapenzi imethibitika kutoka kinywani kwake alipelekwa Oysterbay kituo cha Polisi
2. Haiwezekani mtu wa kawaida ampeleke njia zote hizo kwasababu ya mapenzi !
3. Kama ana matusi au mapenzi, mtuhumiwa anafikishwa Polisi si Porini halafu anafunguliwa mashtaka
4. Ndugu walikwenda Polisi na kuambiwa hayupo, leo inajulikani alikuwepo. Polisi walificha nini? na kwanini
5. RPC wa katavi alisema '' wanaanzisha uchunguzi'' sasa mtuhumiwa kasema alikuwa Oystebay Police
6. Kituo cha Polisi Oyesterbay hawajakanusha kauli ya Sativa
Jambo hili linakwenda sehemu hii
1. IGP ajitokeze kueleza nini kilitokea katika Jeshi la Polisi na kwanini
2. Waziri wa mambo ya ndani ajitokeze aeleze jambo hili
IGP na Waziri wa mambo ya ndani wanaweza kukaa kimya na kudharau, kitu kimoja hakikwepeki tayari kuna kujichanganya katika Jeshi la Polisi kuanzia kukataa mtuhumiwa alipo, kituo cha Polisi kuhusishwa na majeruhi kuwa hai. Viongozi hawa wawili wanapaswa kujitathmini kwasababu tatizo linazidi kupanda ngazi!
Tindo JokaKuu Pascal Mayalla Maxence Melo