Kunahitajika kauli moja ya Watanzania kuhusu matukio ya utekaji na kuumizwa

Mimi nilipoona yule jambazi Daudi Albert Bashite anarudishwa kazini na muda si mrefu haya matukio kuanza Wala sikupata shida kujua nani ni mastermind wa huu ufedhuli.
 
Jeshi la polisi limeshazoea kutekateka. Hili jambo litaleta aibu kubwa sana kwa siku za baadae
 
Mie natamani kujua kwanini alitolewa Osterbay police station na kupelekwa Arusha, huko Arusha kwa nani na kwanini huko?
Daudi Albert Bashite ni wazi amerudi kuendelezea pale alipoishia.
 
Code imefunguka hata mimi nimeelewa sasa.
 
Hakika huu utekaji si afya kwa Mama wanamharibia kiaina. Watu wenye makosa kwanini hawapelekwi kwenye vyombo vya sheria?
 
Ili kuondokana na matukio haya ya kishetani, tujiulize ni kwa nini zamani hayakuwepo. Matukio haya yalianza wakati wa utawala wa Kikwete kwa kiasi kidogo, yakashamiri wakati wa utawala wa Magufuli, na yamekuwa mengi kupindukia wakati huu wa utawala wa Samia.

Hii ni dhahiri kuwa matukio haya yana uhusiano na aina ya watawala tunaokuwa nao.

Cha kufanya, ni wananchi tutoe tamko kuwa kama haya mambo hayakomi, bila ya kujali namna yoyote ile, mtawala wa sasa na chama chake, kamwe wasiungwe mkono katika jambo lolote lile, maana wametuthibitishia pasipo shaka kuwa hawana uwezo wa kuyalinda maisha ya Mtanzania. Uhai wa mwanadamu hauna mbadala. Aheri madaraka na uongozi wa nchi apewe mtu yeyote na chama chochote, alimradi chama hicho na kiongozi huyo, awe na uwezo wa kuwahakikishia wananchi usalama.
 
Acheni kutukana serikali na viongozi, unaweza kujenga hoja bila matusi,kedi,dharau,dhihaka,ukitaka kuonekana mwamba,watakutatua tu marinda
Wewe utakuwa ni miongoni mwa hao mashetani.

Mtu kama amefanya jinai kwa nini asikamatwe na kushtakiwa? Hao viongozi wanafanya makosa mara ngapi? Kama ingekuwa kila anayefanya kosa anauawa, Tanzania unaamini tungekuwa bado tuna viongozi?

Mtu yeyote anayeshanikia huu ushenzi wa utekaji, ni shetani asiyestahili kuishi pamoja na wanadamu.
 
Chadema si iliwaiteni pale muongee kutukana mamlak?
 
Hakika huu utekaji si afya kwa Mama wanamharibia kiaina. Watu wenye makosa kwanini hawapelekwi kwenye vyombo vya sheria?
Hiyo inaitwa sheria mkononi swali fikirishi je hizo sheria za mkononi jamii ikiamua na yenyewe kuziishi, (asmillate), nadhani itakuwa mwaga ugali vs mwaga mboga hapa tunaongea kama utani lakini ndiyo huko tunaelekea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…