Kundi kubwa la wanaodai Katiba Mpya hawajui wanachokitafuta na hawana kazi ya kufanya

Kundi kubwa la wanaodai Katiba Mpya hawajui wanachokitafuta na hawana kazi ya kufanya

Terrible Teen

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2017
Posts
1,009
Reaction score
2,934
Unafiki wa Watanzania umeendelea kudhihirika baada ya kifo cha JPM na kuingia madarakani kwa Mhe. RAIS. SSH. JPM alitumia udikteta kunyamazisha kila sauti na hakuna aliyedai Katiba mpya wala nini. Aidha, kwa udikteta huohuo aliharibu uchumi na haki za kiraia bila ya kuulizwa.

Leo ameingia Rais Samia amefanya kazi kubwa kuondoa uonevu na udikteta wa Hayati Magufuli, kabla hajamaliza kuweka mambo sawa kumeibuka viruka na njia vilivyokuwa vimefunga midomo kwa JPM na kuanza chokochoko sijui katiba mpya na nini.

Hawa watu hawana ajenda na hawajui wanataka nini. Katiba mpya haitafutwi kwa mayowe na movements za kishamba za felaini na macho kumchuzi.

Muacheni Mhe. RAIS atekeleze ajenda zake za kuleta pesa kwa watanzania , kuinua haki za kiraia na utengamano. Masuala ya Katiba ni yanyie wanasiasa msio na kazi. Mmekosa ajenda and you are irrelevant kwa watanzania muda huu. Mliufyata kwa JPM leo mmeona mwanamke msikivu ndio mnatoa pembe, shauri yenu akianza kuwabutua.
 
Umemsikia Anthony Diallo leo, kiongozi wetu wa CCM, ??

Inawezekana na wewe una file lako mirembe siyo bure! Huwezi ongea upup.u wote huu!!
 
Diallo mwenyewe atakuwa ametoroka mirembe kuja kwenye kipindi.
 
Haki za binadamu sio hisani ambayo mtawala anawapa raia wake kama dikteta Magufuli alivyowaaminisheni bali ni haki yao ya kikatiba isiyo na mjadala.

Mimi nawashangaa sana wale wanaomuomba rais katiba mpya sijui rais anahusikaje na katiba mpya wakati na yeye ni mpita njia tu.

Katiba sio mali ya rais bali ni kielelezo cha namna wananchi wanavyotaka waongozwe na viongozi wanaowachagua kwa kura zao.

Sasa wasioelewa wanachukulia katiba kama waraka maalumu wa rais, hii ni dhana potofu sana na kwa fikra hizi hiyo katiba mpya hatuwezi kamwe kuipata kwani mpaka impendezee huyo rais ndio aridhie mabadiliko.
 
Yeyote aliyeko madarakani ameapa kuilinda na kutetea katiba, kama unasema katiba sio kipaumbele tujiulize tunaongozwa na nini
 
Back
Top Bottom