tutambue kuwa kama hakuna mahakama iliyo huru basi hata kama katiba itatupa haki yawezekana haki hiyo tusiipate, kama hakuna bunge lenye nguvu na lenye wabunge wanaojua majukumu yao, wanaotekeleza majukumu yao kusimamia serikali haitakuwa rahisi kuisimamia serikali ili ituretee maendeleo,
moja ya mambo ambao yanaleta vurugu nyingi katika nchi ni nafasi za uteuzi anazopewa raisi kuwateua watendaji mbalimbali na hapa wengi hijukusanya kutengeneza makundi kwenda kutafuta nafasi hizi. ni kuhatarisha amani ya nchi kwa kuweka nafasi nyingi katika uteuzi wa raisi. lakini pia ni kuleta uzembe na ujanja kwani wapo wananchi wengi wanakaa kutafuta fitina, vijembe na kujuana katika kutafuta nafasi hizi huku wakiwa wababaishaji watupu wasioweza kufanya lolote. kundi lao likishapata uraisi huwa ni vigumu kuwaepuka watu hawa kwani wanazombinu hata za kuwatumia wananchi kugeka watu wanaowatumikia kwa kujenga fitina.
kuepuka haya ni kuweka nafasi chache za juu pengine za nafasi ya uwaziri peke yake kuwa ndiyo zinateuliwa na raisi na nyingine zitafutwe kiushindani.
lakini tusiwawekee watu hawa mifumo ya kuwalinda kama hawafanyi kazi.
bunge liwe huru ili lisimamie,
vipo vyombo havifanyi kazi kwa mifumo tuliyokuwa nayo huko nyuma.
leo hii vipo vyombo vya kushughulikia maadili ya umma havifanyi kazi mpaka viagizwe, kwa nini tusivipe uhuru viondokane na kujikuta vikitaka kuchunguza mara refa wa mtu fulani ndiye anachunguzwa hivyo wanafungwa mikono.
mashirika ya umma yanakufa tatizo ni mifumo ambayo haisimamiani na kuwajibishana.
haiwezekani ATC imekufa, hakuna aliyewajibishwa, mifumo inarejesha lawama kwa raisi maana yeye anateua watu watatu katika mashirika na kila mmoja anajiona mteule wa raisi. bodi za makampuni ni mabosi wa wakurugenzi watendaji lakini hawa wanachukua posho tu na wengine wanakoromewa na wakurugenzi.
hivi ni nani anayetaka mashirika yetu kufa, najua wapo wenye biashara zao lakini ni wachache na kwa kuweka mifumo mibovu taifa linadidimia kiuchumi hivyo hata wao biashara zao haziwezi kukua.
tukibadilisha mifumo taifa linaweza kwenda mbele lakini wengine akili zimeganda wanafikiria hatari tu hawaangalii faida na bila kuwa risk taker hatuwezi kupuga hatua.
Huyo EGO ana matatizo afu nahisi huyu jamaa sio Mtanzania maana hajui kuwa uhalali wa Katiba unatokana na wananchi naona hajasoma sehemu inayoeleza Mamlaka ya Wananchi kwenye Ibara ya 7 kwenye katiba pendekezwa inayoweka wazi kuwa Nchi yoyote inayoamini katika demokrasia na utawala wa kisheria ni sharti itambue mamlaka ya wananchi wake. Katiba Inayopendekezwa inazingatia ukweli kwamba wananchi ndiyo msingi na chimbuko la mamlaka yote ya uendeshaji na utawala wa nchi, sasa unapoendelea kubisha hata sikuelewi kapige kura ya ndio uone hiyo haki kama hutatendewa!