kwa kutambua kuwa serikali ni kampuni na mwananchi ndiye mmiliki itamfanya mwananchi yeyote kujitambua yeye na kuitambua serikali kuwa ni watumishi waliojiriwa na wananchi kuwatumikia.
utatambua kuwa hakuna kampuni ambayo mkurugenzi anamnyima mmiliki taarifa au anakaidi maagizo ya mmiliki akabaki salama labda anataka kufukuzwa kazi.
lakini katika nchi za wajinga serikali inawanyima wananchi wake taarifa na kudai mambo mbalimbali ni siri za serikali????? yaani nimekuajiri unifanyie kazi katika duka langu ninakuomba taarifa za duka unaniambia eti ni siri za duka?????
kutokuelewa huku ndiko kunakotufanya tunadhani raisi anatakiwa kuteua anavyotaka badala ya kutambua kuwa hakuna mtu anamuajiri mkurugenzi mkuu katika kampuni eti anamuacha mkurugenzi mkuu katika kampuni kila sehemu ateue anavyotaka.
wewe ukiwa mmiliki unaouwezo wa kuamua hivyo kwa maana ukiamua kampuni yako watumishi watumishi wake wawe watoto wako, ndugu zako na marafiki zako hakuna wa kukuuliza.
lakini hakuna mtendaji wa kuajiriwa au kuteliwa au kuchagukliwa anaweza kujiamlia kuweka ndugu zake, mrafiki zake, washirika zake.
hapa namaanisha wananchi wanaweza kuamua katika makampuni yetu hatuajiari watumishi wageni kwa maana ya watumishi kutoka nje ya nchi lakini raisi hawezi kusema mimi nitaajiri marafiki zangu tu katika utumishi wa umma ingawa hilo linaweza kutokea pale tu wananchi wanapokuwa wapumbavu na kutokujitambua wao ni nani kwa serikali na nini haki zao na wakaruhusu kutunga katiba yenye mianya kama hiyo.
lakini mimi napenda kuwaonyesha kinachokuja kwa nchi za wapumbavu wenye kuruhusu mambo kama hayo ni nini?
ni nchi hizo kurudi katika utumwa wa aina nyingine !
kama tulivyoona baadhi ya nchi kama misri na libya na nyingine nyingi viongozi wajiweka kuwa watawala wa milele na baadhi wakitafuta kuwarithisha watoto wao uongozi lakini kwa utumwa huu unaokuja hautatoka kwa watawala bali utatoka kwa matajiri kuchukua kila kitu cha masikini kupitia rushwa and any kind of corruption na hapo matajiri hawa watashikilia uongozi wa wananchi na kutoruhusu fikra tofauti kutoka katika makundi yaliyonyanganywa mali kutafuta kujikomboa.
tahadhari ni kuweka mifumo ya kudhibiti jamii zetu zisielekee katika hali hizo kabla hazijaanza kutokea kwa maana kama matajiri hao watakuwa wamekwisha jitambua na kuona mwelekeo itakuwa vigumu kuwazuia kwa maana nguvu ya pesa ni mbaya sana katika corruption.
tajiri anayepata mali kwa njia sahihi ni mtu mzuri sana katika jamii yoyote, lakini tajiri anayepata mali kwa corruption ni mtu hatari sana katika jamii. ni hatari kwa viongozi au mtu yeyote anayemtumia kwa maana akihisi hakuhitaji au akijisikia hofu au ukibadili mawazo itakula kwako na daima utakuwa mtumwa wake. lakini kwake yeye mpenda haki ni adui kwake, kwake fitina ndio ushindani, mtafuta mali kama yeye katika eneo lake ni adui yake.
katika kutengeneza katiba tuwaze mbali kuielekeza jamii yetu.
tusiweke mazingira ya fedha za kundi dogo kuteka vyombo vyetu vyote siku moja na kutugeuza watumwa tena.
lakini kama tukiweka mifumo ya kujihami na yenye kuhamasisha jamii kuzalisha nani atapata hasara? kwangu mimi nona mtanzania yeyote anapata faida zaidi pale nchi yetu inapotoka katika umasikini na kutoka katika umasikini si swala la kubahatisha bali zipo kanuni za kiunongozi na kibiashara, je sisi tunajielekeza huko?
unataka nisemeje wakati hilo linafahamika kuwa serikali sio kampuni??? Lol