ni vema ungefunguka kaka tukusikie labda una point za msingi kuhusu katiba inayopendekezwa.!!
Nitajitahidi. Naomba ustahimilivu lama nitashindwa kujieleza.
Binafsi nashindana na nafsi yangu kukata tamaa au kuendelea na vita ya kupigania amani haki na maendeleo ya mtanzania.
Kila mtanzania anatakiwa ajisikie kama mtu muhimu hapa tanzania. Lakini sasa kuna jinsi tumeshikiliwa na kitu fulani hadi kuona kama mipango muhimu si haki itokee kwa mwananchi'wa kawaida'
Neno siasa badala ya kuwa utashi mwema kwa mama Tanzania limekuwa kichaka cha kujificha wenye kutaka agenda zao za kibepari zihalalishwe au kufumbiwa macho na sheria.
Nilitamani wateule wetu wachache waongozwe na utakatifu wa chombo hiki katiba ambacho wamepewa jukumu kukitengeneza lakini kwa udhaifu wa nafsi zao wanajikuta wanapigania masilahi binafsi yao au ya kizazi chao.
Kuanzia mwanzo tumeona maoni na mawazo ya kuleta haki na uwazi katika mchaakato vikijadiliwa katika vikao tofauti vyenye utashi tofauti.
Itakuwaje amani iwe tunu haki isiwe tunu? Itakuwaje kama tusipoenzi ufanyaji kazi kwa bidii na uadilifu???
Tukiwa kwenye familia zetu maadili ya kwanza ni imani bidii uaminifu.
Inakuwaje maoni yetu kwa wingi wetu yanapuuzwa na watu wachache waliopigiwa kura na watu wachache watusemee?
Tanzania tumetoka mbali na safari ni ndefu.
Hakuna msafi ila kuna agenda safi.
Sipati shida kusimamia agenda nzuri toka kwa mtu mwenye historia chafu.
Wala kupinga agenda ya ovyo ya ndugu au rafiki yangu mpenzi.
Tusiogope, tusimamie agenda nzuri. Historia ituhukumu.
Tunaambiwa mwenye haki ataishi milele.
HAKI HAKI HAKI.
Tanzania