kutafuta chanzo cha migogoro ya jamii usiishie kwenye swali moja au mawili tu na ukafikia muafaka.
jiulize jamii kabla ya kuingia katika migogoro ilikuwa inaishi vipi? jiulize waliingiaje katika migogoro, jiulize migogoro yao kama imekuwa ikibadilika au ni ya aina moja, jiulize mambo mengi sana.
lakini katika yote hayo utagundua kuwa jamii zinaanzia katika kutokuwa na usawa, zinafuata propaganda za kueneza chuki na baadae jamii inaingia katika vurugu na vurugu hizi zinakuwa wakati mwingine zinabadilika au zinakuja na sababu tofauti tofauti.
hapa unaweza kulinganisha taifa linaloelekea katika vurugu na mwili wa mgonjwa wa ukimwi kwa maana mwili ukishakuwa dhaifu kila ugonjwa ni wake. jamii inapokuwa imekwisha vurugika kila vurugu inawezekana.
lakini kama tunaweza kutambua hayo ni kurekebisha mifumo ili ianze kufanya kazi na kila mwananchi ataridhika na utendaji.
nitakupa mifano.
zipo nchi zimeingia kwenye vurugu kwa sababu ya rasilimali za nchi watu wanaona haziwanufaishi wananchi. leo hii sisi hatutaki kutengeneza mifumo ili isimamie, unapokuwa huna mifumo ya kusimamia ukimpa mmoja wenu dhamana ya kuongea na wawekezaji basi anachukua rushwa anasaini mikataba ya kipuuzi maana mtoa rushwa anatoa ili apore apatiwe mkataba wa kumpa faida.
sasa anayepinga kuweka mifumo ya kusimamia katika nchi hii hivi kweli anajua anachokifanya
kama anajua je analitakia nini taifa hili kiuchumi, je analitakia nini taifa hili kiamani?
leo hii mnaleta wawekezaji mnalegeza masharti ili waje kuwekeza kwenu lakini mkijua baadae mtakuja kuwatoza kodi lakini kutokana na kutokuwepo kwa mifumo ya usimamiaji mnayemkabidhi ofisi ya kusimamia haya mda ukibaki mchache katika mkataba basi anachukua rushwa anaongeza mda wa mwekezaji huyu kutolipa kodi na mwisho ni nchi kutopata faida iliyolengwa.
hivi anayegangania nchi kutokuwa na mifumo ya usimamiaji anajua analolifanya au ni mbambaishaji tu, hivi analitakia nini taifa hili kiuchumi? hivi analitakia nini taifa hili kiamani?
leo hii taifa linakaa linabuni mashirika au taasisi na inaonekana wazi kuwa mashirika haya yataleta faida na tija kwa taifa. lakini kutokana na kutokuwepo kwa mifumo ya kusimaia na kudhibiti basi mnayemkabidhi ofisi kazi yake ni kuandaa miradi ya kutafuta mianya ya kujinufaisha, wanaandaa mipango ya kuibia ofisi zao.
katika mazingira kama haya nani anaweza kutuletea maendeleo?
katika mfumo kama huu hakuna mtu mmoja anaweza kudhibiti taifa hili bali ni kila mmoja wetu kuwa polisi kutokomeza haya.
kila mmoja wetu kuwa polisi ni kwa kufanya mifumo ya kitaifa ya usimamiaji ifanye kazi kwa maana raisi anasimamia walio chini yake ambao ni mawaziri, mawaziri wanasimamia walio chini yao, bodi, wakurugenzi wanasimamia walio chini yao. bunge linafanya kazi yake, mahakama inafanya kazi yake.
kila anayezembea hatua ya kwanza ni kumwajibisha mzembe na sio kumuunga mkono ili aendelee kuwa mzembe kwa kuwajibisha walio chini yake na yeye akabaki salama.
hapo kila mtu mwenye dhamana atawajibika kutekeleza majukumu yao.
katiba ndio sehemu pekee ya kufanya mifumo ifanye kazi.
wapo wababaishaji wachache ambao ndio wanatufanya tupotee lakini wapo watanzania makini wengi tu ambao mifumo ikifanya kazi watatuletea maendeleo kwa haraka sana.
Wewe unajifanya unajua sana theories za kuvuruga amani basi nenda Field work Somalia ukajiunge na Elshabab. Tanzania ninayoijua mimi imejengwa kwenye msingi imara Mvua zinakuja, Mafuriko yanakuja na Pepo zinakuja zinaipiga lakini haianguki ng'ooo kwa kuwa imejengwa juu ya Mwamba! mawazo uliyonayo hayako applicable in Tanzania nakuonea huruma mtoto!Na Katiba inayopendekezwa inakuja mwendo mswano ucpime!