swala la kujenga nchi liko wazi
nitakupa mfano wa familia, kama wewe ni kiongozi katika familia kwa maana wewe ni baba au mama. sasa umejitahidi kutafuta fedha na kununua mali au kuanzisha biashara. sasa mwanafamilia anayetafuta kuiba mali za familia pengine akiona umeleta hela anakwenda kupanga na majambazi waje kuiba na kumpatia sehemu kidogo tu ili akasterehe au anaiba mali ulizonunua kwa gharama kubwa na kwenda kuuza kwa bei za kutupwa ili apate fedha ya kutanulia na mgeni kutoka nje ya familia ambaye anaweza kuja nyumbani kwako akaangalia mali za familia, kama biashara unamuweka anasimamia na kuziendesha unapata faida.
kwa familia ni vigumu kumuuliza nani muhimu kwa maana kamba zilizofunga familia ni tofauti na zile zilizofunga taifa.
kama taifa tunayo mambo mengi ambayo tunataka kuyafanya.
ni faida sana kama mambo hayo tutayafanya kwa kutumia watanzania wenyewe.
lakini yapo mambo ambayo wageni wanaweza kuyafanya vizuri zaidi yetu.
sasa mgeni huyu anayeweza kuja kwetu akatutumikia kutusaidia tupate faida tukimlipa ujira ana faida zaidi kwa nchi yetu kuliko mtanzania ambaye anabomoa nchi yetu.
katika kubomoa lazima tusichukulie kuwa yeyote anayetofauti na wewe kimtizamo anabomoa au yeyote ambaye bahati mbaya system imeshindwa kumpatia jambo la kufanya anabomoa. lakini yapo mambo ya wazi kuwa huu ni ubomojai ambao yeyote anayeufanya hatuwezi hata siku moja kumthamini kwa kuzaliwa au kuandikishwa kwake tanzania na kumuona bora kuliko mgeni anayetusaidia kujenga nchi yetu.