sijui nikuiteje maana nikikueleza ukweli utasema nimekutukana.
bado narudia kilichotajwa katika kifungu kimoja cha katiba kama muundo wa katiba yenyewe hauwezeshi kilichotajwa katika kifungu hicho kimoja kupatikana on ground ni kama kifungu hicho hakipo.
kama katiba imetaja haki fulani lakini haiweki mifumo ya kuwezesha haki hizo zipatikane, katiba hiyo haiweki mifumo ya kusimamia ili wenye dhamana kutimiza wajibu wao, kama katiba haiweki mifumo ya kuhakikisha kuwa pale wenye dhamana wanapokiuka ni lazima haki itendeke, katiba hiyo yaweza kufanana na kitabu cha hadithi ambacho msomaji ana hiari ya kuyakubali au kuyakataa yale yaliyoandikwa.
tumefika hapa tulipo kutokana na wale wanaojidhani ni wataalamu wa uandishi wa katiba kumbe sometimes they can be ignorant katika mada hiyo.
nani ni mtaalamu inahukumiwa na kile kilichoandikwa kukidhi mahitaji ya kilichokusudiwa.
kama huwezi kutambua ukweli kuwa jambo lolote linalotajwa katika katiba, ndani ya katiba hiyo hiyo kuna mamlaka inatakiwa kutekeleza jambo hilo, kuna mamlaka inatakiwa kusimamia utekelezaji wake, kuna mamlaka ambayo ukiona hujatendewa haki unatakiwa unaweza kwenda kuidai huko.
kimsingi nilichokisema ni kuwa katiba ni sawa na treni. kwa kawaida treni ina kichwa ambacho huvuta mabewa. haki za makundi ni sawa na mabehewa ambapo kundi linakimbilia kuangalia sisi behewa letu lipo? lakini hapa tukumbuke kuwa mabehewa yetu yanaweza kuwepo lakini kichwa cha kubeba mabehewa haya je kipo?
hapa tunachokifanya watanzania ni kuunda treni yetu, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa tunatengeneza kichwa cha kuvuta mabehewa yote na tukisha maliza kutengeneza kichwa ndio sasa makundi yaanagalie mabehewa yao.
kichwa ni mihimili mitatu kuhakikisha inakuwepo.
kuwepo kwa mihimili mitatu sio kuitaja tu katika vifungu bali ni kuhakikisha mihimili hii kila mmoja haumezwi na mhimili mwingine na hakuna mhimili unaoweza kuwa na nguvu zaidi ya mingine.
lengo hapa ni kutokana na rasilimali za jamii kutowezekana kwa jamii kuzisimamia yenyewe moja kwa moja hivyo jamii inalazimika kutengengeneza vyombo ambavyo vitafanya kazi ya jamii kwa kusimamiana vyombo vyenyewe.
ukiwa na chombo kimoja au chombo kimoja chenye nguvu au vikaungana na kuwa chombo kimoja matokeo yake ni uwezekano wa chombo hiki kimoja au chombo chenye nguvu kupora madaraka ya wananchi.
mtaalamu wa uandishi wa katiba anayeweza kujigamba ni si yule wa kuangalia kifungu kimoja kimoja kinasemaje bali ni yule anayeweza kutengeneza "checks and balansi " katika mtiririko mzima wa katiba na kujumuisha mambo muhimu yote.
katiba sio tu kile kilichotajwa bali katiba nzima inasimamiaje yale yalitotajwa.
Kama unataka kujua mfumo wa ulindaji wa hizo haki narudia tena coz nimeshakuandkia kweny post nyingne......... nenda kasome ibara ya 65 kuanzia (1)-(6) sikwambii inasemaje ila take ua time n read halafu urudi tena huku...