Kundi la M23 latangaza uongozi wake katika eneo la Kivu, hofu ya kuundwa taifa huru yaibuka

Kundi la M23 latangaza uongozi wake katika eneo la Kivu, hofu ya kuundwa taifa huru yaibuka

Kama wamefanikiwa kumega Congo na kuifanya sehemu yao waishie hukohuko wasitamani kumega maeneo ya magharibi mwa Tanzania watapigika mpaka kwao wakose na hilo eneo walililolimega
 
Leo hali ilikuwa shwari baada ya mapigano ya jana na juzi. Jana na juzi mapigano yalikuwa makali ambapo m 23 na AFD walipata kipigo na kuondoshwa kutoka katika sehemu walizozikalia.

M 23 sasa wapo Ruchuru ambapo huko wamewachagua viongozi wa serikali za mitaa,ili waongoze kwa niaba yao.

Vikosi vya m 23 na washirika wao wamepata pigo kubwa sana,na mimi ningekuwa mnajimu ningesema Paul Kagame amekalia kuti kavu,kwa sasabu bila shaka sasa ,hasira dhidi ya Paul Kagame itakuwa kubwa sana huko Rwanda.

Lakini rais wa Poland jana labda ameleta nuru katika giza aliposema kama usalama wa Rwanda unatishiwa Poland iko tayari kusaidia.

Ni uongo kabisa unayoona katika vyombo vya habari,kwamba m 23 inatisha watu huko DRC. M23 wanapigwa na Kamanda mmoja wa Wazalendo alikuwa anaeleza sasa hivi kwamba wameithibiti Sasha. Huyu Colonel wa Wazalendo anasema kwamba wamefanikiwa kuwatimua m23 waliokuwepo Sasha. ( Hili jina la huu mji sijui kama nimelipata sawa kwa sababu Sasha ni jina la mtoto wa Barack Obama. Ah,Sasha! Ule mji unaitwa Shasha. M23 wametimuliwa Shasha).

Sasa,huko Kinshasa wameandamana kuelekea Ubalozi wa Marekani jana,na leo wamekwenda Ubalozi wa Uingereza. Wanasema hizi nchi mbili hazifanyi juhudi ya kutosha kuumaliza mzozo wa DRC. Pia sasa Warusi wanasema wataisaidia Kongo kama vita itaendelea,watamsaidia Felix Antoine Tshitsekedi.

Halafu yapo malalamiko ya hapa na pale kwamba jeshi la Kongo FRDC,linawakamata watu wote wanaoongea na lafudhi ya Kinyarwanda. Hawa watu wanaitwa wapelelezi wa m23. Hawa watu wanakamatwa wanapelekwa Kinshasa for interrogation.

Halafu leo amefika mjumbe wa UN kuwahakikishia Wakongomani kwamba UN itashirikiana nao kuwaondoa m23. Lakino ukweli no kwamba MONUSCO wanajitayarisha kuondoka,na wanaanza kwa kuondoka South Kivu,ambako ndiko huko huko yalipo mapigano.

Sasa hivi wanaopigana huko wansopigana ni majeshi ya Afrika Kusini,Malawi na Tanzania dhidi ya hao rebels.
Ingawa Mama Samia anatueleza kwamba majeshi yetu,they are shooting at nobody,lalonyo tunaona picha majeshi yetu yakiwalenga waasi na makombora ya masafa marefu.

Leo imekuwa shwari kidogo,wamekuwa wanazingukazunguka katika uwanja wa vita wanafanya clearing,wanaokota maiti; utawasikia wanasema," huyuguru ulikatika"," Tazama hspa,mguru hakuna." Utasikia wanasema,"hii mbwa ililungula."

Mambo yenyewe ndio hivyo. M23 imeanzisha mtindo mpya. Inaunda Baraza za Serikali za mitaa zinazoongozwa na wenyeji wa pale.

Huu nadhani ndio mtindo mpya wa majeshi ya siku hizi. Zamani walikuwa wanasema kazi ya kiongozi wa jeshi ni Command and Control. Na wakisema Command( wana maana,toa amri) na Control( ina maana,hakikisha kwamba ile amri inatekelezwa).

Lakini siku hizi wanasema Mission Control,wanasema viongozi lazima wawape walio chini yao madaraka makubwa zaidi ya kufanya maamuzi.

Hapa nadhani kuna hitilafu. Mungu wangu,jambo la mwisho unalotaka unapotoa amri ni askari ajiulize,hii amri niifuate au nisiifuate?
 
Back
Top Bottom