Kundi la watu wachache linapofanikiwa kupitiliza husababisha chuki na wivu, haya ni matukio yaliyopelekea kuuawa, kufukuzwa, kubaguliwa

Kundi la watu wachache linapofanikiwa kupitiliza husababisha chuki na wivu, haya ni matukio yaliyopelekea kuuawa, kufukuzwa, kubaguliwa

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
Katika historia ya dunia, kumekuwa na matukio ambapo makundi ya watu wachache yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kijamii, kisiasa, kielimu, kiuchumi, n.k. Hali hii mara nyingi imepelekea chuki kutoka kwenye kundi kubwa na hatimaye mauaji ya kimbari (genocide), kuwafukuza, n.k. Aidha, wachache hawa mara nyingi walitumiwa kama "mbuzi wa kafara" wakati mambo hayakwenda vizuri katika nchi zao. Hapa kuna mifano ya kihistoria:

1. Wahutu na Watutsi wa Rwanda

1737915082656.png


Ingawa kabila la Watutsi lilikuwa wachache, walikuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiuchumi chini Rwanda hata kabla ya uhuru, Hali hii ilipelekea Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (1994) ambapo Wahutu waliwaua Watutsi zaidi ya 800,000 ndani ya siku 100.

Hata hivyo hali hii inahofiwa kuzuka tena kwasababu Rwanda ya sasa nafasi za juu nyingi, fursa za elimu, biashara, n.k. wamejaa watutsi.

2. Wayahudi Ulaya


1737914990391.png


Wayahudi walipopelekwa ulaya kama watumwa baada ya kushindwa vita waliteswa kwa karne nyingi. Walizuiliwa kumiliki ardhi na kushiriki katika taaluma kama vile Kilimo na kuuza ardhi.

walianza kutilia mkazo kwenye elimu kwa kuwa utamaduni wao unaipa kipaumbele elimu na wakaweza kufanikiwa kupata ajira nzuri kama usimamizi wa fedha, sheria, uhandisi na tiba. haikuishia hapo walipata mafanikio makubwa zaidi kwenye biashara na kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya benki

Hata hivyo watu wengi hawakupenda maendeleo yao kwa kuona wamepigwa gap refu sana, viongozi waliwageuza kuwa "mbuzi wa kafara" pale uchumi uliporomoka ama nchi iliposhindwa vita, Matokeo ya chuki hizi yalipelekea mauaji ya Holocaust, ambapo Wayahudi milioni sita waliuawa chini ya utawala wa Hitler.

3. Wachina Kusini-Mashariki mwa Asia

1737915142049.png


Katika nchi kama Ufilipino, Indonesia, Malaysia na Thailand, Wachina walihamia kwa wingi na walifanikiwa hasa katika sekta za biashara na uchumi. Walimiliki biashara kubwa, huku wakiwa na ushawishi mkubwa wa kiuchumi. Mafanikio haya yaliibua wivu mkubwa.

Kuzilizuka Ghasia za 1998 nchini Indonesia, Wachina walilengwa wakati wa machafuko ya kisiasa na kiuchumi. Biashara zao ziliharibiwa, waliuliwa na wengi walilazimika kukimbia.

4. Waigbo wa Nigeria

1737915181146.png

Hapo zamani Nigeria ilipopata uhuru waigbo walionekana kuwa na mafanikio makubwa sana, hali zao zilikuwa tofauti sana na wanaigeria wengine, hii ilipelekea Vita vya Biafra (1967–1970): Waigbo walijaribu kujitenga kutokana na ukandamizaji waliokumbana nao, lakini vita hiyo ilisababisha mauaji makubwa na mateso kwa jamii yao.

Waigbo walionekana kama "wanaojinufaisha" kutoka kwa uchumi wa nchi, hali iliyochochea chuki za kikabila na kuhalalisha kuanza kuwabagua.

Baada ya vita waigbo walifilisiwa mali zote na kila moja aliachiwa pesa ndogo pauni 20 tu, hata hivyo ni ndani ya muda mchache sana wakajirudi kiuchumi kupitia biashara, leo hii waigbo ndio kabila kenye watu wengi kuwa na mafanikio Nigeria, Licha ya hivi bado serikali inawakandamiza kwenye soko la ajira, kuwabana kimaendeleo mikoa yao, hivyo waigbo wanalazimika kwenda mikoa mingine kutafuta maisha.

5. Wahindi Afrika Mashariki

1737915278429.png


Wahindi waliletwa Afrika Mashariki na wakoloni wa Uingereza kama wafanyikazi na wachuuzi. Walifaulu sana katika biashara na kumiliki uchumi wa nchi kama Uganda, Kenya, na Tanzania.

Rais Idi Amin wa Uganda aliwafukuza Wahindi akiwatuhumu kushikilia uchumi wa nchi, Biashara na mali zao zilitwaliwa kwa nguvu. Hali hii ilionyesha jinsi wachache wenye mafanikio wanaweza kuwa waathirika wa siasa za ndani.


6. Waarmenia wa Dola ya Ottoman

1737915329115.png


Waarmenia walikuwa wachache wenye mafanikio makubwa ndani ya Dola ya Ottoman. Walikuwa maarufu katika sekta za biashara, elimu, na sanaa. Mafanikio yao yaliwafanya waonekane kama tishio.

Waarmenia zaidi ya milioni moja waliuawa katika mauaji ya halaiki yaliyopangwa na serikali ya Ottoman 1915 hado 1917.

Waarmenia walitafutiwa kisingizio cha njama za kisiasa, hali ambayo ilitumika kuhalalisha mauaji hayo.
 
Mafanikio huwa yanaleta majivuno na dharau. Binadamu hapendi kudharauliwa.
watu wengi wanachukiwa kwa mafanikio yao kwasababu wengine hawajafikia sehemu walipo.

hata uwe mwema unaweza kuchekewa mbele ya uso lakini anaekuchekea hapendi mafanikio yako
 
Tunafanya biashara ili kupata faida,

Ili upate faida nzuri lazima umlalie mteja

Mifumo yote ya kupata Ela duniani Ina unyonyaji ndani yake.

Iwe siasa,kilimo,uchumi, n k
 
Mafanikio huambatana na unyonyaji.
mtu katoka familia masikini, kakaza shuleni kawa profesa mshahara milioni 5 unyonyaji upo wapi ?

mtu anaagiza battery za vitochi kutoka China shilingi 300 kwa piece, Kariakoo anauza piece kwa buku, unyonyaji upo wapi ?
 
watu wengi wanachukiwa kwa mafanikio yao kwasababu wengine hawajafikia sehemu walipo.

hata uwe mwema unaweza kuchekewa mbele ya uso lakini anaekuchekea hapendi mafanikio yako
Mafanikio ya mmoja mmoja hayana shida. Shida huanza pale kikundi cha watu wa chache wa aina fulani kinapofanikiwa. Kwanza wafanikiwe kama kikundi wengi wanakuwa wajamaa kati yao na mabepari kuelekea wengine. Hili tu pekee yake huleta mgongano. Mfano baadhi ya Wayahudi wanaamini watu wengine wote(Gentiles) wameumbwa ili kuwatumikia.
 
Back
Top Bottom