Uchaguzi 2020 Kundi la WhatsApp lachukua sura mpya baada ya Tundu Lissu kutangazwa Mgombea Urais CHADEMA

Uchaguzi 2020 Kundi la WhatsApp lachukua sura mpya baada ya Tundu Lissu kutangazwa Mgombea Urais CHADEMA

Lazia Sultan

Senior Member
Joined
Jun 4, 2020
Posts
120
Reaction score
328
Nipo kwenye group la graduates mwaka fulani wa nyuma, ambao tulinufaika na Loan board kipindi cha Kikwete, na ajira ya Kwanza(first appointment) tukiwa na Kikwete. Tunakumbushana mengi tu hasa Neema za kipindi hicho cha nyuma.

Wadau wengi wa kundini walitia Nia kupitia chama tawala(sikuona chama pinzani aliyepost kundini ingawa walikuwepo, nawafahamu) picha za kijani zilijaa kwenye devices zetu, hadi watu wakafikia hatua kushauri tuwachangie fedha za kuchukulia fomu, ingawa hoja hiyo ilipotea hewani na wengine waliishia kuleft. Wakati huo watu wenye itikadi tofauti na chama cha kijani walionekana kuwa wachache sana.
Hivi sasa napata picha kuwa kumbe wale walioleft hawakuwa na 'Political tolerance' tuliobaki active kwenye agenda za kisiasa nadhani ni mimi na wenzangu Kama wanne hivi Kati ya wanagroup zaidi ya 300.

Aisee watu ni waoga ati! Lile group limebadili gia angani tangu kutangazwa kwa TL kuwa Mgombea Urais CHADEMA. Wanakijani wanahesabika Kama wakivyohesabika wa rangi nyingine hapo awali. Picha ya Tz yetu kwa sasa nimeipata kupitia grupu langu la wasap. Grupu lina wasomi na maafisa wengi tu walioendelea na masomo hadi PhD. Tulikuwa tunaogopana lakini tangu 3/8/2020 woga umeisha.

Utawala huu umeniadhibu mambo kadhaa makubwa ambayo sitokuja kusahau maishani. Nadhani tupo wengi nyuma ya haya na mengine.

1.Baba yangu kastaafu tangu October 2017, yapata miaka miwili na nusu hajapata mafao yake hadi leo. Amehangaika, akapatwa na stroke ingawa alikuwa na historia ya BP ila nadhani hili limechangia. Ameparalaizi kwa sasa.

2. Mimi na mdogo wangu tulipata ajira ya ualimu wa sekondari 2009 na 2011. Serikali ikatupeleka kufundisha shule za msingi mwaka 2018. Si vibaya kufundisha msingi lakini iliniuma kuona wenye degree tunapelekwa msingi na wenye diploma wanabaki secondary Schools. Bila kujali seniority kazini(umri kazini) yaani miaka yangu 9 kazini unanipeleka kwenye kazi ambayo sikuisomea na Wala kuifikiria halafu unamwacha dogo wa diploma mwenye miaka 5 kazini. No!! Huu siyo utumishi wa umma.

3. Uhakiki wa vyeti feki ulinifurahisha sana, niligundua walimu wengi wana vyeti zaidi ya kimoja, yaani waliunga unga elimu(wali resit) na wengine walisomea majina tofauti ili warudie darasa. Cha kushangaza hao hao waliachwa wafundishe sekondari sisi wenye division one(na umahiri katika masomo) tukapelekwa shule za msingi, kisa tunamchalenji hedimasta. Kuna shule ambazo wanafunzi waliandamana kupinga uhamisho onevu wa competent teachers mwaka 2018, waliopelekwa msingi.

Niliacha kazi ya serikali nikaenda private school na baadae kwenye biashara za mazao hadi leo hii. Naiona Tanzania yenye HAKI na Usawa mbeleni kama Uongozi utageuka upande wa pili, Binafsi natamani hivyo na dalili naoina.
Time will tell!!
 
Raia wengi hawaikubali serikali hii, sema walinyimwa kuonyesha choice ya allegiences zao za kisiasa kutokana na upinzani kubanwa sana kufanya siasa.

Ujasiri wa Lissu unainspire watu wengi kuonyesha hisia zao halisi

Ukweli ni kuwa Magufuli hakubaliki sana, ila propaganda zimesukwa ionekane as if anakubalika mno
 
Raia wengi hawaikubali serikali hii, sema walinyimwa kuonyesha choice ya allegiences zao za kisiasa kutokana na upinzani kubanwa sana kufanya siasa.

Ujasiri wa Lissu unainspire watu wengi kuonyesha hisia zao halisi

Ukweli ni kuwa Magufuli hakubaliki sana, ila propaganda zimesukwa ionekane as if anakubalika mno
Hakika wananchi wengi wameichoka CCM......

Ila hivi sasa ndiyo kimbunga kimeanza kujionyesha baada ya Chadema kumchagua Tundu Lissu kuwa mgombea wake, kwa kiti cha Urais
 
Back
Top Bottom