Uchaguzi 2020 Kundi la WhatsApp lachukua sura mpya baada ya Tundu Lissu kutangazwa Mgombea Urais CHADEMA

Uchaguzi 2020 Kundi la WhatsApp lachukua sura mpya baada ya Tundu Lissu kutangazwa Mgombea Urais CHADEMA

Hongereni sana Bavicha naona ajira imepatikana na mumeanza tena ngonjera za kwenye mitandao ya kijamii kujiaminisha kuwa eti mnakubarika wakati. Hizo keyboard mlizozikusanya Chumba kimoja mnajijibu wenyewe siasa hizo ziliisha pitwa na wakati.

Ukitaka kuwavuta Wapiga kura waeleze ukiwa kiongozi wa Chadema Jimbo flani au nafasi flani ndani ya Chadema umesaidia vipi kuhakiisha Changamoto ya ajira kwa Wanachadema imeondolewa kwa kutumia vyanzo vya ndani vya Chadema, Umeshiriki vipi kuishauri Serikali kama Mbunge ukiwa Bungeni na wapi ulifanikiwa au eleza kwanini ulikuwa unachukua Posho na unakimbia Bungeni.

Waeleze Wananchi Mwenyekiti wa Chadema kwanini alibadilisha Katiba ya Chadema ili awe Mwenyekiti wa kudumu , na kwanini anajiamini peke yake na kwanini hawaamini Wenzake na Mara nyingi wanaogusa kiti wanaishia kutandikwa Risasi Mfano Waliompiga shaba Mgombea Kikosi maalum cha Mwenyekiti, kuwaita Wasaliti wengine na kuwafukuza uanachama Mfano Zitt Kabwe n.k.

Mnatakiwa kuwaeleza Wananchi kwamba Ruzuku ya Chadema imekinufaisha vipi Chadema.
Mnatakiwa kuwaeleza Wananchi kuwa Mbowe Makato aliyokuwa anawakata Wabunge fedha zilikuwa zinaenda wapi.

Mnatakiwa kuwaeleza Wananchi kuwa utaratibu wa kuwapata Wabunge viti Maalum Mlikuwa mnatumia utaratibu gani na mbona mapka saizi haupo wazi na Wengi wao walikuwa ni babies kutoka hukooooo kwao.

Mnatakiwa kuwaeleza Wananchi kuwa kwanini Chadema hakina Ofisi, na Ofisi ya Chadema ni Mifuko ya Watu. Mnatakiwa kuwaeleza Wananchi kuwa Bilion 900 za Whitehair zilienda wapi na zimefanya nini yakowemo Magari. Hayo ni baadhi ya kuwaeleza Wananchi.

Sidhani kama mnauwezo wa kuwafumbisha Macho Wananchi wasioone Flyover, Viwanja vya NDEGE, Kufufuliwa kwa shirika la Ndege ATC, na Miradi mingi mikubwamikubwa sidhani kama eti Chadema hapo ambapo na nyie mnapaona mtakuwa na hoja labda za kuburudisha na kupumbaza Watu.

NB: Eti issue ya Lissu kutandikwa Risasi Mbw ni mwagizaji 😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Naiona Tanzania yenye HAKI na Usawa mbeleni kama Uongozi utageuka upande wa pili, Binafsi natamani hivyo na dalili naoina.
Time will tell!!
Mkuu Lazia, kwanza nimeguswa sana na maswahibu uliyppitia, pole sana kwa mapito hayo, pili ni kweli tunakwenda kupata Tanzania njema na yenye haki na usawa mbeleni, ila ni kwa upande ule ule na sio upande wa pili, kwasababu kwa mfumo, hakuna uwezekano wa upande pili kutoboa!, ila kitu kizuri ni upande uliopo unabadilika, mabadiliko chanya kwenye utoaji haki yameisha anza, hivyo awamu ya pili ni neema tupu!.

Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The Better!. Hongera Sana!

Magufuli is Doing Good For This Nation, Tumuassess kwa Positive Attitude, Kwa Mazuri Tumpongeze, Tumuunge Mkono Kumsupport, lakini kwa Mabaya Tumkosoe

Kiukweli nimeguswa sana na uchapakazi wa Rais Magufuli!. Je, kuna uhusiano kati ya kabila la mtu, na uchapakazi wake?. Je, 2020 kuna haja ya...

P
 
Acha uongo hakuna mstaafu asiyelipwa mafao yake zaidi ya miezi sita baada ya kustaafu. Tatizo lenu mnaleta uongo wa kitoto sana.
Wewe kama bibi na babu yako wamelipwa haina tafsiri kwamba "wote" wamelipwa, hii habari ya watu kitokulipwa mafao yao ni dhahiri kabisa, nina mzee wangu alistaafu tangu August,2018 mpaka leo bado hajapewa haki yake!

Ukweli ni kwamba mzee Magu ana roho ya kikatili, achilia mbali wazee hao (ambao hawajalipwa), najaribu kumtazama namna anavyodhulumu haki za watumishi wa umma kwa sasa!

Kwa miaka 5 ameikanyaga sheria ya utumishi wa umma, kwani kutowaongezea basic salary maana yake hakuna nyongeza yoyote kwenye mchango wa mfuko wa hifadhi ya jamii (kwa miaka yote ya uongozi wake)

Wakati huo huo Kuna sheria ipo "pending" ya kulazimisha wastaafu kuchukua 25% ya mafao yao kwa kisingizio cha "kuwatunzia" wastaafu pesa zao wakati wao (viongozi Magu akiwemo) kwa miaka yote wamekuwa wakijikwapkulia pesa zao zote kila baada ya miaka mitano utadhani wao hawazeeki (high level of selfishness)

Huyu mzee ni katili mnoooooo!
 
Jana nilimtibu mama mmoja 62yrs,akaniambia mwili unamuuma sana anahisi in sababu ya kazi ngumu anayofanya ya kugonga kokoto. Baadae akaniambia yeye ni Mwalimu amestaafu 2018 lakini mpaka leo hajalipwa mafao yake.

Huyo Mother nimemkuta na BP 200/110 mmHg na RBG 15mmol/dl, halafu kachanganyikiwa na kufuatilia pesa yake ya kustaafu amesahau hata kufuatilia NHIF card ya mstaafu na pesa hana anvunja kokoto. Nimemuambia afuatilie hiyo card ya NHIF imesaidie kwenye matibabu.

Magufuli anatesa sana watu,hali ni mbaya sana.
Magufuli kaungaanisha mifuko yaa jamii ili achote vizuri michango ya wanachama, mifuko inabaaki mitupu mpaka wastaaafu wanakosa pesa za malipo yao
 
Natamani siku chadema ichukue nchi ili tuone maajabu watakayo fanya. Tatizo hii ni ndoto
 
Acha uongo hakuna mstaafu asiyelipwa mafao yake zaidi ya miezi sita baada ya kustaafu. Tatizo lenu mnaleta uongo wa kitoto sana.
Usiwasemee watu. Kaka yangu alistaafu tangu August 2016 bahati mbaya akafariki February 2017. Tulifuatilia mafao for 3 years yamelipwa June 2020. Usitutie hasira watu tulioathirika na hii system
 
daaaaaah
Wadau katika silidi nzima wamegungua whatsap kua na member 300.
 
Raia wengi hawaikubali serikali hii, sema walinyimwa kuonyesha choice ya allegiences zao za kisiasa kutokana na upinzani kubanwa sana kufanya siasa.

Ujasiri wa Lissu unainspire watu wengi kuonyesha hisia zao halisi

Ukweli ni kuwa Magufuli hakubaliki sana, ila propaganda zimesukwa ionekane as if anakubalika mno
mnanifurahisha mnavyojipea moyo, sio mbaya kuota lkn
 
C
Nipo kwenye group la graduates mwaka fulani wa nyuma, ambao tulinufaika na Loan board kipindi cha Kikwete, na ajira ya Kwanza(first appointment) tukiwa na Kikwete. Tunakumbushana mengi tu hasa Neema za kipindi hicho cha nyuma.

Wadau wengi wa kundini walitia Nia kupitia chama tawala(sikuona chama pinzani aliyepost kundini ingawa walikuwepo, nawafahamu) picha za kijani zilijaa kwenye devices zetu, hadi watu wakafikia hatua kushauri tuwachangie fedha za kuchukulia fomu, ingawa hoja hiyo ilipotea hewani na wengine waliishia kuleft. Wakati huo watu wenye itikadi tofauti na chama cha kijani walionekana kuwa wachache sana.
Hivi sasa napata picha kuwa kumbe wale walioleft hawakuwa na 'Political tolerance' tuliobaki active kwenye agenda za kisiasa nadhani ni mimi na wenzangu Kama wanne hivi Kati ya wanagroup zaidi ya 300.

Aisee watu ni waoga ati! Lile group limebadili gia angani tangu kutangazwa kwa TL kuwa Mgombea Urais CHADEMA. Wanakijani wanahesabika Kama wakivyohesabika wa rangi nyingine hapo awali. Picha ya Tz yetu kwa sasa nimeipata kupitia grupu langu la wasap. Grupu lina wasomi na maafisa wengi tu walioendelea na masomo hadi PhD. Tulikuwa tunaogopana lakini tangu 3/8/2020 woga umeisha.

Utawala huu umeniadhibu mambo kadhaa makubwa ambayo sitokuja kusahau maishani. Nadhani tupo wengi nyuma ya haya na mengine.

1.Baba yangu kastaafu tangu October 2017, yapata miaka miwili na nusu hajapata mafao yake hadi leo. Amehangaika, akapatwa na stroke ingawa alikuwa na historia ya BP ila nadhani hili limechangia. Ameparalaizi kwa sasa.

2. Mimi na mdogo wangu tulipata ajira ya ualimu wa sekondari 2009 na 2011. Serikali ikatupeleka kufundisha shule za msingi mwaka 2018. Si vibaya kufundisha msingi lakini iliniuma kuona wenye degree tunapelekwa msingi na wenye diploma wanabaki secondary Schools. Bila kujali seniority kazini(umri kazini) yaani miaka yangu 9 kazini unanipeleka kwenye kazi ambayo sikuisomea na Wala kuifikiria halafu unamwacha dogo wa diploma mwenye miaka 5 kazini. No!! Huu siyo utumishi wa umma.

3. Uhakiki wa vyeti feki ulinifurahisha Sana, niligundua walimu wengi wana vyeti zaidi ya kimoja, yaani waliunga unga elimu(wali resit) na wengine walisomea majina tofauti ili warudie darasa. Cha kushangaza hao hao waliachwa wafundishe sekondari sisi wenye division one(na umahiri katika masomo) tukapelekwa shule za msingi, kisa tunamchalenji hedimasta. Kuna shule ambazo wanafunzi waliandamana kupinga uhamisho onevu wa competent teachers mwaka 2018, waliopelekwa msingi.

Niliacha kazi ya serikali nikaenda private school, na baadae kwenye biashara za mazao hadi leo hii. Naiona Tanzania yenye HAKI na Usawa mbeleni kama Uongozi utageuka upande wa pili, Binafsi natamani hivyo na dalili naoina.
Time will tell!!
CCM .OYEEEE
CCM.JUUU
KIDUM CHAMA CHA MAPINDUZI
CCM2025
AMKATWENDE
 
NIMEMWELEWA MZEE BASHIRU SASA
CCM SIO CHAMA CHA MITANDAONI
ATUCHAGUI RAISI WA MITANDAON TUNACHAGUA RAISI WA WATANZANIA

AISEE .,NAHIKI KITUKO SASA NAMWELEWA
TENA
GRADUATES LOH
 
Nimeshakufahamu umemaliza 2010 ud pole sana magufuli for life
 
NIMEMWELEWA MZEE BASHIRU SASA
CCM SIO CHAMA CHA MITANDAONI
ATUCHAGUI RAISI WA MITANDAON TUNACHAGUA RAISI WA WATANZANIA

AISEE .,NAHIKI KITUKO SASA NAMWELEWA
TENA
GRADUATES LOH
Graduates hawana ajira,hali ngumu,democracy,human rights,watumishi wa umma hakuna nyongeza kwa miaka mitano,uhuru wa mahakama,
Niendelee ?
 
Sipati picha kampeni mwaka huu zitakuwaje maana huyu Magu ametenda jinai kibao sana.Kama kutakuwepo na free and fair election lolote laweza kutokea mwaka huu.CCM kila kukicha naona wana loose ground kwa kasi sana ! Mungu tenda miujiza

Back
Top Bottom