Uchaguzi 2020 Kundi la WhatsApp lachukua sura mpya baada ya Tundu Lissu kutangazwa Mgombea Urais CHADEMA

Uchaguzi 2020 Kundi la WhatsApp lachukua sura mpya baada ya Tundu Lissu kutangazwa Mgombea Urais CHADEMA

Wewe ni muongo tu kama waongo wengine.
kuna maneno umeandika ukiyatafakari mojakwamoja mtu anagundua kuwa wewe ni muongo.
 
Raia wengi hawaikubali serikali hii, sema walinyimwa kuonyesha choice ya allegiences zao za kisiasa kutokana na upinzani kubanwa sana kufanya siasa.

Ujasiri wa Lissu unainspire watu wengi kuonyesha hisia zao halisi

Ukweli ni kuwa Magufuli hakubaliki sana, ila propaganda zimesukwa ionekane as if anakubalika mno

Kunywa chochote kwa Mangi nakuja kulipa. Alichokifanya Magufuli ni kushurutisha kukubalika, na amehakikisha kuwa yeye tu ndio anatangazwa. Matokeo yake wanafiki ndio wanaeneza kuwa anakubalika sana, na yoyote anayeonesha kutomkubali, anahujumiwa kwenye shughuli zake halali za kumuingizia kipato, kutekwa, ama kufanyiwa unyama wa hatari. Hiyo imepelekea wote wasiomkubali kukaa kimya kulinda usalama wao.
 
Masuala ya
  1. COVID 19;
  2. Kodi Kwa vikoba;
  3. Viwango vya juu vya Bima ya afya;
  4. Vurugu kwenye sekta binafsi na NGOs;
  5. Sheria zinazokandamiza haki na Uhuru wa kujieleza;
  6. Wananchi kubambikizwa kesi za utakatishaji pesa; na
  7. Wastaafu na wakulima kutolipwa Kwa wakati au kutolipwa kabisa.
Hayo yote, pengine pamoja na mengineyo kadhaa ni popular policy areas kuwekwa kwenye ilani za vyama vya upinzani pamoja na kujua namna ya kuzi-articulate kwa wananchi.
Watapata ushindi wakiweza kusimamia Sera hizo.
 
Mtoa post bwana😊😊😊

Najua baada ya oktoba 28 2020 utakuja tena hapa kulalamika
 
Hilo group tupo wote endeleeni na mambo yenu mahesabu October 29,30.
 
Niliacha kazi ya serikali nikaenda private school, na baadae kwenye biashara za mazao hadi leo hii. Naiona Tanzania yenye HAKI na Usawa mbeleni kama Uongozi utageuka upande wa pili
Para ya mwisho inajieleza
Ukisoma sio lazima kuajiriwa,si umeiona guess umepata kivingine,chuki ya Nini?
 
Jana nilimtibu mama mmoja 62yrs,akaniambia mwili unamuuma sana anahisi in sababu ya kazi ngumu anayofanya ya kugonga kokoto. Baadae akaniambia yeye ni Mwalimu amestaafu 2018 lakini mpaka leo hajalipwa mafao yake.

Huyo Mother nimemkuta na BP 200/110 mmHg na RBG 15mmol/dl, halafu kachanganyikiwa na kufuatilia pesa yake ya kustaafu amesahau hata kufuatilia NHIF card ya mstaafu na pesa hana anvunja kokoto. Nimemuambia afuatilie hiyo card ya NHIF imesaidie kwenye matibabu.

Magufuli anatesa sana watu,hali ni mbaya sana.
Very sad, yani huyu jamaa na serikali yake anakula pesa za wastaafu halafu kila kukicha anagawa hizo pesa zao barabarani kama karanga, hii ni laana anayoitafuta.
 
Ushahidi upo Mgombea TL ni mprnda haki na utawala bora. Manyanyaso haya hawezi kuyaepuka chini ya mtawala yeyote kutoka ccm
Unasema kwa hisia au uhalisia? Una ushahidi kuwa Lissu ndivyo alivyo?
 
Naona wengi kwenye huu uzi badala ya kujadili content za mleta mada, wanaishia kujadili idadi ya members wa group la whatsap, haya ndio mawazo halisi ya mtz wa leo.
Kwenye magrup huko wapo hivyo hivyo. Tena pengine kuna watu humu wapo kwenye group ninalolizungumzia. Namna ya uandishi wao na hoja zao, ni zile zile.
 
Raia wengi hawaikubali serikali hii, sema walinyimwa kuonyesha choice ya allegiences zao za kisiasa kutokana na upinzani kubanwa sana kufanya siasa.

Ujasiri wa Lissu unainspire watu wengi kuonyesha hisia zao halisi

Ukweli ni kuwa Magufuli hakubaliki sana, ila propaganda zimesukwa ionekane as if anakubalika mno
Subiri siku ya kura ndio utaelewa, hata Kwa Lowassa 2015 mlikuwa mnamshagilia hivi mwisho wa siku mkaanza mara ccm imeiba kura, chadema iko mjini ambako watu wengi hawapigi kura, tena mwaka huu ndio amna mwamko kabisa maana hata kujiandikisha watu walikuwa kama wanabemberezwa. Kama alishindwa Lowassa kungoa ccm ambaye aliondoka na Wenyeviti na wa fanya biashara akina Lostam, Manji, bado Lowassa alisanda eti ameibiwa kura wakati hakufikisha hata wabunge 100 sijui hata kama angeshinda serikali angeliundaje. Sasa subiri kichapo atatacho kipata Lissu atasahau maisha yake yote
 
Mbona unakomalia vitu vidogo vidogo. Hayaa amedanganya umefrai?? Punguza ujuaji.

Jadili mada mezani.
Achana na mimi kwani umelazimishwa kusoma nilichoandika? Nilikuwa na maana yangu kuuliza hilo swali na comments zilizofuatia nilikuwa najibu kulingana na nilivyoqutiwa
 
Back
Top Bottom