Kundi la Yanga ndio litatoa bingwa wa hii michuano

Kundi la Yanga ndio litatoa bingwa wa hii michuano

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Huu ndio ukweli na ndio maana mpaka leo timu namba moja kwa ubora bado haina uhakika wa kutinga robo fainali(mpaka sasa inahaha kuingia robo fainali).

Labda Mamelodi ndio anaweza kuleta ushindani.
 
Huu ndio ukweli na ndio maana mpaka leo timu namba moja kwa ubora bado haina uhakika wa kutinga robo fainali(mpaka sasa inahaha kuingia robo fainali).

Labda Mamelodi ndio anaweza kuleta ushindani.
Mnajificha kwenye kichaka cha makundi sasa. Aibu kubwa hii mkuu.
 
Kosa la yanga ni kuleta utoto wa NBC kwenye mechi nene za CAFCL,

mfuatiliaji mzuri wa mpira anakumbuka namna ambavyo wanafainali wa CAFCL msimu uliopita walivyoingia robo fainali, Hii ndio huwa strategy yao,

Mara nyingi al ahly na wydad kwenye makundi wananzaga hivi na mara nyingine humaliza wa pili lakini hao hao ndio wamecheza fainali nyingi

Huku ukileta tamaa ya kufunguka eti ushinde popote yatakutana manene, angali inaowaita wakubwa wote hakuna aliyeshinda wala kufosi kushinda ugenini bali wana relax na kujilinda,

Gamondi anaamini katika kujilinda kwa kumiliki mpira, mbinu ambayo ni rahisi sana kufungika ukikutana na timu inayocheza technically

Nashauri Gamondi abadilishe mfumo wa uchezaji kwenye hizo games, otherwise atawala chenga kisha afungwe yeye
 
Huu ndio ukweli na ndio maana mpaka leo timu namba moja kwa ubora bado haina uhakika wa kutinga robo fainali(mpaka sasa inahaha kuingia robo fainali).

Labda Mamelodi ndio anaweza kuleta ushindani.

Kundi D lina matokeo ya kushtusha hasa mechi hizi za mzunguko wa tatu.
Al Ahly 0 - CRB 0 (Cairo)
Mediama 1 - Yanga 1 (Kumasi)

Binafsi sikutarajia CRB apate Sare hapo Cairo, kwa vile alishafungwa kule Kumasi, Ghana!

Kwa matokeo ya raundi ya tatu, Al Ahly na Mediama kila mmoja amebakiza mechi moja nyumbani na mechi mbili ugenini, ilhali CRB na Yanga kila mmoja ana mechi mbili nyumbani na mechi moja ugenini.

Nikidhani kuna home ground advantage, nawapa nafasi CRB na Yanga kwenda robo fainali, LAKINI kwa ushindani na ubora wa hizi timu zote nne, ni kama kundi bado lipo wazi.

Burudani ziendelee
 
Back
Top Bottom