Kundi lipi lipo upande wa Mungu, Je ni CHADEMA au viongozi wa dini?

Kundi lipi lipo upande wa Mungu, Je ni CHADEMA au viongozi wa dini?

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Viongozi wa dini yaani wakristo na Waislam wakiwemo Mapadri, Mashekh, Wachungaji, Maaskofu wanamuenzi, wanamsifu na kumtukuza Magufuli. Lakini CHADEMA na uongozi wote wa mnanga, wanamponda, wanamtusi na kumkashifu Magufuli.

Kwania njema kama kuna wadadavuaji wa mambo ya imani, ni kundi lipi hapa lipo upande wa Mungu kwani nakumbuka Chadema wenyewe wanamsemo usemao TUNAANZA NA MUNGU NA TUNAMALIZA NA MAUNGU.

Ukijiona ujaelewa au unahasira tulia tu kaa kimya si kutukana majibu ndiyo mjadala tujifunze wote hili tumuelewe huyu Mungu.
 
Ila viongozi wengi wa dini ni wanafiki eti leo wanakemea SASHA kusifiwa wakati kuna mtu aliitwa Yesu wakakaa kimya kama hawakusikia vile.
 
Mungu ndio anawajua waja wake.
Sisi binadamu (maaskofu/chadema/magufuli) ni hatuwezi kumpangia.
Mama anafanya kazi nzuri sana kuliendesha nchi
 
Viongozi wowote wa dini wanasifia na kuabudu watawala ovyo ovyo, wengi ni wanafiki na wezi. Kama huamini chunguza.
 
Kundi lililo upande wa Mungu ni Chadema, viongozi wa dini ,hawa wa bakwata na cct, wapo kwa ajili ya matumbo yao na familia zao.
 
Kwa hiyo " tunaanza na Mungu tunamaliza na Mungu", na kwa title ya thread yako "nani yupo upande wa Mungu", then ukaeleza "viongozi wa dini wanamsifu Magufuli" then "Chadema wanamkashifu",

Unamaanisha kuwa "Magufuli ni mungu??""

Me nimeuliza tu🙉🙉🙉
 
Nanukuu "Usihukumu, utahukumiwa maana hukumu ile utoayo ndiyo utakayopewa na kipimo kile upimacho ndicho utakacho pimiwa" Mwisho wa kunukuu.
 
Samia ndiye rais, hao viongozi wa dini sio wa kuwaamin kirahisi
 
Jibu nimoja tu hapo hakuna kuzunguka mbuyu, viongozi wa dini ndio wapo upande wa Mungu.

Sababu hao unao waita chadema kila siku za ijumaa,juma mosi na juma pili wana kwenda kuongozwa na hao viongozi wa dini jinsi ya kumjua Mungu na kumtumikia.

Full stop.
 
Viongozi wowote wa dini wanasifia na kuabudu watawala ovyo ovyo, wengi ni wanafiki na wezi. Kama huamini chunguza.
Du ila kila dini yaani Quraan na Biblia Mungu amekuwa mkali sana kuwalinda watumishi wake na ametangaza laana ukiwagusa vibaya, vp hapo.
 
Mara mía viongozi wa dini kuliko viongozi wa Chadema

Viongozi hawa wa Chadema walishatuaminisha umma wa Watanzania kwamba Lowassa ni fisadi mkuu na wakamuweka mpaka kwenye ile 'The List of Shame',,, lakini alipokatwa na CCM ktk uteuzi wa ugombea uraisi ghafla Cdm wakamchukua na wakatuambia umma EL sio fisadi tena na kwenye website ya chama ile 'The List of Shame' ikafutwa papo hapo

Kipindi Jk akiwa madarakani viongozi wa Cdm hasa wakiwa bungeni walikuwa wakipiga kelele namna nchi inavyoibiwa kupitia mikataba mibovu ya madini,
Alipoingia JPM madarakani na kuamua kushughulika na mikataba mibovu ikiwemo mpaka kuzuia makontena 270 ya mchanga wa Accacia Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa CDM akasema nchi itashitakiwa MIGA kwa hatua ambazo Serikali inazichukua

Mwanzoni mwa mwaka huu walimtaka Jpm atangaze kwamba nchi ina corona na tuanze kuchukua hatua stahiki ikiwemo social distancing na mengineyo,
Majuzi Mbowe anatoa speech anamtaka Rais Samia aruhusu vyama vya siasa viendelee na mihadhara ya wazi

Yaani ni unafiki, uongo uongo siasa za ujanja ujanja ndio mtaji mkuu
 
Viongozi wa dini Tanzania huwa wako upande wa serikali siku zote.
 
Back
Top Bottom