ni kitu gani hupakwa makwapani ili jasho lisitoke kulowesha Nguo???
MATIBABU YA HARUFU MBAYA YA JASHO/MWILI NA KUTOKWA NA JASHO JINGI
Kutokwa na jasho ni kitendo chema kwa afya na mwili hufanya kwa makusudi mazuri kabisa. Kutokwa jasho kunasaidia mambo yafuatayo
- Kusaidia kupunguza joto na kupoza mwili
- Kusaidia kutoa takataka kutoka mwilini pamoja na maji ya ziada
Hizo ndio sababu baada ya kutokwa na jasho unajihisi mwili kupoa au hata baridi. Pia jasho lina ladha ya chumvichumvi na uchungu, hiyo inatokana na hizo takataka ilizozibeba.
Kwenye kutoka jasho huko kunaweza kukawa na matatizo kidogo hususan kwenye upande wa kiasi na harufu.
SABABU ZA MATATIZO HAYO
Kutokwa na jasho jingi kunaweza kusababishwa na kazi au shughuli anazofanya mtu, aina za vyakula (vyakula vyenye viungo vingi au mafuta mengi nk), magonjwa (mfano mmoja kifuakikuu) na msongo (stress)
Harufu mbaya ya jasho/mwili huweza kusababishwa na uchafu unaotoka na jasho hilo, uchafu wa makwapani pamoja na maambukizi ya vijidudu (bakteria) katika ngozi
MATIBABU YAKE
Kama tunavyosema mara kwa mara, njia nzuri zaidi ya kutibu tatizo ni kujua chanzo chake kisha kuanzia hapo na kuondoa kabisa tatizo hili.
- Kama ni ugonjwa au maambukizi ya vijidudu vya magonjwa basi ni vyema kupata matibabu mazuri ya magonjwa hayo na kisha tatizo hili litaondoka kwa urahisi tu
- Kama ni uchafu ni vyema kujisafisha mara kwa mara kwa kunyoa na kuoga vizuri kwa sabuni inayosaidia kuondoa uchafu vizuri na vijidudu vya magonjwa. Sabuni zenye dawa kama vile Protex (Aina zote), Dettol (Aina zote), Rungu, Family Medicated Soap nk
- Kwa tatizo la jasho jingi unaweza kutumia Antiperspirant na itakusaidia sana. Hiki ni kipodozi maalum kabisa kwa ajili ya kupunguza au kuzuia jasho kutoka. Hupatikana famasi, maduka ya vipodozi na supermarkets
- Kwa tatizo la harufu mbaya ya jasho/mwili unaweza kutumia Deodorant na itakusaidia sana. Hiki ni kipodozi maalum kabisa kwa ajili ya kupunguza au kuzuia kabisa harufu mbaya. Hupatikana famasi, maduka ya vipodozi na supermarkets
Oga vizuri na safisha makwapa yote kwa sabuni yenye dawa, hakikisha makwapa yote hayana nywele kubwa na kisha tumia
deodorant (kama tatizo ni harufu mbaya) au
antiperspirant (kama tatizo ni jasho jingi).