Kunuka kikwapa: Fahamu chanzo, tiba na namna ya kuepuka tatizo

Kunuka kikwapa: Fahamu chanzo, tiba na namna ya kuepuka tatizo

Tumia Deodorant, au pakaa maji ya limao (hii ni kwa mujibu wa Jf Doctors)
 
Niliwahi kusikia lakini sijui kama ni kweli eti dawa ya kienyeji ya kikwapa hata kiwe kikalo vipi inachukua sufuria uliyopikia ugali kisha unailoweka na maji halafu asubuhi unaoga yale maji yaani kama unajikanda sehemu za kikwapa kabla ya kuoga kwa muda wa siku mbili tatu halafu nasikia kinapotea!

Nilisikia watu wanajadili dawa hii baada ya jamaa yangu mmoja kuwa na kikwapa na kushauriwa tumwambie afanye hivyo mambo yatakuwa mazuri!!!!
 
Great Thinkers.

Mimi ni mpenzi wangu leo tuna mwaka na nusu toka tuwe kwenye mahusiano. Lakini napata shida sana kupambana na harufu ya kikwapa chake.

Tumejaribu kutumia kila aina ya vipodozi bado wakati mwingine nakuwa kama nazidisha harufu, mtanisaidiaje ili kikwapa kisiwepo!

Umevumilia mwaka na nusu sasa, kwann usiendelee kuvumilia tu....😛hoto:
 
Great Thinkers.
Mimi ni mpenzi wangu leo tuna mwaka na nusu toka tuwe kwenye mahusiano.
Lakini napata shida sana kupambana na harufu ya kikwapa chake.

tumejaribu kutumia kila aina ya vipodozi bado wakati mwingine nakuwa kama nazidisha harufu, mtanisaidiaje ili kikwapa kisiwepo!

Pole sana, ila kama unampenda kwa dhati hiyo harufu ya kikwapa inabidi ndio uione kama pafyumu, teh teh teh "natania"!

Mmeenda hospitali? Inabidi uvumilie hiyo hali huku mkiendelea kutumia tiba mbalimbali. Ila hii thread ungeipeleka JF Doctors ungepata msaada wa madaktari.

Mwambie ajaribu kupaka limao kwenye kwapa nasikia husaidia kukata harufu ya ngwapa!
 
Labda ana nywele za kwapani kama anazo awe ananyoa coz huwa sometimes zinasababisha harufu ya kikwapa.
 
Mwanzoni ulikua husiiikiii harufu umeanza mchoka ndo waleta hapa toka
 
Mwambie apunguze kula mayai na awe anakunywa maji mengi. Pia akioga achukue limao akamue maji yake apake kwenye makwapa mara nyingi kadri awezavyo kitaisha. Ulete feedback akifanikiwa!

UOTE=Chinchilla;2878120]Great Thinkers.
Mimi na mpenzi wangu leo tuna mwaka na nusu toka tuwe kwenye mahusiano. Lakini napata shida sana kupambana na harufu ya kikwapa chake.

Tumejaribu kutumia kila aina ya vipodozi bado wakati mwingine nakuwa kama nazidisha harufu, mtanisaidiaje ili kikwapa kisiwepo![/QUOTE]
 
Great Thinkers.
Mimi na mpenzi wangu leo tuna mwaka na nusu toka tuwe kwenye mahusiano.
Lakini napata shida sana kupambana na harufu ya kikwapa chake.

tumejaribu kutumia kila aina ya vipodozi bado wakati mwingine nakuwa kama nazidisha harufu, mtanisaidiaje ili kikwapa kisiwepo!

Msugulie ndimu kutwa mara tatu kabla na baada ya kukoga. Ukiona haijakata baada ya wiki aanze kuosha kwa siki nyeupe "white vinegar" kutwa mara tatu na aendelee na kusugulia ndimu, ndimu unaikata kati na kila kipande kimoja unasugulia kwapa moja.

Pole sana, hilo ni tatizo linalotibika na si la kudumu.

Lakini hakikisha huyo mpenzi wako ni mume/mke wako wa halali, kama unakula vya haramu basi hicho kikwapa ndio hakikatiki.
 
Niliwahi kusikia kuwa maji ya limao ni dawa nzuri
 
Great Thinkers.
Mimi na mpenzi wangu leo tuna mwaka na nusu toka tuwe kwenye mahusiano. Lakini napata shida sana kupambana na harufu ya kikwapa chake.

Tumejaribu kutumia kila aina ya vipodozi bado wakati mwingine nakuwa kama nazidisha harufu, mtanisaidiaje ili kikwapa kisiwepo!

Paka kwenye kikwapa ndimu au limao baada ya kuoga
 
Tuacheni utani jamani. Mpenzi wako aende kununua ndimu kwa ajili ya 'kikwapa' chako..dah lol

Hata wageni wakiuliza. eti hizo ndimu ni za uji? Unaweza kuhisi 'wana ku enjoy ' lol
 
Jasho la mtu halinuki, kinachosababisha harufu ni byproduct inayotokana na maisha ya bacteria. Njia ya kwanza ya kupambana na kikwapa ni usafi. Anyoe makwapa kila mara, aoshe na sabuni walau mara tatu kutwa. Ndimu na white vinegar, kama acid inasababisha pH kuwa ndogo na hivyo kusababisha bakteria kufa.

Kama ulivyoambiwa sugua na ndimu ama vinegar b4 kuoga na ukishaoga futa kwapa vema na kisha tumia deodorant. Kwa kweli harufu ya kikwapa inakera, mkipambana nayo itaisha tu! kila la kheri
 
Mimi nadhani mwambie azidishe round za kuoga. Kama alikuwa anaoga mala moja kwa siku basi at least iwe mala tatu kwa siku. Japo hakiwezi kwisha lakini kitapungua
 
Mimi kwa uzoefu wangu. Watu wenye tatizo la kunuka midomo, kikwapa na miguu

Tatizo lao sugu ni kuwa 'hawapati' watu wa kuwaeleza ukweli.

Wengi hawajijui.
 
Mwambie achukue pamba awe analowesha kwenye spirit halafu aweke kwenye hayo makwapa yake na abana kwa dakika kazaa. Fanyeni hivyo kila siku kwa muda wa wiki 2.
 
Caution: Kamwe sirudie nguo bila kufua. Na asitumie deodorant kama hajatoka kuoga. Kuna watu wana tabia ya kutembea na deodorants kwenye handbags sijui wanatumiaje!
 
Kama ulivyoambiwa sugua na ndimu ama vinegar b4 kuoga na ukishaoga futa kwapa vema na kisha tumia deodorant.

Siyo tu atumie deodorant. Anachotakiwa kutumia ni 48 hr clinical strength ANTI-PERSPIRANT deodorant. Kuna tofauti baina ya deodorant na ANTI-PERSPIRANT deodorant.

Mtu mwenye tatizo kubwa la kikwapa deodorant pekee haitasadia kuondoa tatizo. Inapaswa atumie deodorant zinazokata utokwaji wa jasho kwenye kwapa na hizo ndiyo ANTI-PERSPIRANT deodorants.

Baadhi ya watu huwa hawajui hilo. Wakiona tu container lina neno deodorant basi anakimbilia kununua. Sasa deodorants zisizo na anti perspirant ingredients huwa haziko effective kwa watu wenye vikwapa vinavyotema na ndiyo maana utakuta watu wanalalamika kuwa wamejaribu kutumia deodorant lakini wapi.

Ni muhimu sana kusoma ni deodorant ya aina gani mtu unanunua. I always recommend ANTI-PERSPIRANT deodorants.
 
Back
Top Bottom