Kununua gari toka Zanzibar

Mwonekano wa Xtrail unavutia sana lakini kumbe ni kama Honda CR-V ukinunua jiandae kufugia sungura
Honda ndio sio gari kabisa, watu walizikurupukiaga CR-V zilivyotoka new model zikaanza kuwafia vibaya mno. Watu hawana hamu nazo kabisa.
 
Boss! Nimeipenda hiyo umeongea kisomi sana. Kuna rafiki yangu alinunua extrail bush tu zikaisha kununua ilikuwa majanga. Wakati za noa au ist ni 20 to 50.



Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaosifia hizo Nissan ujue hayajawakumba mazito. Kubadilisha engine oil, plug na matairi sio complicated sana. Kimbembe gari ilete technical failure na jinsi nissan ilivyo na umeme na ma sensor kila mahali ndio hapo mtu atapoelewa somo. Nissan ni gari nzuri kwa wenye residual income sio watu wa kudunduliza hela.

Tulikuwa na Nissan Terrano ikaleta shida ya suspension halafu ni zile za upepo electronically controlled, picha linaanza inatakiwa uzinunue kwa pair. Mbona ilikuwa kimbembe aisee. Hela iliotumika kui service ilikuwa ni mishahara ya miezi kadhaa ya watoa comment humu. Nikajiuliza tu je ingekuwaje hii gari anaimiliki mtu kama Mwalimu wa sekondari au bank teller?
 
Asante sana mkuu. Paper work sina shaka nayo. Nina wasiwasi na gharama za TRA. Isijenigharimu zaidi. Kwani Dar zipo nyingi ila naangalia ahuweni ya gharama.
Mwambie mje kuuziana ikishafika Dar. Kuwa mjanja saa mbaya
 
Sawa inategemea na kipato ndg.nawewe unatumia mazingira gani off road au?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Semawew mkulu wengine tunaambiwa mara mafundi garage oooh hatujamiliki hata bajaji hahaha.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kununua nenda na documents za gari TRA Znz watakupa gharama unazotakiwa kulipia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
XTRAIL ni nzuri kama mtunzaji lakini hiyo sita mbona unapata hata hapa DSM .
 
Na ukute mbuzi kapona teh teh.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Honda ndio sio gari kabisa, watu walizikurupukiaga CR-V zilivyotoka new model zikaanza kuwafia vibaya mno. Watu hawana hamu nazo kabisa.
Honda CR-V sijui watu wanazipendea nini. Labda ubadilishe engine iwe 1MZ
 

ilikua gar gani mkuu na ilitumika mda gan zanzibar!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nissan ni kizungu zungu asee. Mi ninayo Fuga naendesha pale ninapotaka Show-off (kwenye sherehe au ninapoenda kung'oa demu mpya) vinginevyo nakwea daladala
 
Hivi kaka kufungua website ya TRA nayo ni kazi kuipata... www.tra.go.tz? ukiingia huko utapata kila kitu
Sawa Mkuu, Kama website ya TRA Ipo basi hata Ya Nissan Ipo, Usingemjibu hata Hiyo ungeweka Website, Mbona Ukaelezea kwa Kina hali Ukijua anaweza pata kwenye Website??

Haya Mambo ni kuelekezana tu ndugu yangu, tena kwa Upole.
 
Nissan ni kizungu zungu asee. Mi ninayo Fuga naendesha pale ninapotaka Show-off (kwenye sherehe au ninapoenda kung'oa demu mpya) vinginevyo nakwea daladala
Hahahahaaa! Asante kwa kunichekesha bure. Maana nsikia kuna watu wanalipaga kiingilio kwenda kucheka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…